Wednesday, January 9, 2013
CCM WAKANUSHA TUHUMA ZA BAVICHA
SIKU
moja baada ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Bavicha), kudai CCM inashirikiana na baadhi ya viongozi wake kukisaliti
chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amekanusha tuhuma
hizo.Nape alisema CCM haihusiki na mgogoro wowote ndani ya chama hicho,
hivyo wanapaswa kumtafuta mchawi wao siyo kukilaumu chama chake.
“Mchawi
wanaye wenyewe ndani ya chama chao, hatuhusiki na lolote hivyo
wanapaswa kujipanga na kuulizana kubaini tatizo linalowasumbua,”
alisema.
Aliongeza kuwa CCM haina muda wa kuhujumu chama hicho, ila wana muda wa kutekeleza ilani za chama maeneo mbalimbali nchini.
Nape alisema kutokana na hali hiyo, CCM imejipanga kuhakikisha ahadi zinatekelezwa kwa vitendo, ikiwamo maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.Baadhi ya viongozi wa Bavicha wanaodaiwa kushirikiana na CCM kudhooficha Chadema na wengine walifukuzwa uanachama
SAKATA LA BASHE NA MEMBE LAFIKIA PATAMU
MGOGORO wa makada wawili wa CCM; Benard Membe na Hussein Bashe umechukua sura mpya, baada ya mbunge huyo wa Mtama, kukiomba chama hicho tawala kuingilia kati ili kuupatia suluhu.
Mvutano wa Bashe na Membe ulianza wakati wa kampeni za uchaguzi wa ndani wa CCM hasa uchaguzi wa NEC baada ya Bashe kumtuhumu Membe kwa mambo mbalimbali ikiwamo kukigawa chama.
Kauli hiyo ya Bashe ilimkera Membe ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa akisisitiza kuwa atamshughulikia mwanasiasa huyo chipukizi wa CCM ili amtambue.
“Nitashughulika na Bashe ndani ya chama kwa maana ya kumfikisha kwenye kamati zetu, ili ayaeleze vizuri ambayo amenipakazia na kunichafua sana… Lakini mambo mengine ambayo yamekaa kijinai sasa hayo ndiyo nitakayoyapeleka mahakamani,” alisema Membe baada ya taarifa hizo.
Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa Membe amemwandikia barua Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phillip Mangula kumwomba amtake Bashe athibitishe kauli zake mbalimbali dhidi yake.
Moja ya mambo Membe anamtaka Bashe ayathibitishe ni kwamba waziri huyo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kuwahi kusema kuwa akiwa Rais, atawafukuza watu kumi na moja nchini ambao anaamini kuwa siyo Watanzania, “Barua hii ina tuhuma nyingi, lakini kikubwa mheshimiwa huyo (Membe) amekiomba chama kimtake Bashe athibitishe tuhuma zake dhidi yake, ikiwamo hili la kuwafukuza Watanzania 11,” kilidokeza chanzo chetu cha habari ndani ya CCM.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa baada ya makamu mwenyekiti huyo kupata barua ya Membe, ameipeleka katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa hatua zaidi. Habari zimeeleza kuwa tayari Kinana ameifanyia kazi barua hiyo kwa kumwandikia barua Bashe ili ajibu tuhuma zinazomkabili ifikapo kesho Januari 10.
Nakala ya barua hiyo ya Kinana imetumwa kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Nzega ambako Bashe anatokea akiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kupitia wilaya hiyo, “Tayari Bashe ameandikiwa barua na CCM kumtaka ajibu malalamiko hayo ya mwenzake Membe,” kilieleza chanzo hicho cha habari.
Membe hakupatikana kwa siku tatu mfululizo, ili azungumzie suala hilo baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana na taarifa zilizopatikana ofisini kwake, zimeeleza kuwa yuko likizo jimboni kwake Mtama, Lindi.
Bashe hakuthibitisha wala kukanusha kupata barua hiyo ya CCM inayomtaka ajibu madai ya Membe, badala yake akasema: “Membe aliahidi kunishughulikia na mimi ninangoja anishughulikie.”
Mangula alipotafutwa juzi kuzungumzia suala hilo alisema asingeweza kusema chochote kwa kuwa alikuwa hajafika ofisini tangu alipokwenda kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, “Sijajua chochote kilichoendelea ofisini kwa sababu nilikuwa kijijini kwangu kwa ajili ya Sikukuu ya Krimasi na Mwaka Mpya. Nikiingia ofisini naweza kuwa katika nafasi ya kujua kilichoendelea,” alisema Mangula. Hata hivyo, alipopigiwa simu jana, iliita bila kupokewa na baadaye ikazimwa kabisa.
Kinana naye hakupatikana jana baada ya simu yake pia kuita na kupokelewa na mtu mwingine mara kadhaa ambaye alieleza kuwa alikuwa mkutanoni siku nzima.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alijibu kwa kifupi na kukata simu,” Sijapata wala kuona barua ya malalamiko ya Membe kwa Bashe.”
Novemba 10, mwaka jana Bashe akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, alimtuhumu Membe akidai kuwa ndiye anayehusika na vipeperushi vya kumhujumu mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete vilivyokuwa vimetawanywa na watu wasiojulikana siku chache kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti na nafasi nyingine kufanyika.
HII NDIO SIRI YA FAST JET KUWA NA BEI RAHISI
Mfumo huu wa gharama nafuu katika mashirika ya ndege umekuwa maarufu sana ndani ya mabara ya Ulaya, Asia na Marekani kwa zaidi ya miaka 10. Kwa uhakika, Easyjet, ni moja kati ya mashirika ya gharama nafuu na ni shirika kubwa sana katika bara la Ulaya (ambaye mwanzilishi wake na mwanahisa mkubwa wa fastjet) na kubeba zaidi ya abiria milioni 55 ndani ya mwaka huu
Ni jinsi gani tunaweza kupata nauli chini mno?
Kuna njia kuu tatu tunazotumia kuwezesha nauli za ndege kuwa chini. Kwanza, tunaajiri watu wajanja na werevu, tunatumia mifumo na mikakati ambayo hupunguza gharama na kuongeza ufanisi wa kazi – hii hufanyika nyuma ya pazia na hutoweza kuona ikifanyika. Pia tunanunua sarafu yetu na mafuta ya ndege kabla, ili kuweka gharama zetu chini. Pia tunazingatia kwenye aina moja ya ndege, ambayo ni Airbus 319 katika kampuni yetu, hii inapunguza gharama pia kwani tuna aina moja ya vipuri na wataalamu wa ndege.Njia mbili zingine utakazo zigundua, Kwanza, tunatumia mbinu ya 'lipia unachotumia' katika usafiri wetu wa anga.
Hii inamaanisha abiria analipia anachotumia wakati wa safari na si zaidi.
Unapolipia tiketi zetu unakuwa umelipia pamoja na siti kwenye ndege na mizigo moja wa kubeba mkononi. Kila kitu kingine cha ziada kwanzia gharama ya mizigo hadi vinywaji - vitalipiwa kwa kutumia Mfumo wa” kulipa-kwa-matumizi”. Kama unataka chakula unaweza kulipa, na kama huhitaji chakula huna haja ya kukilipia. Katika mashirika mengine ya ndege unalazimika kulipia huduma ambazo hata hutotumia, mfano unakuta ndege zingine zina madaraja na huduma za gharama, lakini kwa fastjet tunatoa bidhaa zetu kwa gharama rahisi sana unaweza kulipia huduma Fulani kama unaitaka, kama huduma ya basi.Njia ya tatu na mwisho tunayotumia kuifanya nauli yetu iwe chini ni kwa kuweka madaraja katika nauli zetu. Nauli zetu zinapatikana kati ya dola $ 20-150: Fanya mipango yako ya safari mapema, upate nauli ya chini. Hii inatusaidia kujaza ndege zetu (ni zaidi ya gharama nafuu) pia tunawapa fursa wateja wetu kupata bei nafuu sana, kinachotakiwa ni kufanya maandalizi ya safari mapema. Tumekuwa sana katika soko la Tanzania na tumefanikiwa kuwapa fursa maelfu ya watu ambao hakuwahi kusafiri kwa anga.
Mfumo wa Gharama nafuu ni muhimu sana kwa fastjet. Nauli zetu si tu za utangulizi, tunaahadi kuwa na nauli nafuu kadri tuwezavyo na kwa muda mrefu. Lengo letu ni kuanzisha aina ya usafiri wa anga wa gharama nafuu katika bara la Afrika kama ambavyo mabara ya Ulaya na Marekani wamekuwa wakifurahia huduma hii kwa miaka mingi.
Kusafiri kwa anga si tu kwa ajili ya matajiri na watu maarufu, Mfumo wetu wa nauli ya chini ina mpa kila mmoja fursa ya kusafiri kwa anga.
Tunapenda kuuita "Usafiri Makini"
Subscribe to:
Posts (Atom)