Tuesday, February 12, 2013
RAIS KIKWETE ATAMBULISHA WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM NA KUMPOKEA JULIANA SHONZA
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia
wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kuwatambulisha wajumbe wapya wa
Kamati kuu ya CCM ilkiyofanyika katika viwanja vya Makao makuu ya CCM
mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCm Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM nje ya ukumbi wa White
House,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na waliokuwa viongozi
waandamizi wa CHADEMA.Kushoto anayevaa kofia ya CCM ni aliyekuwa mgombea
Ubunge jimbo la Mbozi Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA Bwana Mtela
Mwampamba na kulia ni Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana
CHADEMA Bi Juliana Shonza.Weninge katika picha ni Katibu mkuu wa
CCMNdugu Abdulrahman Kinana(kulia) na kushoto ni Makamu Mweyekiti wa CCM
Bara Ndugu Philip Mangula.(picha na Freddy Maro).
TFF WAOMBA YANGA WAWASHANGILIE SIMBA NA AZAM KWENYE MECHI ZA KIMATAIFA
Release No. 026
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 12, 2013
WASHABIKI WAZIUNGE MKONO AZAM, SIMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linawaka washabiki wa mpira wamiguu kujitokeza kwa wingi
wikiendi hii kuzishangilia timu za Azam na Simbazitakazocheza mechi za
mashindano ya Afrika jijini Dar es Salaam.Nguvu ya washabiki ni muhimu katika
kuziweza timu hizo kufanya vizuri katikamechi hizo za nyumbani dhidi ya Al
Nasir Juba ya Sudan Kusini na Club Liboloya Angola.Azam itacheza Jumamosi (Februari
16 mwaka huu) dhidi ya Al Nasir katikamechi ya Kombe la Shirikisho wakati Simba
itaikabili Club Libolo kwenyemechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika
Jumapili. Mechi zotezitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
LYON, YANGA KUUMANA UWANJA WA TAIFA
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara inamalizaraundi ya 16 kesho (Februari 13 mwaka huu)
kwa mechi kati ya wenyejiAfrican Lyon dhidi ya Yanga itakayochezwa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.Mechi hiyo itakayochezshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka
Morogoroinakutanisha timu zenye mazingira tofauti. Wakati Yanga wakiwa ndiyo
vinarawa ligi hiyo kwa pointi 33, African Lyon ambayo sasa inanolewa na
SalumBausi inakamata mkia ikiwa na pointi tisa tu.Nayo Toto Africans
itaikaribisha Polisi ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCMKirumba jijini Mwanza
katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi JacobAdongo kutoka Musoma. Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga wenye uwezo wakuchukua watazamaji 20,000 utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya MgamboShooting na Oljoro JKT.Nahodha wa zamani wa
Taifa Stars, Mecky Maxime ambaye sasa ni kocha waMtibwa Sugar ataiongoza timu
yake hiyo katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Manungu ulioko
Turiani, Morogoro. Ni kwenye uwanja huo ambapo Mtibwa Sugar katika mechi yao
iliyopita walichapwa mabao 4-1na Azam.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
USIWE NA HARAKA YA KUHUKUMU MAMBO
Katika dirisha lile la treni,ndani yake
Alikuwa kakaa mzee mmoja na kijana wake,
Ambaye alikuwa na makamu ya umri wa miaka 25.
Yule kijana akaanza kuonesha usoni mwake
alaza za furaha na mshangao.
Akatoa mkono wake dirishani,kisha akaurudisha
Haraka na kusema kwa sauti ya juu:
Baba angalia miti yote yakimbia kurudi nyuma!!
Yule mzee akatabasamu na kuonesha ya kwamba
Anaungana na mwanae katika furaha.
Kando yao walikuwa wamekaa wanandoa wawili.
Na wakisikiliza mazungumzo kati ya baba na mtoto.
Wakawa wakihisi aibu na kushikwa na mshangao,
Vipi kijana huyu mwenye makamo ya umri wa miaka 25
Anafanya vitendo kama vya mtoto mdogo???
Ghafla yule kijana akapiga kelele akisema:
Baba angalia umeme wa radi!
Angalia mawingu yanakwenda pamoja na treni!
Wanandoa wawili wakaendelea kushangaa!
Kulingana na mazungumzo na vitendo
Vya yule kijana.
Kisha mvua ikaanza kunyesha,na matone ya maji
Yakatua katika mkono wa yule kijana,ambaye
Alikuwa akionesha alama ya furaha katika uso wake.
Akapiga kelele kwa mara nyingine na kusema:
Baba mvua inavyesha !!! Na maji yamegusa mkono wangu !!!
Baba angalia !!!
Mara hii wanandoa walishindwa kujizuia,
Wakamuuliza yule mzee:
Mzee kwa nini humpeleki kijana wako hospitalini,
Ili aweze pata matibabu???
Yule mzee akawajibu:
Hivi sasa ndio twatoka hospitalini,
Na mwanangu ndio ameanza kuona kwa
Mara ya kwanza katika maisha yake.
******************************
Siku zote usiwe ni mwenye kutoa
Majibu ya mambo mpaka ujue uhakika wake.
Na daima uwe ni mwenye dhana nzuri
Kwa ndugu zako.
WAJUMBE 14 WA KAMATI KUU YA CCM
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake
cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma,
pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe
14 wa Kamati Kuu yake.
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM.
Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-
Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara
1. Ndugu Pindi Chana
2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Slaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira
Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM.
Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-
Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara
1. Ndugu Pindi Chana
2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Slaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira
Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud
MADAKTARI KUPIGA SIMU BURE
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif
Rashid(katikati),Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya
Mwakifulefule (kulia) Mkurugenzi wa Shirika la Switchboard Ali Block
wakionesha mabango ikiwa ni inshara ya uzinduzi wa kuwawezesha wahudumu
wa Afya na madaktari kuwasiliana kwa simu za mkononi bure,huduma hiyo
inatolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la
Switchboard ili kurahisisha huduma za kiafya mahosipitalini.Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid
(kushoto)Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule
(katikati)pamoja na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum
Mwalim,wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwawezesha
wahudumu wa Afya na madaktari kuwasiliana kwa simu za mkononi bure
huduma hiyo inatolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la
Switchboard ili kurahisisha huduma za Afya mahosipitalini.Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)