Facebook Comments Box

Thursday, May 23, 2013

MAJAMBAZI WAMELIVAMIA HILI GARI NA KUPORA PESA LEO




Matundu matatu ya risasi katika kioo cha gari lililovamiwa na majambazi.

Wanausalama barabarani wakichukua taarifa eneo la tukio.

Majambazi yaliyokuwa na silaha aina ya SMG yakiwa na pikipiki aina ya Bajaj Boxer yamevamia gari ndogo aina ya VITZ N a kuwajeruhi watu wawili wenye asili ya asia na kupora kiasi cha fedha ambacho bado thamani yake haijafahamika mara moja.


KIBONZO: VURUGU ZA MTWARA

Picture


SHEHA AMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR

\
Sheha Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.

Sheha Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo.


BUNGE LA AHIRISHWA TENA LEO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati ya uongozi ya Bunge iendelee kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.
BUNGE LAAHIRISHWA TENA LEO:Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati ya uongozi ya Bunge iendelee  kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU