Sunday, February 17, 2013
MBELA ASKARI ALIEKATWA MIKONO ANATUMIA MIGUU KULIMA
PAMOJA na kuwa na ulemavu wa kutokuwa na mikono yote miwili, Salim Mbela mkazi wa eneo la Delux, nje kidogo ya mji wa Songea, amefanikiwa kulima shamba la mahindi kubwa na zuri kwa kutumia miguu yake.
Ukiliona shamba hilo la Mbela licha ya kuwa na mahindi, pia lina maharage, magimbi na ndizi yaliyostawi na kupendeza.
Huwezi kuamini kuwa shamba hilo linalimwa na Mbela, ambaye ni mlemavu kwa kutumia miguu yake.
Ulemavu huo umemkuta na kulazimika kulima kwa
miguu, baada ya kukatwa mikono yake alipokuwa akidai kurejeshewa mahari
kutoka kwa wakwe zake.
Mbela anasema kuwa pamoja na ulemavu alioupata
ukubwani, hawezi kutembea mitaani kuomba omba, wakati bado mwili wake
una viungo vingine anavyoweza kuvitumia kujipatia mahitaji yake ya kila
siku.
Kilichosabisha kukatwa mikono
Mbela alizaliwa miaka 53 iliyopita akiwa na mikono miwili na mwenye afya tele, lakini misukosuko ya maisha imemfanya leo abaki hana mikono yake miwili, huku akiishi peke yake.
Mbela alizaliwa miaka 53 iliyopita akiwa na mikono miwili na mwenye afya tele, lakini misukosuko ya maisha imemfanya leo abaki hana mikono yake miwili, huku akiishi peke yake.
Anaeleza kuwa kabla ya kuwa mlemavu, aliwahi
kuajiriwa na Jeshi la Polisi, akifanyia kazi Kituo cha Polisi Makuyuni
mkoani Arusha miaka ya nyuma, lakini alicha kazi hiyo baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Baada ya hali hiyo, aliona bora arudi nyumbani kwao Kijiji cha Malumba wilayani Tunduru ili kuendelea kupata matibabu.
Mbela anasema kuwa alipofika kijijini kwao, aliendelea kupata matibabu na baadaye akapona.
Akizungumza kwa kusaidiwa na rafiki yake wa karibu ambaye amejitambulisha kwa jina la Zacharia Dikala, maarufu kama Babu Masai, Mbela anasema kuwa alikutana na matatizo ya kukatwa mikono miaka minne iliyopita.

Mbela ambaye pia ni baba wa watoto Mwanabibi Salim
(28), Siku Salim (19) na Said Salim (24) anaeleza kuwa akiwa na mkewe
na familia yake, siku moja ali kwenda nyumbani kwa wakwe zake waliokuwa
wakiishi katika kijiji hicho cha Malumba na kuchukua mbuzi wake aliotoa
mahari miaka ya nyuma wakati akimchumbia mkewe ambaye ndiye aliyemzalia
watoto hao.
Anasema kuwa wakati huo alikuwa na nguvu na
alitumia mabavu kufanya fujo, hadi akafanikiwa kufika zizini na kupora
mbuzi, bila kujua kama maisha yake yange badilika na kuishia pabaya.
Hata hivyo, anajutia kitendo hicho akisema kwamba iwapo angefahamu mapema yataka yomkuta, asingethubutu kwenda kufanya fujo hizo.
Hata hivyo, anajutia kitendo hicho akisema kwamba iwapo angefahamu mapema yataka yomkuta, asingethubutu kwenda kufanya fujo hizo.
“Nilikuwa najiamini sana, nilikuwa na nguvu sana,
nikaamua kwenda ukweni kwangu kufuata baadhi ya mifugo yangu, niliyotoa
mahari wakati namposa mke wangu,” anasimulia na kuongeza:
CHUO CHA ST JOHN'S DODOMA CHAFUNGWA BAADA YA WANAFUNZI KUGOMA
Chuo
Kikuu cha St John’s cha mkoani Dodoma kimefungwa baada ya wanafunzi
kususia mitihani wakituhumu na kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa na
wahadhiri kwa kuwangusha kwenye mitihani na baadhi kuwabaka wanafunzi wa
kike.
Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Gabriel Mwaluko, wanafunzi zaidi ya 290 wamesimamishwa masomo baada ya kukiuka sheria na kugomea mitihani, hivyo chuo kimefungwa kikisubiri taratibu za kinidhamu kuchukuliwa.
Awali uongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo ulieleza kuwa wanafunzi 290 wa St John’s na vyuo vikuu vishiriki vya Dar es Salaam walisimamishwa masomo huku uongozi wa chuo ukiwapa barua za kuwaondoa chuoni kuanzia wiki hii.
Habari hizo zilisema wanafunzi 196 wanaosoma Dodoma na wengine 94 wanaosoma katika vyuo vishiriki vya St. Mark's na Town Centre vya jijini walipewa barua za kuondolewa chuoni.
Rais wa serikali ya wanafunzi, Andrew Chiduo, akizungumza na NIPASHE Jumapili, alisema hatua ya kuwasimamisha inalenga kuwatisha ili kuendelea kuwalinda walimu wanaodaiwa kuwanyanyasa na kuwadhalilisha na kwamba wanasusia kufanya mitihani inayofanyika mwezi huu. Alisema wahadhiri wanalazimisha kufanya ngono na wanafunzi wa kike, kuwabaka na wale wanaokataa wanaangushwa kwenye mitihani.
Alisema katika tukio la hivi karibuni muhadhiri (jina tunalo) alituhumiwa kumbaka mwanafunzi baada ya kumhadaa kumpa mitihani mingine baada ya kushindwa ile aliyofanya mhula uliopita. Alisema wamelazimika kugomea mitihani baada ya mhadhiri mmoja (jina linahifadhiwa) kuwafelisha kwa makusudi wale wanaochukua kozi ya biashara wa mwaka wa kwanza huku akiwapa vitisho.
Akijibu tuhuma hizo Profesa Mwaluko alisema madai ya mwalimu kumbaka mwanafunzi yanachunguzwa kwa kuwahusisha polisi, kadhalika alisema mhadhiri anayetuhumiwa kuwafelisha wanafunzi madai yake yanafuatiliwa pia.

HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOPIGWA MOJA NA LIBOLO
Ngassa akimtoka beki wa Libolo, Antonio Cassule |
Haruna Chanongo wa SImba akipasua katikati ya wachezaji wa Libolo |
Ngassa akimtoka Cassule |
Ngassa na Cassule |
Kiungo wa Simba SC, Amri Kiemba (kushoto) akiwania mpira dhidi ya beki wa Libolo, Pedro Ribeiro kulia |
Simba na Libolo wakiingia uwanjani |
Kikosi cha Libolo leo |
Simba wakiomba dua na nyuma yao ni Libolo pia wakiomba dua |
Kikosi cha Simba SC leo |
Wachezaji wa Simba SC wakiwapungia mikono mashabiki wao kabla ya mechi |
Mrisho Ngassa akipiga krosi baada ya kufanikiwa kumtoka beki wa Libolo |
Kipa wa Simba, Juma Kaseja akienda kuokota mpira nyavuni baada ya Libolo kufunga bao |
Libolo wakiwapungia mikono mashabiki wao baada ya mechi kuwashukuru kwa kuwashangilia |
Haruna Moshi 'Boban' (kushoto) akipiga shuti mbele ya beki wa Libolo |
Beki wa Simba, Juma Nyosso akimiliki mpira mbele ya beki wa Libolo |
Haruna Chanongo akipasua katikati ya mabeki wa Libolo |
Kiungo wa Libolo, Manuel Lopez akiondoka na mpira baada ya kumzidi maarifa Mwinyi Kazimoto wa Simba SC |
Manuel Lopez kulia akigombea mpira na Mwinyi Kazimoto wa Simba SC kushoto |
Mwinyi Kazimoto akigombea mpira wa juu na kiungo wa Libolo |
Beki wa Simba SC, Shomary Kapombe akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Libolo |
Haruna Moshi 'Boban' akimtoka beki wa Libolo |
Amri Kiemba akimtoka beki wa Libolo |
Mwinyi Kazimoto wa Simba akigombea mpira wqa juu na kiungo wa Libolo |
HAKI YA KUCHINJA WANYAMA: DESTURI ILIYOPO IENDELEE - WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ameagiza kuundwa kwa kamati maalumu itakayohusisha pande mbili za waumini wa dini ya Kiislam na Kikristo, ili ishughulikie mgogoro mbichi unaohusu haki ya kuchinja wanyama.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana alipofika mkoani Mwanza na kufanya kikao -kilichodumu kwa saa tano- na wawakilishi wa madhehebu ya dini hizo mbili ikiwa ni hatua ya kutafuta njia ya kutatua mgogoro wa nani mwenye haki ya kuchinja wanyaka kati ya waumini wa dini hizo mbili.
Kwa wakati huu, Waziri Mkuu amesema shughuli hiyo iendelee kufanywa kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa desturi zilizokuwepo hadi hapo yatakapofikiwa na kutolewa maagizo mapya.
Waziri Mkuu ameagiza kamati hiyo ifanye shughuli zake na kuwasilisha ripoti yake Serikalini haraka iwezekanavyo kwa ajili ya hatua zaidi za kimaamuzi.
Hata hivyo, hadi Waziri Mkuu anaondoka katika kikao hicho, Waislam waliridhia kuundwa kwa Kamati hiyo wakati Wachungaji na Mapadre walikataa.
Waziri Mkuu alikumbushia kuwa suala hili ni la kiimani na ijapokuwa Serikali haina dini, wananchi wake wanazo imani kwa mujibu wa dini zao hivyo ni vyema Wachungaji, Mapadre na Masheikh wakawasihi waumini wao kuwa na subira hadi hapo utakapopatikana ufumbuzi mwingine.
Waziri Mkuu pia ameonya kuhusu redio mbili ambazo zimenyooshewa vidole na waumini wa pande zote mbili kuwa zinachochea uhasama wa kidini. Akazitaja kuwa ni redio Imani iliyopo Morogoro na redio Neema iliyopo mkoani Mwanza na kuzionya kuhusu mafundisho yake ambayo ikilazimu, Serikali itachukua hatua dhidi yake.
PADRE MUSHI APIGWA RISASI NA KUFA LEO ASUBUHI
Taarifa
kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati
kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi
wa Kanisa la Parokia ya Minara Mirefu huko Zanzibar amepigwa risasi
majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.
Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.
Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.
Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.
Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.

Subscribe to:
Posts (Atom)