Facebook Comments Box

Monday, July 8, 2013

MWANAFUNZI WA VETA DODOMA AJICHOMA MOTO KISA WIVU WA MAPENZI


MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.

Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua.

“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.

“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).

Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.


LIVERPOOL REJECT £ 30 M ARSENAL BID FOR SUAREZ


Luis Suarez Liverpool have turned down a £30m bid from Arsenal for 26-year-old Uruguayan striker Luis Suarez. Suarez has been at the centre of transfer speculation since saying in May that it would be a "good moment for a change", and admitted it would be "difficult to say no" to Real Madrid. Liverpool refused to comment on reports of Arsenal's move and have previously insisted Suarez is not for sale. However, it is understood an approach was made and instantly rejected. Chelsea have also been linked with a move for Suarez and it remains to be seen if Arsenal take their interest further as manager Arsene Wenger continues to finalise a deal for Real Madrid's Gonzalo Higuain. Real are expected to emerge as the most serious test of Liverpool's resolve not to sell Suarez unless they receive an offer in the region of the £50m which saw Fernando Torres move to Chelsea in January 2011. Liverpool manager Brendan Rodgers remains relaxed about Suarez's situation and the striker has yet to indicate to the club that he wishes to leave. The Merseyside club's stance has always been that they have no desire to part with Suarez - and even if Liverpool's hand is forced by the player's own discontent they will not be pushed into a deal and will hold out for the maximum price.


MLIPUKO WA KIPINDUPINDU MBEYA: MIKUSANYIKO YAPIGWA MARUFUKU

UGONJWA wa kipindupindu, umeingia katika wilaya ya Kyela na kuua watu wawili na 39 wakiwa wamelazwa.

Taarifa zinasema ugonjwa huo umeibuka wilayani humo wiki iliyopita ukisadikika kuanzia katika Kijiji cha Ngonga na kisha kusambaa hadi Kilwa.

Kutokana na hofu ya kupata maambukizi kwa wananchi wengine, serikali imepiga marufuku mikusanyiko ikiwemo ya harusi, kipaimara, ngoma, michezo na sikukuu inayosherehekewa kila mwaka ya wakulima. 


--- taarifa via Kalulunga blog



SABABU ZA ZITTO KABWE KUTOSHIRIKI TAMASHA LA MATUMAINI

Kupitia account yake ya facebook Mh. Zitto Kabwe amepost hotuba hii akielezea kushindwa kwake kufika katika tamasha la siku ya matumaini.
POST YAKE AMEANZA KWA KUANDIKA HIVI.

Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji.

TAMASHA LA MATUMAINI

Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka. Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.

Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.

Nawaomba muiombee amani nchi yetu na msimamie haki kwa wananchi wote bila kubagua dini zao, rangi zao, hali yao kimaisha na ufuasi wa vyama vya siasa. Mwaka huu tumeshuhudia matukio ambayo yanatikisa msingi wa Taifa letu – Umoja. Hivi sasa msingi wetu una nyufa ambazo kwa kweli hatujajua bado nini kinacholeteleza mambo haya kama kulipua makanisa, kulipua mikutano ya vyama vya siasa na kuua viongozi wa dini.

Matukio haya yanatuelekeza kuwa makini sana na kauli zetu kwani baadala ya kuunganisha wananchi tunawezajikuta tunawagawa zaidi Watanzania na hivyo kuwa na mzunguko wa machafuko (vicious circle of violence). Ni wajibu wa viongozi wa kisiasa na wananchi kuepuka kabisa kuanza kurushiana maneno na lawama kuhusu matukio haya, kwani inawezekana lawama na maneno yetu yakawa yanampa nguvu adui wetu ambayo hatujamjua bado.

Napenda niwakumbushe kwamba ni rahisi sana kusambaza chuki na ni vigumu sana kuondoa chuki miongoni mwa wananchi. Viongozi hatari kama Hitler walitumia sana mbinu ya kueneza chuki dhidi ya jamii ya Jews na matokeo yake yalikuwa ni vita vikuu vya pili vya dunia na zaidi ya watu milioni 6 wasio na hatia kupoteza maisha. Sisi sote tuna jukumu moja la kuhakikisha tunajenga Taifa lenye kujali HAKI na lenye mshikamano mkubwa miongoni mwa raia. Kwa nia hii tu ndio tutaweza kuwa na Taifa imara lenye heshima mbele ya mataifa mengine duniani. Ni kwa njia hiyo tu ndio tutaweza kutokomeza umasikini uliokithiri mijini na vijijini hapa nchini kwa kuongeza uzalishaji na kupanua ajira. Ikumbukwe bila HAKI hakuna AMANI na bila UWAJIBIKAJI hakuna UTULIVU.

Tukiegemea siasa za CHUKI. Tukashindwa kuwa na mahusiano ya kawaida miongoni mwa viongozi kuhusu masuala ya msingi ya nchi. Tukashindwa kujadiliana kwa hoja kuhusu sera zetu. Tutapata viongozi aina ya Hitler nchini mwetu. Wote tukatae. Sisi ni Watanzania. Muwe na Tamasha jema la Matumaini.

Zitto Kabwe
7.7.2013, Aspen Colorado, USA.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU