Facebook Comments Box

Tuesday, September 23, 2014

MECHI ZA CAPITAL CUP ZINAZOCHEZWA LEO NA MUDA WAKE




PICHA YA KIUMBE KILICHO ONEKANA PEMBA LEO

Kengeja Likoni kisiwani Pemba watu  wameshuhudia kiumbe kikubwa sana cha baharini kilicho pwewa katika mwamba wabahari kuu Kengeja
Kuna watu wengine wanasema ni  nyangumi wapo wanao sema chongowe na wengi wanasema hawamjui ni aina gani ya kiumbe hicho.

Hadi sasa wapo hapa Vijana Wa tawi la likoni zaidi ya Vijana 200 kujionea kiumbe cha ajabu urefu wake karibu mita 40 upana na  mita 25 kwa kwenda juu.


SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI LAKANUSHA KUTAKA KUWAAJIRI VIJANA 500

SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA UVUMI WA KUAJIRI VIJANA 500 NA KUWAPATIA MASOMO YA MAFUTA NA GESI


Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na maelezo kuwa:  " Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na Machi 2015, hivyo wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014. Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira  moja kwa moja baada ya kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3, kozi ya oil and gas management!...Ada kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014".

TPDC inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na kwamba TPDC haijafanya makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu suala hilo. TPDC inawaasa Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea, tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu zilizooneshwa hapo nchini.

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO,
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA

​​​​BWM Pensions Towers, Tower A,
​​​​Junction of Azikiwe /Jamhuri Streets
​​​P. O. Box 2774,
​​​Tel: +255 22 2200103/4
​​Dar-es-Salaam, Tanzania


WATOTO SITA WALAWITIWA KANISANI ARUSHA

Watoto sita wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.


Kamanda wa Polisi Arusha, Leberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapo kwa uchunguzi zaidi.

Wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru walikopelekwa kwa matibabu na kuangaliwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, watoto hao walidai kufanyiwa mchezo huo kwa nyakati tofauti  na wachungaji watatu wa kanisa hilo lililopo eneo la  Feed Force, Kwamorombo jijini Arusha.
 
Mmoja wa watoto hao anayesoma darasa la 4 katika shule ya msingi alieleza kuwa yeye na wenzake wamekuwa wakifanyiwa mchezo mchafu katika kanisa hilo baada ya wachungaji hao kuwapatia shilingi 2,000.

“Siku moja nilipofika shuleni wenzangu wakaniambia niende pale kanisani tukapewe hela, nilipofika niliwaona wenzangu wengine wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname akanifanyia kitendo kibaya na kunipa shilingi 2,000/- niliumia sana,’’ alisema mwanafunzi mmoja.

Mwanafunzi mwingine alisema amekuwa akitoroka shuleni na wenzake na kwenda kwa watumishi hao ambapo huwaingiza katika kanisa hilo na kujifanya wanawaombea baadaye huwafanyia mchezo mbaya.
 
Wanafunzi hao walieleza kuwa watumishi hao huwarubuni kwa kuwaeleza kuwa watawasaidia kuwasomesha iwapo watakuwa wakienda kwenye kanisa hilo na kuwaingilia.

Mzazi mmoja wa watoto hao, Julius, mkazi wa Kwamorombo alisema mtoto wake alimweleza kwamba amekuwa akifanyiwa mchezo mbaya na watumishi hao baada ya kupewa shilingi 2,000. Alisema aligundua hilo kufuatia tabia ya mtoto wake kuchelewa kurudi nyumbani.

Naye Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema ambaye alifika hospitalini kuwajulia hali watoto hao alisikitishwa na kitendo hicho na kulitaka jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vipimo vya kidaktari ili kupata ukweli wa tukio hilo.

“Nimeongea na mkuu wa mkoa, Magesa Mulongo ambaye ameahidi kulifuatilia kwa kina suala hili na kujua undani wake,’’ alisema Lema.

 

Hata hivyo, watoto hao baadaye walihamishiwa katika Hospitali ya Seliani kwa ajili ya vipimo zaidi huku taarifa za awali zikithibitishwa na daktari wa hospitali hiyo kuwa, baadhi yao walikutwa na michubuko na kupanuka sehemu za siri hali inayooneshwa kuingiliwa.





DEGE ECO - VILLAGE YAANZA UJENZI WA NYUMBA ZA NSSF KIGAMBONI


Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba yaliyofanyika jijini Dar es Salaam umeanza hivi karibuni.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zitakuwa tayari ifikapo Januari 2015. 
 
Mradi huo unajengwa kwenye eneo la eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018. 














IKIFIKA MACHI GHARAMA YA KUUNGANISHA UMEME NYUMBANI ITAKUWA BURE

Gharama za kuunganisha umeme wa majumbani zitatolewa bure kuanzia mwezi Machi mwakani baada ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, kukamilika kwa asilimia 90.

Aidha gharama za matumizi ya umeme wa majumbani na viwandani zitapungua kwa kiasi kikubwa baada ya mtambo huo kuanza kufanyakazi.

Msemaji Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, alisema hayo jana alipotembelea mtambo huo Kinyerezi akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa na Waandishi wa habari.

Alisema kuwa gharama za watumiaji wa umeme kwa Tanzania ziko chini kwa asilimia tano ukilinganisha na nchi za Uganda (asilimia 24) na Burundi (asilimia 20).
“Mtambo wa kusafirishia umeme wa gesi ambao ukubwa wake ni kama ule wa Ubungo umekamilika kwa asilimia 90.

Alisema kuwa serikali imeajiri wafanyakazi Watanzania kwa asilimia 95, na ifikapo Januari vijana 60, watapelekwa nchini China kwa masomo ili wapate ujuzi wakuendesha mitambo hiyo.

Mhandisi anayesimamia mradi huo, Saimoni Gilma, alisema mradi huo umetumia Dola za Marekani milioni 103, ambazo zote zimelipwa na Serikali ya Tanzania.
Alisema ujenzi wa miundombinu ya mitambo hiyo umekamilika kinachosubiriwa ni kuletwa kwa mitambo hiyo kutoka bandarini.

Aidha, nyumba za wafanyakazi, watakaoendesha mitambo hiyo zimekamilika kwa ajili ya kuanza kazi. Alifafanua kuwa mabomba ya gesi yaliotandazwa aridhini kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ni transfoma 200. Na yatawekewa ulinzi mkali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa helikopta itakayokuwa inazunguka usiku na mchana.

Alisema kuwa gharama za kuweka umeme majumbani zitagharamiwa na nchi ya Japan na Finland, wananchi watatakiwa kutoa sehemu ya viwanja vyao au mashamba ili kupisha bomba hilo kupita.


SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 23 SEPTEMBA 2014 HAPA

1_797b9.jpg
2_755c0.jpg
3_bbf6d.jpg
4_ab685.jpg
005_3863f.jpg
05_96e9e.jpg
5_5a7af.jpg
15_b219c.jpg
16_858ae.jpg
17_39785.jpg
18_6193f.jpg
20_c755e.jpg
21_e531c.jpg
22_9ac88.jpg
23_5a695.jpg
25_c0154.jpg
26_10fb0.jpg


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU