Tukio la Arusha limesibitisha pamoja mambo mengine kuna vipaji vilivyojificha kwa watu wengi hasa kwenye mchezo riadha!
— peter serukamba (@serukamba) June 19, 2013
Thursday, June 20, 2013
HAYA NDIO MAONI YA MBUNGE WA KIGOMA KUHUSU TUKIO LA MABOMU ARUSHA
MBOWE NA LEMA WAJISALIMISHA POLISI LEO ASUBUHI
WABUNGE WA CHADEMA WATHIBITISHA MKONG`OTO WALIOPEWA NA POLISI ULIKUWA WA NGUVU
Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu akiwaonyesha waandishi wa habari miwani yake aliyodai kuvunjiwa na polisi. Lissu alipata dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati, jijini Arusha jana baada ya kukamatwa juzi. Picha na Moses Mashalla |
Arusha/Dar es Salaam. Wabunge wanne wa Chadema, ambao waliachiwa
na polisi kwa dhamana wamesimulia mateso waliyoyapata wakiwa rumande
baada ya kukamatwa juzi.
Vigogo hao; Mbunge wa Mpanda Mjini Said Amour
Arfi, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce
Mukya (Viti maalumu), walikamatwa juzi baada ya wao na wafuasi wa chama
hicho kutawanywa kwa mabomu ya machozi na polisi kwenye Viwanja vya
Soweto, Arusha.
Wabunge hao waliachiwa baada ya kujidhamini
wenyewe huku watu wengine 65 waliokamatwa pamoja nao wakiachiwa baada ya
kudhaminiwa.
Wote wanatakiwa kuripoti kwenye kituo hicho Julai 22, mwaka huu na wataelezwa hatma ya suala hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa
Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jeshi lake
linaendelea kuwasaka Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na
Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na kuwaonya kuwa wanatakiwa
kujisalimisha mara moja.
Chagonja alisema Mbowe na Lema wanatafutwa kwa
kosa la kufanya kusanyiko lisilo halali katika viwanja hivyo vya Soweto
walipokuwa wakitaka kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi,
Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki dunia baada ya kuumizwa kutokana
na mlipuko wa bomu, Jumamosi iliyopita.
Pia aliwaamuru Mbowe na Lema kuwasilisha mara moja
ushahidi wa kuwahusisha polisi na shambulio la bomu na kama hawana
imani na Polisi, basi wawasilishe ushahidi wao kwa Rais Jakaya Kikwete.
Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni, alilalamikia kitendo cha polisi kumwagia maji ya
kuwasha baada ya kumkamata.
“Walinimwagia maji ya kuwasha kwa mfululizo
nikalazimika kulala chini kifudifudi huku nikiwa nimefunika macho
kukwepa yasiingie maji. “Kuna askari walitaka kunipiga lakini
niliokolewa na mwenzao mmoja aliyenikinga nisishambuliwe. Kwa kweli
ilikuwa hali ya hatari,” alisema.
Alisema polisi hao waliomkamata walivunja miwani yake kwa makusudi akisema aliikabidhi kaunta ikiwa haijavunjika.
“Wakati naingia mahabusu nilikabidhi miwani yangu
lakini ajabu wakati tukiachiwa ilikuwa imevunjika.” Alilalamikia hatua
ya polisi kuwashambulia kwa mabomu, kuwamwagia maji ya kuwasha
walipokuwa wakiwatawanya watu waliokusanyika Soweto akisema awali,
waliwaruhusu.
TUME YA UCHAGUZI YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA KAMPENI ARUSHA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, imevikataza vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Madiwani kwenye Kata nne za Arusha Mjini, kufanya kampeni katika kipindi hiki ambacho uchaguzi huo umehairishwa hadi Juni 30 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, JULIUS MALLABA amesema kwamba sheria za uchaguzi haziruhusu kwa sasa vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuwa uchaguzi katika Kata hizo umeahirishwa baada ya muda wa kampeni ulikwisha.
Vyama ambavyo vitaonekana kukiuka taratibu hizo vitachukuliwa hatua na kamati za maadili ambazo zinajumuisha wajumbe kutoka vyama vyote vya siasa nchini.
MALLABA pia ametoa wito kwa wananchi wa Kata hizo nne -- Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai -- kuwa ifikapo siku ya kupiga kura, washiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu.
Subscribe to:
Posts (Atom)