Facebook Comments Box

Thursday, September 25, 2014

CHUO CHA IMTU CHAFUNGWA NA TCU

TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Imekifungia kwa mda,Chuo kikuu cha tiba na Sayansi IMTU kutofanya udahili kwa Wanafunzi wapya wa Mwaka wa Masomo 2014-2015,kutokana na chuo hicho kukiuka sheria ya inayosimamia Vyuo Vikuu nchini.

Uamuzi huo wa kikifungia Chuo hicho
Umetangazwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Profesa Magishi N Mgasa wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari ambapo alisema maamuzi hayo yamefikiwa baada kikao cha Dharura kilichoitishwa na (TCU) wiki iliyopita na kujadili taarifa ya timu iliyotathimini chuo hicho, Ambapo kikao hicho kikabaini mapungufu makubwa katika chuo cha IMTU yakiwemo matatizo ya uongozi,kukosa wahadhiri wakutosha na wenye sifa,kutokuwepo na Vifaa pamoja na kudahili wanafunzi bila hata kuwa na taratibu zilizowekwa na tume.

Profesa Mgasa alisema kwa kufanya hivyo chuo cha IMTU imekiuka sheria ya namba 5(1),sura ya 346 ya sheria za Tanzania ambayo inakitaka chuo Kikuu chochote kufuata taratibu zilizowekwa na tume.
Vilevile Profesa Mgasa alizidi kusema baada ya Tume kubaini makosa hayo,ndipo wamefikia maamuzi ya kukifungia chuo cha IMTU kufanya
udahili kwa wanafunzi wapya wa Mwaka
2014-2015,mpaka pale itakakapo rekebisha mapungufu yaliyotajwa na Tcu.

Pia tume imetoa notsi ya miezi 3 kwa chuo cha IMTU,kuanzia tarehe 16 mwezi huu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na endapo chuo hicho kikikaidi basi TCU haitosita kuwachukulia hatua kali ikewemo hata kukifungia kabisa.
Aidha Profesa Mgasa aliwataka wanafunzi nchini wasijiunge na chuo Kikuu chochote bila ya kufuata maelekezo kutoka Tume ya vyuo Vikuu
nchini (TCU).


DOWNLOAD RASIMU YA KATIBA MPYA INAYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAAALUM

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta

 Mambo yameiva, na hii hapa ndiyo Rasimu ya Tatu ya Katiba, ambayo inapendekezwa na Bunge Maalum. 

Vipengele vingi vimebadilishwa. Haya hapa ni mambo ya Muungano:

Mambo ya Muungano
 
1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3. Usalama na usafiri wa anga.

4. Uraia na uhamiaji.

5. Jeshi la Polisi.
 

6. Sarafu na Benki Kuu.

7. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na Mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania na zinazosimamiwa na Idara ya Forodha.

8. Mambo ya nje.

9. Usajili wa vyama vya siasa.

10. Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani.

11. Elimu ya Juu.

12. Baraza la Taifa la Mitihani na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.

13. Utabiri wa hali ya hewa.
 

14. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano. 
 

DOWNLOAD/IPAKUE MWENYEWE HAPA: RASIMU YA TATU

DEREVA TAX NA MWANDISHI WA HABARI WALISAIDIA NYERERE ASIPINDULIWE

SIRI ya mashujaa waliozima jaribio la kutaka kupindua Serikali ya Tanzania chini ya Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1982, imewekwa hadharani kwamba mashujaa hao walikuwa vijana wawili; mmoja dereva wa teksi na mwingine mwandishi wa habari wa gazeti la Serikali la Daily News.

Akitoboa siri hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Balozi Augustine Mahiga, alisema kama si vijana hao, huenda mapinduzi yangefanyika na yangefanikiwa, amani ya Tanzania leo isingekuwepo.

Akisimulia ilivyokuwa, Balozi Mahiga ambaye alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa akiwa kijana wa miaka 30, alisema kuna kijana wa miaka 23 aliyekuwa dereva wa teksi (bila kumtaja jina), ambaye alipata taarifa hizo ambazo Serikali haikuwa nazo.

Baada ya kupata taarifa hizo, Balozi Mahiga alisema kijana huyo alimweleza mwandishi wa
habari wa Daily News (bila kumtaja jina), ambaye naye alikuwa kijana mdogo wa miaka 27, ambaye alipeleka taarifa hizo kwake.

Kwa mujibu wa Balozi Mahiga, alipopata taarifa hizo, aliamua kufanya uchunguzi na kubaini kama kweli kulikuwa na mpango wa kutaka kupindua Serikali, ambao waliuzima kwa kukamata washukiwa ambao walipelekwa mahakamani na kufungwa.

Watu hao ambao alisema walisamehewa wakati wa uongozi wa Awamu ya Pili, sasa wapo huru lakini mpango wao kama ungefanikiwa, huenda amani iliyopo sasa isingekuwepo kwa kuwa kuipoteza ni rahisi kuliko kuirejesha.

“Rasilimali kubwa ya amani ni vijana kwa kuwa kama si wale vijana kutoa taarifa, mapinduzi yangetokea na amani iliyopo sasa isingetokea…amani ikipotea ni shida kuirejesha.

“Msiombe kutokee vita…mimi nimeona watu wanaoishi katika vita, hawana hata muda wa kula wala kulala, akifa mmoja mwingine anabeba silaha anaendelea,” alisema Balozi Mahiga.
Daily News ni moja ya magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya TSN, mengine yakiwa HABARILEO, HABARILEO Jumapili, Sunday News na SpotiLEO.

HabariLeo: Mwandishi TSN atajwa kuzima uasi


WANAFUNZI WALIO CHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU MBALIMBALI TANZANIA


Nakala hizi ni zimepatikana via JamiiForums


SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 25 SEPTEMBA HAPA




MAN CITY YAIRARUA SHEFF WEDNESDAY

Timu ya Man city usiku wa kuamkia leo imeishushia kipigo kikubwa cha mabao timu changa ya Sheff Wed kwa kuitandika 7 kwa 0, Mabao hayo yaliwekwa kimiani na Lampard dk ya 47 na 90, Dzeko 53 na 77, Jesus Navas dk ya 54, Yaya Toure dk ya 60 kwa penati.
Dzeko akiukwamisha wavuni mpira kama anavyoonekana hapo akiwa ameruka juu.
Frank Lampard akishangilia kwa kugongeana na Navas katika moja ya bao lake.
 Makocha wa timu zote mbili katika harakati zao uwanjani hapo.




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU