Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF
limetangaza majina ya wachezaji wa
kiafrika watakaowania tuzo ya mchezaji
bora wa Afrika kwa mwaka 2013 na
Mchezaji bora wa Afrika anayechezea
vilabu vya ndani ya Afrika mwaka 2013.
Katika majina hayo yapo majina mawili
ya wachezaji wanaotoka Afrika Mashariki
ambao ni Victor Wanyama raia wa Kenya
anachezea Southampton FC ya England
ambaye ni miongoni mwa wachezaji 25
watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa
Afrika, huku Mbwana Samatta raia wa
Tanzania anayechezea klabu ya TP
Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Congo yeye ameteuliwa kuwania tuzo
ya Mchezaji bora wa Afrika anayechezea
timu za Afrika.
Wachezaji 25 watawania tuzo ya mchezaji
bora wa Afrika na 21 Mchezaji bora wa
Afrika anachezea timu za ndani ya
Afrika.
Washindi wa tuzo hizo wanatarajiwa
kutangazwa Januari 9, mwaka 2014 mjini
Lagos nchini Nigeria.
Orodha kamili ya wachezaji
waliotangazwa na CAF na timu
wanazotoka hii hapa chini.
1. Ahmed Musa - Nigeria - CSKA Moscow
2. Asamoah Gyan - Ghana - Al Ain
3.Dame N'Doye - Senegal - Locomotiv
Moscow
4. Didier Drogba - Cote d'Ivoire -
Galatasaray
5. Emmanuel Emenike - Nigeria -
Fenerbahce
6. Islam Slimani - Algeria - Sporting
Lisbon
7. John Mikel Obi - Nigeria - Chelsea
8. Jonathan Pitroipa - Burkina Faso -
Stade Rennais
9. Kévin Constant - Guinea - AC Milan
10. Kwadwo Asamoah - Ghana - Juventus
11. Luís Carlos Almada Soares (platini) -
Cape Verde - AC Omonia
12. Mehdi Benattia - Morocco - AS Roma
13. Mohamed Aboutrika - Egypt - Al Ahly
14. Mohamed Salah - Egypt - Basel FC
15. Nicolas Nkoulou - Cameroon -
Marseille
16. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon -
Borussia Dortmund
17. Ryan Isaac Mendes da Graça - Cape
Verde - Lille
18. Saladin Said - Ethiopia - Wadi Degla
FC
19. Seydou Keita - Mali - Dalian Aerbin
F.C
20. Sofiane Feghouli - Algeria - Valencia
21. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves
22. Victor Wanyama - Kenya -
Southampton FC
23. Vincent Enyeama - Nigeria - Lille
24. Yao Kouassi Gervais 'Gervinho' - Cote
d'Ivoire - AS Roma
25. Yaya Toure - Cote d'Ivoire -
Manchester City
1. Adane Girma - Ethiopia - St George
2.Ahmed Fathi - Egypt - Al Ahly
3. Alexis Yougouda Kada - Cameroon -
Coton Sport
4. Ali Machani - Tunisia - CAB
5. Bapidi Fils Jean Jules - Cameroon -
Coton Sport
6. Daine Marcelle-Klate - South Africa -
Orlando Pirates
7. Fakhreddine Ben Youssef - Tunisia -
CSS
8. Getaneh Kebede - Ethiopia - Bidvest
Wits
9. Idrissa Kouyate - Cote d'Ivoire - CS
Sfaxien
10. Iheb Msakni - Tunisia - Esperance
11. Luyanda Lennox Bacela - South Africa
- Orlando Pirates
12. Mbwana Samatta - Tanzania - TP
Mazembe
13. Moez Ben Cherifia - Tunisia - EST
14. Mohamed Aboutrika - Egypt - Ahly
15. Rainford Kalaba - Zambia - TP
Mazembe
16. Senzo Meyiwa - South Africa -
Orlando Pirates
17. Soumbeila Diakite - Mali - Stade
Malien
18. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves
19. Tresor Mputu - DR Congo - TP
Mazembe
20. Waleed Soliman - Egypt - Al Ahly
21. Yannick N'djeng - Cameroon - EST
Sunday, November 17, 2013
MBWANA ALI SAMATA ATAJWA KATIKA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA
RIPOTI YA MAREKANI KUHUSU USAFIRISHAJI WA BINADAMU 2013 ISOME HAPA
Marekani imetoa ripoti
inayozungumzia usafirishaji wa binadamu ya mwaka 2013, huku ikiitaja Tanzania kuwa kinara wa kunyanyasa wasichana, kuwatumikisha katika ngono na usafirishaji wa binadamu.
Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya nchi hiyo inayohusika na diplomasia (US Department of State, Diplomacy in Action), pia inaitaja Tanzania kuwa ni kitovu cha njia ya kusafirisha wanawake, watoto na wanaume ambao hutumikishwa kwenye kazi za mashambani na biashara ya ngono.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa Julai mwaka huu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Seneta John Kerry inaweka bayana kwamba biashara ya usafirishaji wa binadamu hufanywa na baadhi ya ndugu na marafiki ambao hutoa ahadi kwa wahusika kwamba wanakwenda kuwasomesha au kuwatafutia ajira nzuri mijini.
“Unyonyaji wa wasichana wadogo na utumikishaji majumbani ndilo tatizo linaloongoza, ingawa kesi za watoto kusafirishwa kwa ajili ya biashara ya ngono katika mpaka wa Tanzania na Kenya zinaongezeka. Pia, wasichana wananyonywa kwenye maeneo ya utalii,” inasema sehemu ya ripoti hiyo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto kutoka Burundi na Kenya, watu wazima kutoka Bangladesh, Nepal, Yemen na India wanatumikishwa kufanya kazi kwenye sekta za kilimo, madini na majumbani nchini Tanzania.
“Baadhi ya raia kutoka nchi jirani huingia Tanzania kwa hiari yao, lakini hulazimishwa kufanya kazi majumbani kabla ya kupelekwa kutumikishwa kwenye biashara ya ngono Afrika Kusini, Ulaya na Mashariki ya Kati,” inaeleza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alimtaka mwandishi kumtumia ripoti hiyo kwa njia ya barua pepe ili aweze kuisoma na kuitolea maelezo.
Alipotafutwa siku ya pili, alisema kuwa ameipokea na kuikabidhi ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) ili ifanyiwe kazi na baadaye kutoa majibu.
“Ripoti niliipata nikaikabidhi ofisi ya DPP kwa kuwa wao ndio wanaoweza kuitolea maelezo baada ya kuisoma. Maoni yangu lazima yawe ya kitaalamu siwezi kusema bila kupata taarifa kutoka kwao,” alisema. Lawama kwa Serikali Ripoti hiyo inaitupia lawama Tanzania kwa kutokuwa na sheria thabiti za kupambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu, huku ikitolea mfano namna ilivyoshindwa kuwasaidia raia wake waliokuwa wakinyanyaswa nje ya nchi.
“Kamati ya Serikali ya kupambana na usafirishaji binadamu, haijachukua hatua za kutosha katika kutekeleza mpango mkakati wa kupambana na vitendo hivyo,” inaeleza na kuongeza:
“Serikali imeshindwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa usafirishaji wa binadamu kama ambavyo inaelekezwa kwenye sheria ya kudhibiti biashara hiyo ya 2008.”
Taarifa hiyo inaitaka Tanzania kuongeza nguvu katika kutekeleza sheria ya kudhibiti biashara ya kusafirisha binadamu ya 2008 kwa kuwakamata na kuwashtaki wahusika wote, lakini ikaikosoa kwa kusema inatoa adhabu ndogo kwa mtu anayebainika kufanya makosa, ikiwa ni pamoja na kumhukumu kwenda jela miaka 10, kulipa faini au vyote viwili kwa pamoja.
“Sheria hiyo haifanani na nyingine kama za mtu anayepatikana na kosa la kubaka au kufanya kosa jingine la jinai. Mamlaka imesema ina kesi nne inazozichunguza, saba zipo mahakamani toka mwaka jana, zikiwepo mbili mpya,” inasema ripoti. Pia, Serikali ya Tanzania imelaumiwa kwa kushindwa kuripoti maendeleo ya uchunguzi wa maofisa wake waliotuhumiwa kujihusisha na biashara ya usafirishaji binadamu. LHRC na TGNP Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema tatizo la usafirishaji wa binadamu pia linachangiwa na wasichana kuwa na tamaa ya maisha mazuri, hivyo kukubali ahadi ambazo hupewa kwamba wanapelekwa kusoma, wasifahamu wanarubuniwa.
“Wengi wanatamani kwenda ‘majuu’ wakidhani watapata elimu, lakini baadaye wanaingizwa kwenye vitendo vinavyowafedhehesha na kuwafanya wakate tamaa kabisa,” alisema. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya alisema katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wasichana waliochukuliwa vijijini kwenda mijini kufanya kazi.
Alisema pamoja na tatizo hilo kuongezeka hapa nchini, hakuna tafiti za kutosha ambazo zimefanywa na wadau mbalimbali kuonyesha madhara yaliyopatikana hadi sasa. “Katika siku za usoni kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya kunyimwa chakula, kupigwa na kufukuzwa kazi huku wasichana wengine wakitumika kwenye biashara ya ngono,” alisema na kuongeza:
“Ripoti hii isiishie kwenye makabrasha bali ifanyiwe kazi ili jamii yote ijue kuwa hili ni tatizo.” Ripoti hiyo inabainisha kuwa watu 47,000 pekee ndio walioweza kuokolewa mwaka jana kutoka kwenye mazingira ya utumikishwaji kati ya milioni 27 waliopo katika hali hiyo duniani. Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi 44 ambazo zinajaribu kupambana na biashara hiyo, lakini hali inazidi kuwa mbaya zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)