Facebook Comments Box

Tuesday, August 27, 2013

ZITTO: SITOGOMBEA URAIS WALA UBUNGE 2015

Photo: Zitto: Sitogombea Urais wala Ubunge 2015

- Asema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili
- Adai ni bora akalime michikichi kuliko kuendelea kushiriki siasa...

Endelea kusoma zaidi => http://bit.ly/1cbWgRh
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu  siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.

Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).

"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.

Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kama atagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani.

Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.

Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.

Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.

Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.


PICHA: SAMAKI SAMAKI MBEZI - MAKONDE YATEKETEA KWA MOTO


Kiota cha starehe jijini Dar es Salaam maarufu kama Samaki Samaki tawi la Mbezi leo kimeteketea kwa moto.Moto huo umesababishwa na shoti ya umeme.





WANAUME WAWILI WAKUBALIANA KUOA MKE MMOJA


Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao walioamua kugawana mke mmoja.

Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda Wamesaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao. Ameeleza BBC kwanini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.
Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.
Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.
Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wako tayari kumtolea mahari.
Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.
Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angelifunga nao ndoa bila ya wao kujuana.
Lakini walipogunduana , ilikuwa ni ugomvi wa mara kwa mara lakini mwanamke huyo alipoambiwa amchague mnmoja wao, alishindwa. Akasema anawapenda wote wawili.
Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa 'kwenda kumjulia hali.'
Vile vile mkataba huo unawashurutisha kugawana majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.

CHANZO: BBC SWAHILI


CCM WAMFUKUZA UWANACHAMA MBUNGE WAO

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.


 HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemaliza kikao chake cha siku tatu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ikiwa imeridhia mapendekezo kadhaa ya Kamati Kuu ya CCM, ikiwemo kumfuta uongozi Mbunge wa jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar, Mansor Yusuf Himid. 

 Kufuatia hatua hiyo, CCM itatoa taarifa kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi kuondoa udhamini wake kwa mwanachama huyo kama Mjumbe wa Baraza hilo kwa jimbo la Kiembesamaki.

 Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

 Hatua hiyo itamfanya Spika wa Baraza hilo kutangaza kiti cha jimbo hilo kuwa wazi na kuitishwa uchaguzi mdogo wa kugombea nafasi hiyo.

 Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa Daud, Ismail akizungumza na Zenji FM radio amesema kikao hicho kimefikia uamuzi huo baada ya kupokea madai ya mkoa wa Magharib kutaka mwanachama huyo afukuzwe kwa madai ya kupinga sera ya Serikali mbili ya Muungano inayoungwa mkono na CCM. 

 Hata hivyo Himid ambaey pia ni mjume wa kamati ya maridhiano Zanzibar, endapo hajaridhishwa na uamuzi wa kufukuzwa kwake anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo.

 Himid aliwahi kuwa Waziri asiekuwa na Wizara ya Maalum katika awamu ya saba ya uongozi inayongozwa na Dk Ali Mohammed Shein. Pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo kabla ya kuwa Waziri wa Maji Ujenzi, Nishati na Ardhi katika Utawala wa rais Amani Abeid Karume. 

Himid alionekana kichocheo kutaka kuliondoa suala na mafuta na gesi asilia kwenye orodha ya Mambo ya Muungano pamoja na kuchukizwa na matatizo ya Muungano yanayoikandamiza Zanzibar. 

Hivi karibuni mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, Mzee Hassan Moyo alisema kufukuzwa kwa Himid hakutathiri shughuli za Kamati hiyo katika kutetea Muungano wa mkataba. 

UTEUZI 

 Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). 

 Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi. 

Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa. 

Pia, NEC imeridhia mapendekezo ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo. 

 Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita). 

Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

 Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera. 

 Taarifa Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC 

Ndugu Ashura Amanzi 
Ndugu Rukia Saidi Mkindu
Ndugu Elias J. Mpanda
Ndugu Jonathan M. Mabihya 
Ndugu Mulla Othman Zuberi 
Ndugu Jumanne Kapinga
Ndugu Ali Haji Makame
Ndugu Jacob G. Makune 
Ndugu Juma A. Mpeli
Ndugu Hawa Nanganjau
Ndugu Abdulrahman Shake 
Ndugu Subira Mohamed Ameir 
Ndugu Abdallah Shaban Kazwika 
Ndugu Juma Bakari Nachembe 
Ndugu Josephat Ndulango 
Ndugu Rajab Uhonde
Ndugu Abeid Maila 
Ndugu Mohamed Lawa 
Ndugu Mariam Sangito Kaaya 
Ndugu Bakar Lwasa Mfaume 
Ndugu Julius Peter 
Ndugu Jumanne Kitundu Mginga 
Ndugu Mathias Nyombi 
Ndugu Mohamed Hassan Moyo


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU