Mwenyekiti
 wa Chama cha Mapinduzi (CCM},Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma 
Kikwete leo wameongoza Matembezi ya Mshikamano yaliyoanzia kwenye eneo 
la Mnarani na kuishia kwenye ofisi za CCM mkoani Kigoma,asubuhi ya leo. 
Matembezi hayo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Chama cha 
Mapinduzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,Rais Jakaya Kikwete {wa pili 
kushoto}na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya mshikamano 
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama cha 
Mapinduzi {CCM} yanayofanyika leo kwenye uwanja wa Lake 
Tanganyika,Mkoani Kigoma.Matembezi hayo hayo yamehudhuliwa na viongozi 
mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla.