Facebook Comments Box

Wednesday, October 3, 2012

MASAA MAWILI KABLA YA MECHI YA YANGA NA SIMBA HALI NDIO HII

Basi la Simba likiwa limepaki makao makuu ya Trafiki, kusubiri ulinzi kwa ajili ya kwenda kuipokea timu Bandarini, ikitokea Zanzibar


Basi la Simba likiwa limepaki makao makuu ya Trafiki, kusubiri ulinzi kwa ajili ya kwenda kuipokea timu Bandarini, ikitokea Zanzibar

Eeneo la Gerezani, karibu na BP kama unaenda Kurasini

Eneo la Gerezani, karibu na BP kama unaenda Kurasini

Jamaa amenunua na kuvaa hapo hapo jezi ya Yanga

Biashara ye jezi

Add caption

Mashabiki wa Simba wanaelekea uwanjani

Daudi Chalamila na Simba mwenzie


Barua ya Wazi kwa Waziri husika - Yah: Kudorora kwa huduma za TTCL 03/10/2012 0 Comments BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI KUHUSU KUDORORA KWA TTCL Kwa mara nyingine tena najitokeza kuweza kutoa kero ambazo zina tupata Sisi Wananchi tunao tumia huduma za TTCL Katika Mabadiliko ambayo Serikali ina himiza Wananchi katika kuingia katika Soko la Afrika Mashariki na ya Kati ni kujiendeleza kielimu lakini kuhizwa huko hakuko kwa TTCL wao bado na mfumo wa kizamani, Kwenye Umeme angalao serekari ime gundua kitu fulani kwa nini shirika hili naslo lisi chunguzwe kujua kama kuna masilahi ya watu au kukwama kwao kuna tokana na Elimu au ni watu wana kwamisha :?. Watanzania tulio kuwepo katika Utawala wa Mwalimu Nyerere tuna usemi wa kusema usiache Mbachao kwa Msala upitao. Methali hii inatubana kuitelekeza TTCL. katika Mitandao ambayo inaweza kumsaidia Mwananchi asiye na kipato ni TTCL lakini Shirika limekuwa na kiburi hata kama wateja wakilalamika Shirika la TTCL halisikii malalamiko ya wananchi. Katika kutumia huduma za Internet .wateja wanalazimika kulipa kwenye mtandao wa TTCL Shilingi 30,000 kwa Mwezi au 7000 kwa Bando na hata Shilingi 500 ili waweze kupata huduma. Cha kushangaza baada ya kulipa kwenye mtandao wa TTCL ili upate huduma unakuwa kama vile umepoteza fedha zako unaweza kuwa na kazi yhati inawezekana ika shindika kutuma yenye MB25 ukianza asubuhi ukiwa na bahati ita enda saa kumi jioni kama huna bahati ndiyo basi Kama Una Attach file MB 25 unaweza kujanza Attachment Saa 2 Asubuhi ukafanikisha saa 9:00 Alasiri au ikakata. Ukiingia kwenye Mtandao mwingine Attachment hiyohiyo unachukua dakika 2 – mpaka dakika 5. Je! TTCL ina Wataalamu waliobobea ni vipi ishindwe kuweka Mazingira mazuri kwa wateja wao. Wafanya kazi wa TTCL ambao hawakutaka Majina yao yatajwe wamedai wameweza kutoa Taarifa ya Malalamiko ya Wananchi hakuna kiongozi wa juu anaye tilia maanani malalamiko hayo. Cha msingi kinachoonekana kwa TTCL badala ya kuboresha huduma wao wanawaza kuuza mali za TTCL kama walivyo fanya wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma , Mimi ni Mteja wa TTCL toka ilipoanza . Namba yangu ya Simu 0252602425. Naishi Songea. Ningeomba Watanzania, Wananchi wanaotegemea sana Mtandao wa TTCL, endapo hali ikiendelea namna hii basi Wale wote wanao ihujumu TTCL Serikari ingeweza kuwawajibisha. Haiwezekani Mitandao mingine ifanye kazi lakini mtandao wa Serikari uhindwe kufanya kazi. By Adam Mzuza Nindi, Songea. web: Songea Habari Add Comment Mhe. Mwanjelwa na Dereva wake wapelekwa Dar es Salaam kwa tiba zaidi 03/10/2012 0 Comments Imeelezwa kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Viti Maalum CCM, Dkt. Mary Mwanjelwa anasafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya huduma zaidi za kiafya baada ya kunurusika ajalini jana. Dkt. Mwanjelwa alikuwa amelazwa katika hospitali teule ya Ifisi tangu jana. Ameweza kuzungumza kwa ufasaha na kuwatambua watu aliokuwa wanaingia na kutoka kumjulia hali. Alisema, "Hali yangu ni nzuri, najisikia maumivu sehemu za kiunoni na kwenye mbavu, lakini najisikia vizuri". Nje ya wodi alimokuwa amelazwa walikuwepo baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na wananchi waliokwenda kumjulia hali. --- picha na maelezo via Mkwinda blog na MbeyaYetu blog Dkt. Mwanjelwa akiwa hospitalini Ifisi asubuhi ya leo. (picha: Mkwinda) Mwenyekiti wa UWT Mbeya bi. Blorence Kyendesya akitoka hospitalini kumjulia hali Dkt. Mwanyelwa (picha: Mkwinda) Bi. Hilda Ngoye (CCM Viti Maalum, mkoa wa Mbeya), akiwafariji ndugu na jamaa wa Dkt. Mwanjelwa baada ya kumwona wodini (picha: Mkwinda) Dereva wa Mhe. Mwanjelwa akisubiri kusafirishwa Add Comment Posta ya Tanzania, Dar es Salaam: Mara tatu ilitosha, si hii ya nne. Hapana! 03/10/2012 2 Comments UPDATE: Ninashukuru sana kwa ushirikiano na msaada mkubwa wa kushughulikia suala hili ambao nimeupata hadi sasa kutoka kwa Niliyemtumia parcel. Anafuata kila 'step' inayotakikana. Baba, Sabato Tarimo kwa kuwasiliana na mhusika wa Bodi ambaye alifanikisha kupatikana mzigo nilioutuma ukapotea mara ya tatu. Dad, you have always been there for me in good and bad times. I will never be able to say enough THANK YOUs. Zitto Kabwe (Mb) kwa kunisikiliza niki-vent off kuhusu mkasa huu na kunipa ushauri pamoja na kuahidi kufuatilia atakavyoweza. January Makamba (Mb, Naibu Waziri) kwa kuzungumza nami na kunipa maelekezo ya nini cha kufanya na ahadi ya kufuatilia kwa kuwa tayari ilikuwa katika mipango, kwa bahati nzuri kuna na mwananchi mwingine aliwasilisha tatizo linalofahanana na la kwangu, kwa hivyo ni kama nimeongeza uzito wa kuonesha umuhimu wa kushughulikia kadhia hii. Marafiki wote wa facebook na twitter mnaonipa moyo na kuniunga mkono katika kupiga vita udokozi na huduma mbovu katika Shirika letu la Posta Tanzania, hasa mkoa wa Dar es Salaam. Ifike mahali upuuzi huu ufe! Posta ya Tanzania, here I come! Kero ya Posta Tanzania. Nimetuma parcel Tanzania (na hii si mara ya kwanza), kwa njia ya USPS Express Mail, 3-5 days delivery na mara zote ninaowatumia wanapokea kati ya siku ya 5 - 7. Hii niliyotuma tarehe 17 Septemba, 2012 aliyetumiwa hakupigiwa simu wala kutaarifiwa kwa namna yoyote kuwa parcel imefika. Baada ya zaidi ya siku 7 kupita, akaanza kufuatilia. Akipiga simu anaambiwa hatuuoni, bado haujafika. Akaamua kwenda kuwaona ana kwa ana jana, akapewa majibu yale yale. Nikamfahamisha kuwa waliwahi kunipotezea mizigo hawa kwa kauli hizo hizo, na baadaye walipopigiwa simu na "Mkubwa" wao, mzigo ulijulikana uliko ndani ya saa chache siku ile ile. Nikamfahamisha aombe kuonana na Meneja, akafanikiwa. Wakatizama parcel, computer zao (huko kwa Mameneja) zikaonesha parcel ilifika tangu tarehe 23. Meneja akaagiza watizame vifurushi ili wampatie. Kwa kuwa ilikuwa imekaribia muda wa kufunga ofisi, wakamwambia arudi kesho (yaani leo) kuuchukua, lakini kwanza apige simu asubuhi au wao watampigia utakapokuwa tayari. Akawapigia simu asubuhi, wakamwambia bado, apige saa nne. Akapiga simu saa nne, anapewa maelezo tofauti na ya jana, Meneja anamwambia kifurushi hakijapokelewa na maelezo mengine ya kuwa maelezo ya jana haikumaanisha hivyo bali vingine. Amepiga simu kutaka kutoa maelezo mwa Mkubwa wa Posta, anajibiwa kuwa hawezi kuzungumza naye suala hilo, amwambie tu aliyetuma ajaze hayo makaratasi ya USPS ya refund alipwe fidia. Nilipoandika juzi pale wavuti.com kuwa baadhi ya Wafanyakazi wa Posta ni wadokozi na waache udokozi, ni kwa sababu nimeshapata usumbufu mara tatu na sasa ni mara ya nne katika Shirika la Posta la Tanzania, EMS, mkoa wa Dar es Salaam. Mara mbili kati ya hizo parcel nilizotuma kwa njia ya kawaida hazikufika. Mara moja nilipotuma kwa njia ya USPS Express Mail waliupoteza lakini walipigiwa simu na Mr. Mndeme na ndani ya saa chache maelezo yote na ulipo mzigo vilipatikana. Hii mara ya nne, inakuwa ni mara ya pili kutuma kwa USPS Express Mail parcel inapotea na maelezo ya kufuatilia kujua ulipo ninayopewa ni hayo niliyoeleza hapo juu. Nimetaka ku-vent off kwa sasa, ila kazi ndiyo (isiyo ya lazima) ndiyo imeanza tena. Kwa bahati mbaya (au nzuri) kazi ndiyo imeanza rasmi. Posta, nina nyie, mpaka kieleweke kwangu kwa lugha yangu! YOU WILL COUGH UP TO THE LAST DIME!!! This I promise you! Here I come... 2 Comments How to disable/turn off Gmail automatic image display from senders 03/10/2012 0 Comments When you receive an email that contains externally linked images, Gmail usually doesn’t display the images automatically. This behavior is designed to help protect your privacy; if Gmail displayed the images automatically, it could potentially allow the sender of the email to track and see that the images are being fetched, and therefore know when you’ve read their message. But, if someone you've sent email at least twice sends you a message with images in it, you’ll see the image by default (because the people in this group are likely people you know and trust). Gmail will only show images in messages that are authenticated, so you won't have to worry about seeing images in messages where the sender's name or address is spoofed. If you’d like, though, you can change your settings so that images from these senders won’t be shown by default either. Here’s how: ALTERNATIVE I While signed on in your Gmail account, Click the gear icon (see the circle in the scree-shot below) in the upper right, then from the drop down menu, select Settings. In the External content section, select Ask before displaying external content. Click Save Changes. Picture ALTERNATIVE II While signed on in your Gmail account, Click on the down facing arrow on the left, just after the the senders' name (see the red circle in the screen-shot below). A small window opens, look at the bottom to see highlighted words reading, “Don’t display image from now on.” and click on them (see the words in ellipsis illustrated in the screen-shot below). Picture You are done. There is nothing more into it, really. You can reverse and display the images in the future by following above steps, this time clicking to re-enable image display. Add Comment WaHasira: Infakti, hawa si wanangu, lakini... 03/10/2012 0 Comments Picture sidymic.blogspot.com Add Comment “Sisubiri ruhusa ya mtu yeyote, nani asiyejua kuwa Chenge ni mtuhumiwa?” 03/10/2012 1 Comment Uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeelezwa kuwa utabiri mwema kwa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kutokana na kuingiza sura mpya huku vigogo wakibwagwa. Aidha, baadhi ya waliong’ara katika uchaguzi huo wametabiriwa neema kushika nafasi za juu katika Serikali ukiwamo urais mwaka 2015 ikiwa watakuwa tayari kusafisha madoa waliyonayo. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Dk Benson Bana aliliambia gazeti hili jana kuwa CCM imedhihirisha ni chama dume, chenye demokrasia na ukomavu kisiasa. Akifafanua, alisema: "Uchaguzi unadhihirisha wazi kuwa CCM bado inadunda na dhana ya kujivua gamba inatekelezwa, watu zaidi ya 5,000 walipitishwa Dodoma huku sura mpya zikijitokeza, miongoni mwao ni vijana, wazee hata wakulima". Dk Bana alisema hatua hiyo imedhihirisha mianya ya rushwa kudhibitiwa ndani ya chama hicho, baada ya kuona magwiji wa siasa akiwamo Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, wakiangushwa, jambo linaloashiria hakubaliki kuwania urais. "Hakuna asiyejua mbio za Sumaye kutaka urais, sasa kama jimbo la Hanang watu wachache wamekukataa, si rahisi Watanzania wakupe urais, namshauri sasa arejee kutumika katika nafasi yake ya siasa kama Waziri Mkuu mstaafu, maana Watanzania wameamua kufanya mabadiliko," alisisitiza Dk Bana. Kuhusu madai hayo, alipoulizwa Sumaye jana, alisema, "najua unataka habari ya uchaguzi, sasa hivi sisemi lolote ila nitakuja Dar es Salaam kati ya siku mbili au tatu hivi, utaniuliza na hilo swali lako nitakapozungumza nanyi waandishi wa habari." Akizungumzia harakati za urais mwaka 2015 kutokana na uchaguzi huo wa CCM, Dk Bana alisema CCM itang’ara katika uchaguzi ujao ikisimamia mweleko wa sasa, lakini hatima yake imesimama katika mambo mawili; Katiba mpya na uteuzi wa atakayepeperusha bendera kuwania urais. "Uchaguzi 2015 tutarajie mambo makuu mawili; Katiba mpya ndio pekee itatoa mwelekeo wa kitakachotokea, lakini pia CCM inateua nani kuwania urais wakati huo, hii itabadili mtizamo wa siasa, wakiteua vizuri, watawafunika wapinzani," alisisitiza Dk Bana. Dk Bana alivunja ukimya na kueleza wazi kuwa, hivi sasa ndani ya CCM kuna mtu anayenukia urais, ila bado ana madoa anayopaswa kuyasafisha ili akubalike. Alimtaja mtu huyo kuwa ni Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa. Hata hivyo, Dk Bana aliitaka CCM iwaadabishe baadhi ya wanachama, baadhi ni viongozi wa nchi akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta na Peter Kisumo (Mdhamini wa CCM) kwa alichodai, wanazungumza bila kufuata utaratibu. "Hawa wana kambi zao ndani ya chama, wanataka kumvuruga Katibu Mkuu Mukama (Wilson) kwa kauli zao, wasipewe nafasi waadabishwe kurejesha nidhamu," alihimiza Dk Bana aliyekuwa akitoa maoni yake kuhusu uchaguzi unaoendelea CCM. Akijibu tuhuma hizo jana, Sitta alisema: "Nimezoea, kauli zangu hazijawahi kuwafurahisha hata siku moja mafisadi, nataka wajue hivi; nitazungumza mpaka tone la mwisho la pumzi yangu, nimefundishwa kukemea maovu na Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere)". Sitta alijigamba kuwa, alijiunga na TANU Oktoba 3, 1960 akiwa kidato cha tatu na sasa ni miaka 52 ndani ya chama, hajavunja utaratibu wowote katika kukemea maovu na wanaotaka anyamaze, anawakera kwa kuwa amewagusa. "Sitachoka kusema mafisadi, maana wanaharibu nchi yetu, hata Ilani ya chama inanilinda nikemee maovu, sisubiri ruhusa ya mtu yeyote, nani asiyejua kuwa Chenge (Andrew-Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM) ni mtuhumiwa, haiingii akilini eti amepita bila kupingwa Bariadi, watu 11 waliochukua fomu wamefutikia wapi?" Alihoji Sitta. Sitta, Spika mstaafu alipotakiwa kufafanua hoja hiyo, alisisitiza kuwa inajulikana wazi ndani ya chama na wachache wenye ujasiri kama yeye, ndio wana uwezo wa kusema na kusisitiza kwamba hatanyamaza mpaka pumzi yake ya mwisho. Hata hivyo, alikiri kuwa uchaguzi wa CCM umekwenda vizuri ila hivi sasa yapo baadhi ya maeneo bado rushwa inatumika kupindisha matokeo na kusisitiza kwamba ikiwa rushwa itakemewa ndani ya chama na viongozi halali wakapatikana, hata dawa hospitalini zitapatikana na ndilo tamanio la wapenda maendeleo. Dk Bana aliendela kumshauri Rais Jakaya Kikwete kutumia muda mwingi kuzungumza na wanachama katika ngazi za wilaya, kwa kuwa anakubalika kwa zaidi ya asilimia 60 hadi 70 na nguvu ya chama ni mwenyekiti. "Hakuna chama bila mwenyekiti, kitayumba, Kikwete anakubalika, binafsi afanye ziara kuzungumza na wanachama, asisubiri kuonekana wakati wa uchaguzi bali afanye ziara kuimarisha chama," alishauri Dk Bana. Alisema mpaka sasa zaidi ya asilimia 51 ya wagombea wa uchaguzi unaoendelea ni wasomi kuanzia Stashahada na Shahada mbalimbali, kinachogomba upinzani ni watu wachache wanaopiga kelele na kusahau kujenga vyama vyao. "Tatizo la Upinzani ni kwamba, wamegeuka kuwa wanaharakati wa kuitisha maandamano ya mpaka kieleweke, nini kieleweke? Tena wachache ndio wanapiga kelele, wanapaswa kurudi kuwa wanasiasa na si wanaharakati, wawaache Tamwa (Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake) na wengine," alikazia Dk Bana. Alisema ni kwa misingi hiyo, anarejea kauli yake kuwa bado ni ndoto kwa upinzani kushika Dola kwa kuwa wamekuwa na kazi ya kuishambulia Serikali kwa kutumia watu wachache machachari na kusahau kuimarisha ndani na kufanya uchaguzi wao usiwe na mvuto wala vuguvugu kutokana na ufinyu wa demokrasia. "Watu hawataacha kusema kuhusu uchaguzi katika upinzani kuwa watu wanapeana vyeo, kwa sababu ya ushemeji, hili litafutika ikiwa demokrasia ya kweli itaachwa ifanye kazi ndani, wasipige kelele nje wakati ndani hakujakaa sawa," alishauri Dk Bana. Alishauri wapinzani kuiga demokrasia iliyotumika ndani ya CCM na kuhakikisha kuwa mikakati yao kupitia M4C (Chadema) na V4C (CUF), zinazaa matunda ya kuimarisha vyama vyao. Katika hatua nyingine, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Method Kilaini ametoa maoni yake kuhusu uchaguzi huo wa CCM na kukipongeza chama hicho akidai kimeonesha ukomavu wa kisiasa. "Wale walioshindwa hawapaswi kupiga kelele na kama wakipiga sana, watu watahoji walikuwa si washindani bali kuna kitu walikuwa wanatafuta. Mshindani siku zote anakubali kushindwa," alishauri Kilaini. Wilayani Bariadi Juliana Mahongo alitetea nafasi yake ya Mwenyekiti huku Andrew Chenge akipita bila kupingwa katika nafasi ya ujumbe wa NEC na Masunga Yabuyeze akitetea nafasi yake ya Katibu Mwenezi. Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima aishinda ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na wajumbe wengine Tina Chenge, Gasper Mjuna, Rachael Subanda na Masanja Kidogosa. Pia wilaya ya Itilima ilipata Mwenyekiti wa CCM ambapo Mabula Mohamed alichaguliwa huku ujumbe wa NEC ukienda kwa Daud Njalu ’Nsagali’, na John Nkululu alichaguliwa kuwa Katibu wa Uchumi na ukatibu mwenezi ukienda kwa Mang’ombe Gwalugwa. Katika wilaya ya Busega aliyechaguliwa kushika nafasi ya Mwenyekiti ni Mshoni George, huku uNEC ukienda kwa Raphael Chegeni na Katibu Mwenezi akichaguliwa Raphael Babasha. Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, alichaguliwa ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na wajumbe wengine wakiwa ni Hamis Haule, Josia Mgemu, John Mkale na Mikinesi Mahela. Wilayani Maswa Mwenyekiti wa Wilaya Peter Bunyongoli alichaguliwa tena kuendelea na wadhifa wake na Aron Mboje akachaguliwa kuwa mjumbe wa NEC. Wajumbe watano wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ni Masanja Mpiga, Pili Kidosela, Amina Almasi, Thobias Kadome na Mercia Emmanuel. --- Habari via Ziro&Tina blog 1 Comment America's Delta Airlines opens office in Dar es Salaam to start direct flights 03/10/2012 0 Comments Picture Picture (photo: blog.delta.com) US-based Delta Airlines has opened office in Dar es Salaam a move the company says is geared towards strengthening the business and economic links that already exist between Tanzania and the US particularly in the tourism sector. Robert Bryan, Delta’s Director Commercial Manager for East Africa and West Africa made the announcement last week during the launching of the new Office. “As US Investors, we are excited to invest in the East African market and we are here because we realize the potential in this country and surrounding the EAC region…” explained the director. With an extensive domestic an international route network Delta in partnership with Kenya Airways and KLM has now opened a direct airline from US to Tanzania and given the market then start the reverse route, from the US to Tanzania Delta Airlines has already opened other sales office in Nairobi and Kampala and the commercial director says they are confident that these new services will attract more US travelers to visit Tanzania. According to Bryan, although Delta does not currently operate direct services to Tanzania, customers traveling to the United States on Delta can book flights via Europe operated by Delta’s joint venture partner KLM or Sky Team partner and Kenya Airways. Additionally, customers can opt to fly via Johannesburg, Lagos or Dubai to Delta’s hub in Atlanta which offers onward connections to more than 150 destinations throughout the U.S and beyond. Delta is investing more than USD 3bn through 2013 in airport facilities and global products, services and technology to enhance the customer experience in air and on the ground. Delta launched its first services between Africa and the United States in December 2006, and right now the airline operates services to the US from five cities in Africa including Accra-Ghana, Lagos- Nigeria, Dakar- Senegal, Johannesburg-South Africa, and Monrovia-Liberia. Delta serves more than 160million customers each year and just in the past year, Delta was named America’s domestic Airline of the Year by Travel Weekly Magazine and it was also named the top Tech-friendly US Airline by PCworld magazine for its innovation in technology and on top of that the company won the Business leading edge awards for US Airlines. Delta headquartered in Atlanta and so far it employs 80,000, employees worldwide and operates a mainline fleet of more than 700 aircraft. With an industry leading global network, Delta and Delta connection carriers offer service to nearly 320 destinations in 60 countries on six continents. --- via The Guardian Add Comment Nyerere Day Oktoba 14, 2012: Unakaribishwa! 03/10/2012 0 Comments Picture Add Comment Ripoti ya MCT ya mauaji ya Daudi Mwangosi kuwekwa hadharani Oktoba 9, 2012 03/10/2012 0 Comments Ripoti ya uchunguzi wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari mwakilishi wa kituo cha televisheni ya Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi, uliofanywa na timu ya waandishi wa habari watatu kutoka Baraza la Habari (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), itawekwa hadharani Oktoba 9, mwaka huu. Azma hiyo ilitangazwa jana Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, baada ya timu hiyo kukamilisha uchunguzi wake hivi karibuni. Mukajanga alitangaza azma hiyo alipotakiwa na gazeti la NIPASHE kueleza lini ripoti hiyo itatangazwa. Akijibu swali hilo kwa njia ya maandishi, Mukajanga alisema kwa kifupi: “Jumanne Oktoba 9, 2012 Inshallah.” Awali, NIPASHE ilizungumza na Katibu Mtendaji wa TEF, Neville Meena, ambaye alisema uchunguzi wa timu hiyo umeshakamilika na kwamba, ripoti yake imekabidhiwa kwa Bodi ya MCT. Timu ya waandishi hao iliyoundwa Septemba 4, mwaka huu, iliongozwa na Meneja wa Utafiti na Machapisho wa MCT, John Mirenyi, wajumbe wakiwa ni Mhariri wa masuala ya siasa wa gazeti la Mwananchi, Hawra Shamte na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Simon Berege. Timu hiyo ilipewa siku nane na ilianza kazi yake Septemba 6, mwaka huu, kubaini ukweli wa tukio hilo na kuweka kumbukumbu sahihi ya tukio hilo. Wakati huo huo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, alikataa kuzungumzia timu ya jeshi hilo iliyoongozwa na Mkuu wake, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, umekwisha au nini kinaendelea, akisema hawaruhusiwi kufanya hivyo kwa kuwa liko mahakamani kisheria. “…Waziri wa Mambo ya Ndani alishalisemea,” alisema Senso. Mwangosi, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (IPC), aliuawa kwa kupigwa na bomu lililosambaratisha mwili wake wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuwazuia kufungua tawi la chama hicho, katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani humo, Septemba 3, mwaka huu. Tayari askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), mwenye namba G2573, Pasificus Cleophace Simon (23), amefikishwa mahakamani akituhumiwa kwa mauaji ya Mwangosi. -- via Nipashe Add Comment New York’s Mayor Bloomberg aims to save mothers, children in Tanzania


 
Picture
A short video on the work of Bloomberg Philanthropies in Tanzania is playing in the background. (photo by Tagie Daisy Mwakawago)
Picture
President Kikwete answering few questions from the reporters (not in the photo). (photo: Tagie Daisy Mwakawago)
Picture
Tanzania Delegation which consisted of Chief Secretary H.E. Ambassador Ombeni Y. Sefue (5th left), Ambassador Liberata Mulamula, Senior Advisor to President Kikwete, Ambassador Mwanaidi Sinare Maajar (3rd left), Ambassador of the United Republic of Tanzania to the United States of America, H.E. Ambassador Tuvako Manongi (left), Permanent Representative of Tanzaia to the United Nations. Others are Deputy Ambassador Ramadhan Muombwa Mwinyi (4th left), Deputy Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations, Mr. Prosper Mbena (6th left), Assistant to President Kikwete and Mr. Salva Rweyemamu, Director of Communications to the Tanzania State House. (photo: Tagie Daisy Mwakawago)
Picture
H.E. Jakaya Mrisho Kikwete (3rd right), President of the United Republic of Tanzania in a press conference held today in New York to unveil results of Innovative Maternal Health Program in Tanzaina. Others are the United Nations Secretary General Ban Ki-moon (2nd left), New York City Mayor Bloomberg (left) and Ms. Helen Agerup 2nd right) of the H&B Agerup Foundation in the Dag Hammarskjöld Library at the United Nations Headquarter in New York, USA. (photo by Tagie Daisy Mwakawago)
UNITED NATIONS (Reuters) - New York City Mayor Michael Bloomberg said on Tuesday he is funding the expansion of a pilot maternal health program in Tanzania that is predicted to help 50,000 mothers and their children during the next three years.

A woman dies every two minutes of pregnancy-related problems with 99 percent of such deaths in poor countries, according to the U.N. Population Fund. Common causes are bleeding after childbirth, high blood pressure, infections and unsafe abortions.

"No one should have to die giving birth," Bloomberg told a news conference at the United Nations with Tanzanian President Jakaya Kikwete. "Too many women die due to complications in childbirth because of inaccessible and inadequate care."

The Bloomberg Philanthropies initiative trains assistant medical officers and midwives in remote areas to perform life-saving procedures including caesarean sections and upgrades isolated health centers.

"If you can build a model that you can show works in remote areas where the doctor to patient ratio is 1 to 50,000 then you can start attracting capital from an awful lot of other foundations and perhaps governments," said Bloomberg, founder of Bloomberg LP who has so far donated more than $2.4 billion to charity.

While U.N. data shows maternal deaths globally halved between 1990 and 2010 to 287,000 annually, many states in sub-Saharan Africa are forecast to fail to reach a U.N. target of reducing maternal deaths between 1990 and 2015 by 75 percent.

Tanzania is not on track to meet the U.N. target and has the eighth highest number of maternal deaths in the world - a woman dies almost every hour. Kikwete said that more money was needed to tackle the problem.

"We need to scale up efforts because still too many mothers and children continue to die," Kikwete told reporters.

The Bloomberg Philanthropies maternal health program began in Tanzania in 2006. Bloomberg has now joined forces with Geneva-based H&B Agerup Foundation to spend $8 million to expand the program over the next three years, taking the total spent since the initiative started to $15.5 million.

Bloomberg's third term as New York City mayor finishes at the end of next year and he has said he will then dedicate himself to philanthropy. He hit No. 10 on Forbes latest ranking of the richest people in the United States with an estimated fortune of $25 billion.

In 2011 Bloomberg Philanthropies spent $330 million and Bloomberg has signed up to the Giving Pledge, a philanthropic campaign by two of the world's richest men - Warren Buffett and Bill Gates - that required him to announce he would give away at least half his wealth during his lifetime or after his death.

(Reporting by Michelle Nichols; editing by Andrew Hay)

---
Yahaoo! News
Picture
H.E. Jakaya Mrisho Kikwete (left), President of the United Republic of Tanzania listens Mr. Ban Ki-Moon, Secretary General of the United Nations prior to the press conference of the Maternal Health Program in Tanzania funded by Bloomberg Philanthropies. Second right is Mr. Michael Bloomberg, Mayor of the New York City and Ms. Helen Agerup (2nd left), President of H&B Agerup Foundation. (Photo by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation)
Picture
President Kikwete explains the much needed training for non-physician clincians in health facilities throughout the regions in Tanzania. (Photo by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation)
Picture
Ban Ki-moon listens to Mayor Bloomberg prior to press conference of Maternal Health Program in Tanzania funded by Bloomberg Philanthropies held today in Dag Hammarskjöld Library at Nations Headquarters in New York, USA. (Photo by Tagie Daisy Mwakawago)
Picture
H.E. Jakaya Mrisho Kikwete (left), President of the United Republic of Tanzania discusses briefly with New York City Mayor Michael Bloomberg (right) about his country's gratitude towards the Bloomberg Philanthropies initiative which resulted in an increase of over 1,000 delivery health facilities in Kigoma, Morogoro and Pwani Regions in Tanzania. Others in the photo are Ambassador Tuvako Manongi (2nd left), Permanent Representative of the United REpublic of Tanzania to the United Nations and Ms. Helen Agerup (2nd right), President of H&B Agerup Foundation. (Photo by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation) 


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU