Facebook Comments Box

Saturday, April 6, 2013

HUU NDIO MSIMAMO WA ZITTO KUHUSU KESI YA RWAKATARE

Kutokana na sakata la Lwakatare na Barua ambayo ilidaiwa kuandikwa na zitto Mwenyewe kuzaga mtandaoni hasa kwa mara ya Kwanza kupitia kwenye mitandao ya kijamii Zitto amejitokeza na kutoa taharifa hifutayo…..

1. Niliandika barua kwa Katibu Mkuu wa chama mnamo tarehe 15 Machi 2013 kutaka chama kifanye uchunguzi wake wa ndani kuhusiana na ukweli wa video iliyowekwa kwenye mitandao inayoonyesha kuwa Kiongozi wetu mwandamizi anapanga mipango ya kumdhuru Mhariri wa moja ya magazeti hapa nchini. Sikuamini kabisa mambo yale na hivyo kutoa ushauri kwa chama kwamba tufanye uchunguzi wetu wa ndani ili kujiridhisha. Uchunguzi wa ndani ungetufanya kuweka mikakati wa namna bora zaidi ya kulinda chama dhidi ya njama zozote, za ndani au za nje ya chama.

2. Mapendekezo yangu ndani ya chama kamwe hayakulenga kumtosa ndugu Lwakatare wakati huu anakabiliwa na changamoto hii bali yalilenga kuhakikisha kuwa wakati tunamlinda na kumtetea ili haki itendeke, lazima tuhakikishe kuwa chama hakitaathirika na sakata hili kwa namna yeyote ile. Ni jukumu letu kuhakikisha sura (image) ya chama inabakia salama maana hatujui mikakati (game plan) ya maadui zetu kisiasa hasa baada ya kauli zao kwamba chama kitakufa kabla ya 2015 ambayo imerudiwa rudiwa sana. Ni lazima kutilia shaka (doubt) kila linalotokea sasa kwa kulipima kwa jicho la mbele zaidi. Ikumbukwe maneno ya Mwenyekiti wetu “Mwenyekiti Freeman Mbowe anataka ikithibitika kuwa Lwakatare alishiriki kurekodi mkanda huo iwe kwa kurubuniwa, ‘kushikishwa’ au kuingizwa mkenge, itamlazimu kuwajibika kwa kosa la kukosa umakini” (Gazeti la Jamhuri).

3. Barua ile ya tarehe 15 Machi 2013 ilikuwa ni ya ndani ya chama, haikuwa ya kiofisi bali ya Zitto Kabwe kwa chama, ilisainiwa na haikukusudiwa kuwa ‘public’. Nimeshangazwa sana kusikia na baadaye kuona barua yenye maudhui kama yale yale ya barua yangu kwa Katibu Mkuu imewekwa mtandaoni. Barua imewekwa masaa machache baada ya kikao cha Kamati Kuu kwisha ambapo tuliweka msimamo wa pamoja wa chama juu ya namna bora ya kushughulikia suala la Lwakatare kama chama. Wakati mweka barua anadai kuwa kulikuwa na mgawanyiko katika kikao, ukweli ni kwamba ajenda hiyo haikuwa na mjadala wenye mgawanyiko kabisa na msimamo wa chama ulipatikana kwa mwafaka bila mgawanyiko. Ni dhahiri kuwa maadui zetu walitaraji mgawanyiko na baada ya kushindwa sasa wanatengeneza mgawanyiko huo kwa kusambaza uwongo wenye uzandiki.


4. Baada ya kufanya uchunguzi mdogo nimegundua kuwa ID iliyoweka video ya Lwakatare mtandaoni na ID iliyoweka barua hii mtandaoni ni IDs za mtu mmoja. ‘Coincidence’ ya namna hii inashangaza na kushtusha, lakini inatuambia jambo moja kubwa ‘kwamba kuna kirusi ndani ya chama kilicho karibu sana na viongozi wa chama chenye kazi moja tu, yani kuonyesha kuwa CHADEMA hapako shwari, kuna migogoro na hatimaye kusambaratisha chama’. Kirusi hiki lazima kina nafasi andamizi au kipo karibu sana na viongozi waandamizi. Inawezekana kabisa kirusi hiki kinahusika na suala zima la Lwakatare katika kupanga, kuendesha na kutekeleza mpango mzima. Maswali kama ‘kwanini Dennis Msacky na Zitto ndani ya Video ya ‘Lwakatare’ lazima sasa yaanze kutafutiwa majawabu.

5. Natoa wito tena kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kwamba, huu ni wakati wa kuwa na umoja na mshikamano kuliko wakati wowote ule katika uhai wa chama chetu. Chama cha Mapinduzi kitatumia njia zote kutugawa, kutugombanisha na kupenyeza chuki miongoni mwetu katika juhudi za wao kubakia madarakani. Umakini wa Kiongozi huonekana wakati wa changamoto kama hizi!

6. Msimamo wa chama umetolewa na Kamati Kuu iliyomaliza vikao vyake jana siku ya ijumaa tarehe 5 Aprili 2013. Huo ndio msimamo wangu pia! Kesi ya Lwakatare ipo mahakamani, chama kimeonyesha dhahiri kumwamini Jaji aliyekabidhiwa kesi hii, sasa tuache mahakama ifanye kazi yake na tusubiri hukumu. Msemaji wa chama kuhusu suala hili ni ndugu Tundu Lissu na amekuwa akitoa ufafanuzi kila inapohitajika.

Asanteni


Kabwe Z. Zitto,MP- Kigoma North, Tanzania. Chairman Public Accounts Committee,
Deputy Secretary General CHADEMA and Deputy Leader of the Opposition,
Shadow Minister of Finance
Mobile: +255756809535
Blog: http://www.zittokabwe.com

AHUKUMIWA MIAKA KUMI JELA KWA KUMNYONYA MTOTO ULIMI

MAHAKAMA Hakimu ya Mkazi ya Wilaya ya Mpanda imemhukumu Kassim Lugendo (41) mkazi wa kijiji cha Kambanga tarafa ya Kabungu kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kumnyonya ulimi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, anayesoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula, bila ridhaa yake.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alitoa hukumu hiyo jana baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Awali katika kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa Lugendo alitenda kosa hilo Machi 30 mwaka jana, saa sita mchana akiwa nyumbani kwake.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mtoto huyo alikuwa akitoka shuleni akielekea nyumbani kwao ndipo mshitakiwa alipoona anapita karibu ya nyumba yake ambapo alimwita msichana huyo na kisha alimwingiza kwa nguvu nyumbani kwake.

Mbwijo aliiambia mahakama kuwa, baada ya mshitakiwa kumwingiza ndani ya nyumba yake msichana huyo, alianza kumnyonya ulimi kwa nguvu huku akimtomasa sehemu za siri kwa vidole.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa wakati akimfanyia uovu huo, mtoto huyo alikuwa akiomba msaada kwa kupiga kelele muda ambapo majirani walifika eneo la tukio na kumkuta mshitakiwa akiwa ameshaanza kumvuta mtoto huyo sketi yake ya shule.

Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ulileta mahakamani hapo mashahidi watatu na mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote.

Akijitetea, Lugendo aliiomba mahakama isimpe adhabu kwa kile alichokieleza kuwa yeye ana familia ya watoto saba na wazazi wake wote wawili ni walemavu, hivyo ana watu wengi wanaomtegemea.

Hata hivyo, Hakimu Chiganga alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa ni cha kinyama na hatari kwani kina weza kumsababishia mtoto huyo ugonjwa wa ukimwi. Alimtia hatiani na kumwadhibu kifungo cha miaka kumi jela. SOURSE: HABARI LEO

MALAWI WAAMBIWA WAACHE KUTAPATAPA


 
Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wapili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu tamko la Serikali juu ya mgogoro wa mpaka wa ziwa Nyasa. 

SERIKALI ya Tanzania imeomba  Malawi iache kutapatapa kuhusu mgogoro wa mipaka wa ziwa Nyasa kufuatia Rais  wa nchi hiyo, Joyce Banda kutangaza katika  baadhi ya vyombo vya  habari  kuwa atapeleka  suala hilo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki(ICJ), badala yake isubiri uamuzi wa jopo la usuluhishi lifanye kazi na litoe maamuzi.
Aidha serikali  imesema kuwa hata siku moja  haijapelekewa taarifa wala nyaraka za siri kutoka kwa Katibu wa jopo hilo, ambalo linahusisha marais wastaafu wa zamani wa Afrika na wanasheria  kama ilivyodaiwa  na  Rais  Banda katika vyombo hivyo , kuwa kuna Mtanzania anayeitwa Dk. John Tesha ambaye wanaamini ametoa  habari na kuiba nyaraka za siri.
Akilitolea ufafanuzi   jambo hili, Waziri Membe amesema kuwa  Tanzania na jopo hilo   limestushwa juu ya madai hayo na hatua ya Rais Banda kupoteza imani.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU