Facebook Comments Box

Sunday, April 14, 2013

HISTORIA YAANDIKWA LEO: MASHABIKI WA YANGA WAKIISHANGILIA SIMBA UWANJA WA TAIFA

Katika hali isiyo ya kawaida katika upinzani wa Soka hapa Dar es Salaam kati ya timu hizi kongwe za Ligi kuu ya soka Tanzania Bara Simba na Yanga. Simba yenye maskani yake katika mtaa wa Msimbazi na Yanga yenye maskani yake kati ya mitaa ya Twiga na Jangwani hazijawahi kushangiliana hata siku moja pindi kila timu inapocheza na timu nyingine.

Leo Historia hiyo imeandikwa Baada ya Simba kutangulia kuifunga Timu ya Azam mabao 2 kwa bila mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, ambapo bao la kwanza lilifungwa na Ramadhan Abdallah Singano 'Mesi' kama ambavyo mashabiki wao hupenda kumwita baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kushoto. Na bao la pili lilifungwa na Mesi tena baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ngasa tena.

Kipindi cha pili Azam walipata Penati baada ya Beki wa Simba kumzuia Khamis Mcha 'Viali' ndani ya Box na Refa kuamuru Penati ambayo ilifungwa na Kipre Cheche, Bao la pili lilifungwa na Hamfrey Mieno baada ya kutokea Faul katika lango la Simba na mpira kupigwa na Khamis Mcha ukamkuta mfungaji alieukwamisha wavuni na kuwa bao la pili kwa Azam.
Mpaka mwisho wa Mchezo Simba 2 na Azam 2, hivyo Yanga wanaendela kukamata usukani kwa kuwa na point 52 wakifuatiwa na Azam yenye point 46 wakifuatiwa na Kagera Sugar yenye point 37 na Simba wanaendelea kubaki katika nafasi ya nne wwakiwa na point 36.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU