Thursday, June 6, 2013
MAREKANI WAANDAA SHERIA ITAKAYO KATAZA WATU KUVAA MLEGEZO
Sina
shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume zenye
majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa majina
lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio.
Kama
ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha miili yao
hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa wakilalamikiwa kwa
style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana wadogo
ambao bado wako shuleni.
Katika hali
ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya makalio uongozi wa
Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria mpya itakayoweza
kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa mlegezo na kukatiza
mitaani.
Sheria
hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali, kaptura, mavazi ya kuogelea na
sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni mwa mvaaji.
Mayor wa
Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia waandishi wa habari kuwa
amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana wanaotembea makalio
nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.
HII NDIO KAULI YA M 2 THE P BAADA YA KUFIKA TANZANIA KUMZIKA MANGWEA
Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini
Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani
Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya
leo (June 6).Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2
The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa
nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake
Mangwea. “Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P
nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili
Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi
changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea
asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi,
asanteni,” alisema. Msikilize hapa
PICHA ZA UTOAJI WA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU MANGWEA MOROGORO
Meza kuu
hii ikiwa ni maandalia ya kuuwaga mwili wa msanii marehemu Albert
Mangwea aliyefariki dunia na anatarajiwa kuzikwa leo mkoani
morogoro.Utaratibu huu umeandaliwa katika uwanja wa jamuhuri mkoani
morogoro kwa lengo la kuwapa fursa wakazi wa mji huo kupata nafasi za
kuuwaga mwili huo kabla ya maziko
Umati
mkubwa wa wakazi wa morogoro waliojitokeza katika zozi za kuwaga mwili
wa msanii huyo mchana huu kabla ya maziko yake leo.Marehemu albert mangwea alifariki wiki
iliyopita nchini afrika kusini na maziko yake yatafanyika leo mkoani
hapa.
Mama Mzazi wa Mangweha, Denisia Mangweha akiwa nyumbani kwake kabla ya safari kuelekea Uwanja wa Jamhuri.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera asubuhi hii amefika nyumbani kwa Mama
Mangwea eneo la Kihonda Mazimbu Road na kumpa pole kwa niaba ya wakazi
wote wa mkoa wa Morogoro. Baada ya kutoa pole, Mhe. Bendera aliongoza
umati wa watu kutoka Kihonda kuelekea Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli za
kuaga mwili wa Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei 28 mwaka huu nchini
Afrika Kusini. Mangwea anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kihonda
nje ya Kanisa la Mtakatifu Monica jirani kabisa na alipozikwa baba yake
mzazi Mzee Keneth Mangwea.
MAJANGA YAZIDI MUANDAMA MR. NICE SASA MKATABA WAKE NA GRAND PA RECORDS YA KENYA WAVUNJWA
Mwanamuziki aliyevumbua staili ya muziki ya TAKEU (Tanzania Kenya Uganda), Mtanzania Lukas Mkenda aka Mr Nice amepoteza mkataba wake na kampuni ya kurekodi muziki ya nchini Kenya, kwa kile kilichoelezwa na kampuni hiyo kuwa ni tabia ya Mr Nice ya uvivu, ulevi, asiyeaminika na asiye na ushirikiano.
Zaidi ya maandishi yaliyoandikwa na GrandPa Records kwenye ukurasa wao wa Facebook, pia wamezungumzia suala hilo walipohojiwa na kituo cha EA Radio ambapo wamesema Mr Nice amesema ataendelea kubaki mjini Nairobi nchini Kenya akitafuta kujiweka sawa.
Subscribe to:
Posts (Atom)