Waziri wa Maliasili na Utalii - Mh. Khamis Kagasheki
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Mh. Shamsi Vuai Nahodha
Waziri wa Mambo ya Ndani - Dk. Emanuel Nchimbi
Waziri Mkuu - Mh. Peter Pinda
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini.
Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa,kubakwa,kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa na uporaji.
Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, akitoa utetezi wake, akidai kuwa ameonewa na kamwe hawezi kujiuzuru.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki zichukuliwe. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa amekutaja kuwa ni muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Amebainisha kuwa hata baada ya kuongea na Rais, Mkuu wa nchi huyo ameridhia tume iundwe na kila aliyehusika awajibike.
Amesema Rais ameshauri kutengua uteuzi wa mawaziri wote wanne ( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Wazir wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo, na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki) kama ambavyo wabunge walivyopendekeza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe James Lembeli alisema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.
Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.
Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha. Spika amuomba Mwanasheria mkuu kutumia kifungu kuongeza muda. Naye ameomba kuundwa tume ya kisheria ya mahakama.