PAMOJA na kuwa na ulemavu wa kutokuwa na mikono yote miwili, Salim Mbela mkazi wa eneo la Delux, nje kidogo ya mji wa Songea, amefanikiwa kulima shamba la mahindi kubwa na zuri kwa kutumia miguu yake.
Ukiliona shamba hilo la Mbela licha ya kuwa na mahindi, pia lina maharage, magimbi na ndizi yaliyostawi na kupendeza.
Huwezi kuamini kuwa shamba hilo linalimwa na Mbela, ambaye ni mlemavu kwa kutumia miguu yake.
Ulemavu huo umemkuta na kulazimika kulima kwa
miguu, baada ya kukatwa mikono yake alipokuwa akidai kurejeshewa mahari
kutoka kwa wakwe zake.
Mbela anasema kuwa pamoja na ulemavu alioupata
ukubwani, hawezi kutembea mitaani kuomba omba, wakati bado mwili wake
una viungo vingine anavyoweza kuvitumia kujipatia mahitaji yake ya kila
siku.
Kilichosabisha kukatwa mikono
Mbela alizaliwa miaka 53 iliyopita akiwa na mikono miwili na mwenye afya tele, lakini misukosuko ya maisha imemfanya leo abaki hana mikono yake miwili, huku akiishi peke yake.
Mbela alizaliwa miaka 53 iliyopita akiwa na mikono miwili na mwenye afya tele, lakini misukosuko ya maisha imemfanya leo abaki hana mikono yake miwili, huku akiishi peke yake.
Anaeleza kuwa kabla ya kuwa mlemavu, aliwahi
kuajiriwa na Jeshi la Polisi, akifanyia kazi Kituo cha Polisi Makuyuni
mkoani Arusha miaka ya nyuma, lakini alicha kazi hiyo baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Baada ya hali hiyo, aliona bora arudi nyumbani kwao Kijiji cha Malumba wilayani Tunduru ili kuendelea kupata matibabu.
Mbela anasema kuwa alipofika kijijini kwao, aliendelea kupata matibabu na baadaye akapona.
Akizungumza kwa kusaidiwa na rafiki yake wa karibu ambaye amejitambulisha kwa jina la Zacharia Dikala, maarufu kama Babu Masai, Mbela anasema kuwa alikutana na matatizo ya kukatwa mikono miaka minne iliyopita.

Mbela ambaye pia ni baba wa watoto Mwanabibi Salim
(28), Siku Salim (19) na Said Salim (24) anaeleza kuwa akiwa na mkewe
na familia yake, siku moja ali kwenda nyumbani kwa wakwe zake waliokuwa
wakiishi katika kijiji hicho cha Malumba na kuchukua mbuzi wake aliotoa
mahari miaka ya nyuma wakati akimchumbia mkewe ambaye ndiye aliyemzalia
watoto hao.
Anasema kuwa wakati huo alikuwa na nguvu na
alitumia mabavu kufanya fujo, hadi akafanikiwa kufika zizini na kupora
mbuzi, bila kujua kama maisha yake yange badilika na kuishia pabaya.
Hata hivyo, anajutia kitendo hicho akisema kwamba iwapo angefahamu mapema yataka yomkuta, asingethubutu kwenda kufanya fujo hizo.
Hata hivyo, anajutia kitendo hicho akisema kwamba iwapo angefahamu mapema yataka yomkuta, asingethubutu kwenda kufanya fujo hizo.
“Nilikuwa najiamini sana, nilikuwa na nguvu sana,
nikaamua kwenda ukweni kwangu kufuata baadhi ya mifugo yangu, niliyotoa
mahari wakati namposa mke wangu,” anasimulia na kuongeza:
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog