Facebook Comments Box

Tuesday, March 19, 2013

MCHOMA MKAA ACHINJWA MVOMERO - MOROGORO, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA UTAKAZOZIONA



 MTU mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Gole John 'Moto' Mkazi wa kitongoji cha Lumanile eneo la Wami Dakawa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro amechinjwa kama mbuzi na watu wasiojulikana.


LWAKATARE ASOMEWA MASHITAKA MANNE YA UGAIDI NA KUNYIMWA DHAMANA


Wakili wa Lwakatare, Tundu Lisu (kulia) akimuelekeza jambo Mbuge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati wakijaribu kuandaa mipango ya dhamana.
 Lwakatare akionesha alama ya vidole viwili wakati akipelekwa kizimbani.
 
Wakili Peter Kibatara akiweka mambo sawa kabla ya kuanza kumtetea Lwakatare.



Wanachama na mashabiki wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili kabla ya kesi kuanza.
 
Wakili Nyaronyo Kicheere akimuelekeza jambo Godbless Lema baada ya kesi kuahirishwa, kulia ni Tundu Lisu.

Wanachama wa Chadema wakiwa wametawanyika nje ya mahakama baada ya kesi kumalizika.
  Lwakatare akipelekwa rumande baada ya kunyimwa dhamana.
 
Mke wa Lwakatare akitahayari baada ya mumewe kunyimwa dhamana.



Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatale akiwasalimia wafuasi wa chama hicho kwa ishara ya vidole viwili baada ya kuwasili katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Picha zote na Jackson Odoyo




Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Chadema Wilfred Lwakatale akiwa chini ya ulinzi mkali wa Askari Polisi baada ya kutinga katika Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu
SOURCE:DJ-SEK


MWANAUME ANATARAJI KUFANYIWA UPASUAJI AWEKEWE UUME


 
Historia mpya inakaribia kuandikwa duniani baada ya mwanaume ambaye anajulikana kwa jina Andrew Wardle, kutoka Stalybridge, Greater Manchester huko Uingereza ambaye alizaliwa bila uume, kufanya mpango wa kutengenezewa na kuwekewa kiungo hicho kwa njia ya upasuaji.

Mwanaume huyu ambaye kwa sasa anaumri wa miaka 39, anatarajiwa kuwa mwanaume wa kwanza kabisa duniani kufanyiwa upasuaji kama huu na ajabu zaidi ni kwamba, kiungo hiki kitatengenezwa kutoka sehemu ya mkono wake.


MTOTO WA RAIS KUSHITAKIWA



 

Saif al-Islam Gaddafi, ambaye ni mtoto wa pili wa Gadaffi amekuwa akishikiliwa na vyombo vya usalama vya Libya tangu Novemba 19, 2011 baada ya kukamatwa wakati akijaribu kukimbia nchi hiyo baada ya kuuawa kwa baba yake na kaka yake, Mtassim Gaddafi.

Mahakama ya Afrika inayoshughulikia haki za binadamu yenye makao yake Jijini Arusha imeamuru  Serikali ya Libya kuendesha kesi inayomkabili mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gadaffi kwa uhuru na haki.

Saif al-Islam Gaddafi, ambaye ni mtoto wa pili wa Gadaffi amekuwa akishikiliwa na vyombo vya usalama vya Libya tangu Novemba 19, 2011 baada ya kukamatwa wakati akijaribu kukimbia nchi hiyo baada ya kuuawa kwa baba yake na kaka yake, Mtassim Gaddafi, Oktoba 20, 2011.
Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika yenye makao makuu mjini Addis Ababa, Ethiopia ndiyo iliyowasilisha shauri hilo kwenye Mahakama ya Afrika kwa kuwa Serikali ya Libya haijaridhia mikataba ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Kutokana na hali hiyo, hata familia ya Gadaffi ilishindwa kufungua kesi hiyo kwani taasisi au watu binafsi wa Libya hawana uwezo wa kisheria wa kufungua kesi kwenye mahakama hiyo kutokana na kikwazo cha Serikali yao.

Shauri hilo lenye namba 002/2012 lilisikilizwa na majaji kumi na moja walioongozwa na Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Sophia Akuffo kutoka Ghana, Ijumaa iliyopita.
Wengine waliokuwemo kwenye jopo hilo ni pamoja na Makamu wake, Jaji Fatsah Ouguergouz, Jaji Mkuu wa zamani, Augustine Ramadhan pamoja na Majaji Sylvain Ore, Duncan Tambala, Gerald Niyugeko, Bernard Ngoepe, Elsie Thompson, Hadji Guisse, Kimelabalou Aba na Ben Kioko.
Jopo hilo la majaji pia limeiamuru Serikali ya Libya kuruhusu ndugu, jamaa na marafiki wa mtuhumiwa huyo kumtembelea kipindi chote shauri dhidi yake linaposikilizwa.
Serikali ya Libya imetakiwa kutoa taarifa mahakamani kuhusu utekelezaji wa amri hiyo siku 15 tangu kupokelewa kwa nakala ya hukumu.
Familia ya Gadaffi imekuwa haifurahishwi na mwenendo wa kesi ya  Saif huko Libya.


ONYO KUHUSU MATANGAZO YA KAZI KWENYE BLOG NA TOVUTI


TAARIFA KWA UMMA
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29 (1).

Ni vyema tufahamu kuwa chimbuko la Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma limetokana na maboresho yanayoendelea katika Utumishi wa Umma nchini.  Ambapo miongoni mwa maboresho hayo ni pamoja na marekebisho ya Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1998 toleo Na. 2 la mwaka 2008 ambapo katika Vifungu Na. 4.6  na 6.6. vya Sera hiyo ambavyo vimetamka kuwepo kwa chombo maalum cha kushughulikia mchakato wa masuala ya ajira katika Utumishi wa Umma.

Kwa mujibu wa Sheria, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ndio chombo pekee chenye wajibu wa kutekeleza  majukumu yafuatayo:-
i)        Kutafuta wataalam wenye ujuzi maalum na kuandaa mfumo wa kuhifadhi taarifa za wataalam.
ii)      Kutangaza nafasi wazi za kazi zinazojitokeza katika Utumishi wa Umma.
iii)    Kuhusisha wataalam maalum ili kushirikiana nao kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji.
iv)    Kuwashauri waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa ajira.
v)      Kuandaa orodha ya wahitimu wa Vyuo na wataalam weledi kwa madhumuni ya kurahisisha rejea za ujazaji wa nafasi za ajira katika Utumishi wa Umma.

Aidha, kwa mujibu wa Sera hiyo, kuwepo kwa chombo hiki kutaziwezesha Mamlaka za Ajira nchini (zikiwemo zile za Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa) kubaki na majukumu yake ya msingi (Core functions) ambayo yameainishwa katika uundaji wa Mamlaka hizo ili kuongeza ufanisi.

Kutokana na maelezo hayo hapo juu ni vyema wananchi wote wakafahamu kuwa ni kosa kwa mtu au taasisi yeyote ile kuchukua Matangazo ya Sekretarieti ya Ajira na kuyafanyia marekebisho au kuandaa matangazo mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kupotosha umma ilihali wakijua wazi kuwa taarifa hizo wanazozichapisha au wanazoziandika katika mitandao ya kijamii hazijatolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Tumefikia hatua ya kusema haya kutokana na baadhi ya taarifa zinazohusu mchakato wa ajira hususani uwepo wa nafasi za kazi zilizopo katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira ametoa matangazo hayo.
Moja ya tangazo hilo  la kughushi na lenye nia ya kupotosha umma ni lile lililoko katika anwani hii www.eastafricajobscareer.com lenye kichwa cha habari kinachosomeka “Tangazo la Kazi Utumishi Tanzania June 2013” ambalo linaonyesha “Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Juni, 2013”.

Katibu anapenda kuwasisitizia wadau wote wa Sekretarieti ya Ajira wanaotafuta kazi pindi wanapoona matangazo katika Vyombo mbalimbali vya Habari wajiridhishe kwa kuthibitisha taarifa hizo kama ni za kweli kwa kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz kwa taarifa sahihi zihusianazo na ajira katika Utumishi wa Umma.

Sekretarieti ya ajira haiwajibiki na wala haitawajibika kwa Matangazo ama taarifa zozote zinazohusiana na mchakato wa ajira  katika Utumishi wa Umma ambazo haijazitoa rasmi.

Imetolewa 18 Machi, 2013 na

Katibu,
Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Maktaba Kuu ya Taifa/Barabara ya Bibi Titi Mohammedi
S. L. P 63100, Dar Es Salaam.

Simu; +255 22 2153517
Nukushi; +255 22 2153518
Barua pepe: katibu@ajira.go.tz
Tovuti; www.ajira.go.tz

Aidha, kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz  au Simu; 255-687624975

Source:WAVUTI


DAVID KAFULILA NA NCCR WAPATANA




MBUGE wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. David Kafulila, amekiri kufanya kosa la utovu wa nidhamu ndani ya chama hicho na kusababisha uongozi kutaka kumvua uanachama.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Samuel Ruhuza, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika katika Kata ya Nguruka Mkoani Kigoma ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.

Alisema pamoja na Bw. Kafulila kukiri kosa na kuomba radhi, wananchi jimboni kwake na viongozi wa chama hicho walikiomba chama kimsamehe ili wasiweze kupoteza jimbo hilo.

“Hoja ya viongozi na wananchi ni kwamba, Bw. Kafulila bado anakipenda chama hiki ambacho ataendelea kukitumikia ili kutetea masilahi yao,” alisema Bw. Ruhuza na kuongeza kuwa, ugomvi uliokuwepo kati ya mbunge huyo na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Bw. James Mbatia haupo tena.

Aliwataka wananchi na viongozi wote wa chama hicho jimboni humo kumpa ushirikiano Bw. Kafulila ili aweze kutetea masilahi yao kikamilifu.

“Mheshimiwa Kafulila alikaa, kutafakari na kugundua kuwa alichokuwa anakifanya si sahihi hivyo aliamua kuomba radhi lakini kabla ya kusamehewa, alipewa masharti ya kutimiza vigezo ili msamaha wake uweze kukubaliwa, hadi sasa tayari ametimiza masharti yote kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama chetu,” alisema.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU