Facebook Comments Box

Wednesday, September 6, 2017

ZAHANATI YA VINGUNGUTI YAPEWA CHEO CHA NYOTA NNE



unnamed
Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Ilala ambaye pia Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto ameeleza sababu zilizopelekea Zahanati ya Vingunguti kufuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali kupitia wakaguzi wake (TRN) na imekuwa miongoni mwa Zahanati tano zilizofuzu.
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti  wa Kamati ya Zahanati Ibrahim Aeshi Nduze, Naibu Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa hali ya mara ya kwanza katika zahanati hiyo haikuwa shwari lakini kwa jitihada zake na kushirikiana na Halmashauri na Serikali alifanikiwa kufanya mambo mbalimbali katika maboresho ya zahanati hiyo na hatimae imefanikiwa kupewa hadhi ya nyota nne.
Akiyataja mambo waliyoweza kuyafanya katika Zahanati hiyo ni pamoja na Ununuzi wa Gari ya Wagonjwa (Ambulance), Mashine ya Kufulia,Jenereta, Choo kwa kinamama wanaojifungua, utanuzi wa maabara, ufungaji wa feni nne, mashne tatu za kupmia uzito kwa watoto,kipimo cha presha na kiti cha kubebea wagonjwa.
Zahanati nyingine zilizoweza kupandishwa hadhi Halmashauri ya Ilala ni pamoja na Zahanati ya Tabata, Mongo la Ndege, Kinyerezi na Kadlugambwa.
Taarifa kutoka Kamati ya Zahanati imeeleza kuwa mwanzo zahanati yetu ilikua na nyota mbili ambapo hizo zahanati nyingine zilikua na nyota tatu hivyo vingunguti imepanda nyota mbili.
Kamati hiyo imewashukuru wananchi kwa mawazo, maoni, na changamoto walizozitoa ambazo zimezifanyiwa kazi na ku pelekea zahanati hiyo kupata nyota mbili za ziada, kamati memshukuru pia Diwani Omary Said Kumbilamoto kwa kuwaongoza, kuwashauri, na kutoa mchango wa hali na mali ii kufikia malengo.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU