Facebook Comments Box

Wednesday, March 4, 2015

SERIKALI YASITISHA MATUMIZI YA TIKETI ZA KIELEKRONIKI KATIKA UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM

TIKETI ZA KIELEKRONIKI ZILIZO SITISHWA NA SERIKALI

Serikali imesitisha matumizi ya tiketi za kielektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia (Machi 3, 2015) hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.

Uamuzi huo umetangazwa Machi 3, 2015 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB.

 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


KAPTENI KOMBA AZIKWA KIJIJINI LITUHI HUKU RAIS JAKAYA KIKWETE AKIONGOZA MAZISHI HAYO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, aliungana na mamia ya waombolezaji kumzika Mbunge wa Jimbo la Nyasa na msanii mahiri wa muziki nchini, Mheshimiwa Kepteni John Damiano Komba, kwenye makaburi ya Kanisa Katoliki katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma. 

Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, akitokea Dar es Salaam, kiasi cha saa tano na robo asubuhi, Rais Kikwete alikwenda moja kwa moja Lituhi, karibu kiasi cha kilomita 140 kutoka mjini Songea, kwa ajili ya mazishi ya Mheshimiwa Komba ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Rais Kikwete alijiunga na waombolezaji akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kiasi cha saa tisa mchana kwa ajili ya mazishi hayo. 
 
Shughuli za mazishi za kidini ziliongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga.

Mwili wa Marehemu Komba uliteremshwa kaburini saa 9:30 mchana huku ukishuhudiwa na mjane wa marehemu Salome Komba na watoto wake 11. 

Rais Kikwete ameondoka Lituhi mara baada ya mazishi kurejea mjini Songea kumalizia ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Ruvuma.



SOMA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 03-03-2015



























 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU