Facebook Comments Box

Thursday, September 4, 2014

MTUHUMIWA WA UGAIDI AONESHA ALIVYO LAWITIWA NA POLISI

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MMOJA wa watuhumiwa wa ugaidi katika kesi
inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na
Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), amevunja ukimya mahakamani baada ya kuonyesha suruali ilivyolowa kwenye makalio akisema ni madhara ya kulawitiwa na kuingizwa miti na polisi.

Mshtakiwa huyo, Salum Ally Salum, aliamua kufanya hivyo jana ili kuithibitishia mahakama kile walichodai ni unyama waliotendewa na polisi wakati wakihojiwa.
“Mheshimiwa hakimu, angalia (anageuka na kuinua suruali katika eneo la makalio), haya ndiyo madhara niliyopata kwa kuingiliwa nyuma na kuingizwa jiti,” alidai.

Baada ya mshtakiwa huyo kuzungumza, Hakimu Hellen Riwa alimshauri kutoa taarifa kwa uongozi wa Magereza ili aweze kupata matibabu ya haraka kwani akiendelea kukaa hivyo anaweza kupata madhara makubwa.
Kwa upande wake, Sheikh Farid, alimuomba Rais
Jakaya Kikwete kuunda tume huru ya kuchunguza vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa.

Sheikh Farid aliieleza mahakama kuwa Tanzania
hakuna ugaidi, na kwamba balaa hilo lisiombwe
kutokea hapa nchini. Alisema kuwa yanayowakuta hivi sasa ni kutokana na
kudai mamlaka ya nchi yao kwani kuna mgogoro
mkubwa unaoendelea. Sheikh Farid alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, wakati kesi yake na wenzake 19 ilipokuwa ikitajwa na kuunganishwa na washtakiwa wengine wawili, Sheikh Mselem Ali Mselem na Abdallah Said Ali.
“Mheshimiwa Hakimu, naomba mahakama ikunjue kifua itusikilize tunayotaka kusema, tunataka ufafanuzi kutoka kwako, kwanza nathibitisha kwamba madhila, unyanyasaji, ukatili tulifanyiwa na polisi wakati wa mahojiano.
“Tatizo letu mheshimiwa ni matibabu, gerezani hakuna matibabu, kuna wenzetu tangu tulipoingia humo miezi miwili sasa, wanalala hospitali, dawa hakuna, inafikia hatua tunaagiza kutoka nje.
“Mheshimiwa hali ni mbaya, watu wanatokwa hadi na usaha, yote hayo ni kwa sababu ya ukatili waliotufanyia polisi, tutakapokwenda katika Mahakama Kuu ya Tanganyika iliyovaa koti la Tanzania tutazungumza mengi.

“Tunahitaji iundwe Tume Huru ya Uchunguzi,
tunaomba Rais Kikwete aunde tume yenye haki, tume ndiyo itatoa ukweli, hiki ndicho kilio chetu.
“Niliuliza hapa mahakamani Zanzibar ni nchi? Yule rais ni rais wa timu ya mpira?” alihoji Sheikh Farid.
Alidai sheria ya ugaidi ni sheria ya dhuluma ambayo ipo kwa ajili ya kuwanyonga Waislamu na kwamba kuna mgogoro mkubwa wa Utanganyika.

“Tanzania hakuna ugaidi hapa, tusiombe balaa hilo, sisi kosa letu ni kudai mamlaka ya nchi yetu,” alidai.
Hakimu Riwa akijibu hoja ya Sheikh Farid, alisema mahakama imewaruhusu kuandika barua kuomba kuundwa kwa tume huru kisha mahakama itajua pa kuipeleka.

Kabla ya kuwasilisha hoja hizo za malalamiko,
washtakiwa walibadilishiwa mashtaka na kusomewa upya mashtaka manne na mawakili wa Serikali, Peter Njike na George Barasa.
Inadaiwa katika shtaka la kwanza, washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maaeneo mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, walikua njama na kuingiza watu nchini kushiriki vitendo vya kigaidi.

Katika shtaka la pili, washtakiwa wote wanadaiwa kuwaingiza watu nchini kushiriki vitendo vya ugaidi huku wakijua ni kosa.
“Mheshimiwa, shtaka la tatu linamkabili mshtakiwa Farid na Mselem, mnadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014, maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mliwaajiri Sadick Absaloum na Farah Omary kushiriki kutenda vitendo vya kigaidi.

“Shtaka la nne linamkabili Farid, unadaiwa kuhifadhi watu waliotenda vitendo vya kigaidi, huku ukijua ni kosa. Ulimuhifadhi Sadick Absaloum na Farah Omary huku ukijua kwamba walitenda ugaidi,” alidai Balasa. Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote, upelelezi wa kesi haujakamilika. Mahakama iliahirisha kesi hiyo
hadi Septemba 17, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally, Juma Juma.
Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour
Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro, Said Sharifu, Sheikh Mselem Ali Mselem na Abdallah Said Ali.

 CHANZO: MTANZANIA


AKAMATWA BAADA YA KUJIFANYA AFISA USALAMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
02/09/2014
 
ANAYEJIFANYA AFISA USALAMA WA TAIFA ANASWA DAR ES SALAAM

Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam kutokana na makosa mbalimbali ya kujifanya ni mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Mtu huyo anayejulikana kwa jina la GUNNER S/O SAIMON MEENA, Miaka 40, Mkazi wa Kinyerezi Segerea anatuhumiwa kuwasumbua wafanyabiashara mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa kuwasingizia au kuwatuhumu kwamba wanahusika na makosa yenye kuhatarisha usalama.

Kwa muda mrefu Jeshi la Polisi limekuwa likimtafuta mtu huyo kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza na uchunguzi unaonyesha kwamba jina lake halipo katika orodha ya watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale
alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aitwaye ABDI S/O MOHAMED DALMAR. Katika tishio hilo la kutishia mtuhumiwa GUNNER S/O SAIMON MEENA ambaye ni Afisa Usalama feki alidai apatiwe kiasi cha fedha za kitanzania T SHS 25,000,000/= (SHILINGI MILLIONI ISHIRINI NA TANO) ama sivyo angechukuliwa
hatua chini ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Mlalamikaji alitoa taarifa na ndipo mtuhumiwa
akakamatwa katika mtego wa Polsi. Uchunguzi zaidi wa shauri hili unafanyika na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya jalada la kesi yake kupitiwa na mwanasheria wa Serikali.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


MAGAZETI YA LEO: ALHAMISI 04/09/2014




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU