![]()  | 
| Yaya Toure na Aisha | 
Aisha Dalal amekuwa msichana mdogo wa kwanza wa Kiingereza (Mascot) kuingia na wachezaji mpira Uwanjani akiwa amevaa Hijabu katika ligi kuu ya Nchini Uingereza.
Aisha
 aliyekuwa ameshikwa mkono na nyota wa mchezo huo Yaya Toure wakati wa 
kuingia uwanjani ilikuwa ni mechi baina ya timu za Manchester City na Liverpool iliyochezwa Agosti 26 mwaka huu. Matokeo ya mechi hiyo Man city walishinda 3-1.
"Ilikuwa ni kupata uzoefu kwangu na nilifurahia sana siku hiyo", alisema Aisha kuliambia Gazeti la Lancashire Telegraph.
"Wachezaji
 walikuwa marafiki mno kwetu na kutufanya tujisikie kama tupo nyumbani",
 alisema Aisha ambaye alikuwa na kaka yake mdogo aitwaye Khalil 
aliyeshikwa mkono na Samir Nasir wakati wa kuingia Uwanjani.
Aisha anasema walikuwa na bahati kwa kuwa waliruhusiwa kuchagua wachezaji waliotaka kuingia nao Uwanjani. 
Anasema
 kaka yake Khalil alichagua kuingia Uwanjani na Samir Nasri kwa kuwa 
ndiye mchezaji anayempenda na yeye alimchagua Yaya Toure.
Anaendelea
 kuhadithia Aisha kwamba Yaya Toure alikuwa mtu mzuri sana kwake kwani 
kabla ya kuingia alikuwa akimtoa woga kutokana na kelele kubwa za 
mashabiki.
Aisha
 anasema kuvaa kwake hijabu kulikuwa ni jambo muhimu sana na alijisikia 
ujasiri kufanya hivyo kwani hakuna aibu katika kudhihirisha imani yako 
popote pale ulipo.



















