Facebook Comments Box

Thursday, August 14, 2014

MTU MMOJA AHOFIWA KUWA NA EBOLA DAR ES SALAAM

Mhudumu wa afya akiwa katika hali ya tahadhari ya Ebola huko Afrika Magharibi

Kuna taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Afya ya Tanzania Nsachris Mwamaja mtu huyo ana asili ya Afrika
Magharibi ambaye ni mkazi wa mji wa Dar es Salaam ambaye alifika katika hosptali moja akiwa na homa kali ikiwa ni dalili mojawapo ya ugojwa huo .
Bwana Mwamaja amesema mgonjwa huyo ambaye ni mtoto wa makamo tayari ameshatengwa na yupo chini ya uangalizi wa karibu madaktari katika hosptali Temeke ambayo ni ndio iliyotengwa kwa ajili ya watakaohisiwa kuwa na ugonjwa huo.
Amesema sababu nyingine ya kuhisiwa kwa mtu huyo kuwa huenda ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo ni kwa vile hivi karibuni alitokea nchini Benin.
Hii ni mara ya kwanza ya kuwepo kwa taarifa za mtu kuhisiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Tanzania. Taarifa hizi zinakuja baada ya hapo awali serikali ya nchi hiyo kukanusha taarifa iliyotolewa na gazeti moja la udaku kuwa kuna mgonjwa mmoja wa Ebola aliyegundulika nchini Tanzania.
CHANZO: BBC SWAHILI


UGONJWA WA EBOLA WAZUA TAFRANI SHINYANGA


Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga, kwa siku mbili mfululizo
walikumbwa na kiwewe, baada ya kuenea uvumi kwamba kuna
mgonjwa wa mwenye homa hatari ya ebola, aliyefikishwa katika
Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
Taarifa za kuwepo kwa mgonjwa huyo, zilidai kuwa mgonjwa huyo
alitoka katika moja ya mitaa ya Manispaa ya Shinyanga na  alikuwa
akitokwa damu puani na mdomoni kabla ya kuzimia.
Akizungumzia hali hiyo jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,
Dk Ntuli Kapologwe alisema mgonjwa huyo ambaye alikuwa
akitokwa damu mdomoni na puani, alifika hospitalini hapo juzi na
baada ya kufika wauguzi na madaktari walitaharuki.
Kwa mujibu wa Dk Kapologwe, mgonjwa huyo alipelekwa chumba
cha wagonjwa mahututi (ICU), huku baadhi ya wauguzi na
madaktari wakimkimbia hali iliyotia hofu kwa baadhi ya wahudumu
na hata wagonjwa hospitalini hapo.
Hata hivyo, Dk Kapologwe alisema baada ya uchunguzi wa awali,
ilibainika kuwa mgonjwa huyo ana matatizo ya kutokwa damu mara
kwa mara na hajaambukizwa virusi hao wa ebola.
Akielezea namna mkoa ulivyojiandaa kukabiliana na ugonjwa huo
uliokwishaua zaidi ya watu 1,000 katika nchi za Afrika Magharibi,
Dk Kapologwe alisema waganga wakuu katika halmashauri zote sita
za wilaya mkoani Shinyanga, wameshajiandaa.
Alisema wamekubaliana atakapogundulika mtu mwenye dalili za
ugonjwa huo, taarifa itolewe mara moja katika ngazi ya mkoa,
ambako kuna timu maalumu ya wataalamu iliyoandaliwa
kushughulika na ugonjwa huo hatari.
Baada ya taarifa kutolewa kwa mujibu wa Dk Kapologwe, timu hiyo
itathibitisha kama mgojwa ana dalili zote za ebola na taarifa
kutolewa kwa umma.
Wakati ugonjwa huo ukisababisha kiwewe mkoani Shinyanga,
mkoani Kagera, Mkuu wa Mkoa, Fabian Massawe ameshauri wakazi
wa mkoa huo kuwa macho na tayari kutoa taarifa kwenye vituo vya
afya vilivyo jirani waonapo mtu mwenye dalili  za ugonjwa huo.
Alitoa mwito huo kupitia kwa waandishi wa habari aliozungumza
nao jana ofisini kwake mjini hapa, baada ya kuibuka taarifa kuwa
Rwanda kulikuwa na mtu anayehisiwa kuwa na ebola.
Hata hivyo, Waziri wa Afya wa Rwanda, Agnes Binagwaho alisema
juzi kuwa mwanafunzi mmoja wa Ujerumani aliyefika nchini humo
akitokea Liberia,  alihisiwa kuwa na ugonjwa huo lakini baada ya
sampuli ya damu yake kupimwa katika maabara za kimataifa,
hakukutwa na ugonjwa huo.
Massawe alisema Mkoa wa Kagera unapakana na nchi mbalimbali
za Afrika Mashariki na pia upo mwingiliano wa watu na shughuli
mbalimbali za kijamii.
Alisema nchi jirani zikipata mlipuko wa ugonjwa huo, upo
uwezekano wa kuvuka mipaka na kuingia mkoani Kagera, hivyo ni
wajibu wa kila mmoja kutoa taarifa akiona mtu anayedhaniwa kuwa
na ugonjwa huo.
Dalili za ugonjwa huo unaoenezwa na virusi vya ebola ni pamoja
na kutokwa na damu sehemu mbali mbali za mwili, kuumwa na
kichwa, mwili kuishiwa nguvu, maumivu ya misuli na hatimaye kifo.
Ugonjwa huo unaambukizwa kwa kugusa damu na majimaji ya
mgonjwa pamoja na kugusa vifaa au nguo za mgonjwa.
Massawe alisema Kagera wamechukua hatua kwa kuweka mikakati
kuhakikisha mlipuko wa ugonjwa  hauingii nchini  kupitia mipakani.
Miongoni mwa halmashauri ambazo zimeelekezwa kuchukua
hadhari kutokana na kuwa mpakani mwa nchi, ni wilaya ya Bukoba,
Missenyi, Karagwe, Kyerwa na Ngara.


HADITHI FUPI YENYE MAFUNZO KWA WANA NDOA

Siku moja niliingia nyumbani nikamkuta mke wangu akiniandalia chakula cha usiku. Nilimshika mkono na kumwambia: “Nina jambo ninalotaka kukueleza.” Alikaa na kunisikiliza kwa makini. Dalili za wasiwasi nilikuwa nikizishuhudia machoni mwake. Ghafla nilijikuta katika hali ya kushindwa kukifungua kinywa changu.
Lakini ilikuwa ni lazima ajue ninachokifikiria, hivyo nilipiga moyo konde, nikamwambia kwa upole: “Ninataka tuachane.” Hakuonekana kuudhika kwa hoja niliyokuwa nimeiwasilisha mbele yake, bali aliniuliza kwa sauti ya upole kabisa: “Kwa nini?” Nilijaribu kulikwepa hilo swali, hivyo
alighadhibika sana na kuniambia kwa sauti ya juu: “Wewe si mwanaume!” Usiku ule hatukusemeshana, na muda wote alikuwa akilia. Nilitambua kuwa alitaka kujua kitu gani kimetokea katika ndoa yetu. Lakini sikuweza kumpa jibu lenye kuridhisha; kwa sababu sikuwa na mapenzi naye tena, moyo wangu ulikuwa umetekwa na binti mwingine aitwaye Jane. Nilimsikitikia sana!
Huku nikiwa na hisia za hatia moyoni mwangu, niliandika pendekezo la
talaka ambalo lilieleza kuwa atachukua nyumba yetu, gari na shea ya asilimia 30 ya kampuni yangu. Mke wangu aliitazama karatasi hiyo kisha akaichana na kuitupa kwenye ndoo ya takataka.
Huyu ni mwanamke aliyekuwa ameishi nami kwa muda wa miaka kumi alikuwa
amegeuka kuwa kama mgeni kwangu. Nilisikitika sana na kumuomba radhi kwa kumpotezea muda, rasilimali na nguvu zake lakini sikuweza kutengua kauli yangu kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana Jane na nilikuwa nimezama kweli kweli ndani ya huba lake na kuwa teja wa penzi lake. Hatimaye alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo nilikuwa nikitarajia kuliona.
Kilio chake kwangu kilikuwa kama faraja. Wazo la talaka lililonitawala kwa wiki kadhaa lilikuwa likizidi kupata nguvu na sasa lilionekana kuwa wazi kabisa. Siku iliyofuata nilirudi nyumbani nikiwa nimechelewa na kumkuta akiandika kiandika kitu mezani. Sikutaka kula chochote zaidi ya kuelekea moja kwa moja kitandani kwa sababu nilikuwa nimechoka sana kutokana na mishemishe za siku hiyo nikiwa na Jane. Niliposhtuka, bado alikuwa hajatoka mezani. Sikujali hata kidogo, nikageuka na kuendelea kuuchapa usingizi. Asubuhi alinipatia masharti ya talaka: hakutaka
mali yoyote kutoka kwangu, bali alitaka kuwe na muhula wa mwezi mmoja kabla ya talaka.
Alitaka kwamba katika kipindi hicho tujaribukuishi kama kawaida kwa kadiri iwezekanavyo. Hoja yake ilikuwa wazi: mtoto wetu alitarajia kufanya mitihani ya shule ndani ya mwezi huo na hakutaka tumchanganye kwa tukio la talaka. Hili nililikubali. Lakini alikuwa na nyongeza:
alinitaka nikumbuke siku ya ndoa yetu nilipomnyanyua kumpeleka chumbani kwetu. Alitaka kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mzima niwe nambeba kila siku asubuhi kumtoa chumbani mpaka mbele ya mlango wa nje ya nyumba. Nilihisi kuwa alikuwa ameshikwa na wendawazimu. Nilikubali ombi lake kwa sababu niliona kuwa mwezi mmoja sio kitu, kwani nilitaka tuachane.
Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya talaka yaliyotolewa na mke wangu. Alicheka sana na kuona kuwa ni upuuzi. “Hata akitumia hila gani lazima apewe talaka,” alisema Jane kwa masihara. Tangu nilipoelezea nia yangu ya kutaka kuachana naye, hatukuwa na uhusiano wa kimwili na mke wangu. Hivyo nilipombeba siku ya kwanza, sote tulionekana kutokuwa na uchangamfu. Mtoto wetu alifurahi na kupiga makofi: “Baba amembeba mama”. Kauli yake ilinipa maumivu moyoni. Kutoka chumbani mpaka barazani, kisha mlangoni, nilitembea mita kumi nikiwa nimembeba mikononi mwangu. Aliyafumba macho yake na kuniambia
kwa upole na ulaini: “Usimwambie mtoto wetu kama tunaachana.” Nilikubali kwa kutikisha kichwa huku
nikiwa nimefadhaika. Nilipofika nje
nilimshusha akaenda kituoni kusubiri basi, nami nikachukua gari langu na kwenda ofisini nikiwa peke yangu. Siku ya pili tulijaribu kutoonesha hali yoyote ya mifarakano. Aliegemea kifuani kwangu nikahisi manukato mazuri ya blauzi yake. Nilibaini kuwa sikuwa nimemtazama vizuri mke wangu kwa muda mrefu. Uso wake ulikuwa umeanza kuwa na mikunjo na nywele zake zilikuwa zimeanza kubadilika. Ndoa yetu ilikuwa imemfanya achoke. Kwa dakika kadhaa niliduwaa na kuwaza kile nilichokuwa nimemfanyia.
Siku ya nne nilipombeba nilihisi aina ya
ukaribu na mvuto ikirejea. Huyu ni mwanamke aliyekuwa amenipa miaka
kumi ya uhai na maisha yake. Siku ya tano na ya sita, kwa mara nyingine, niliona hali ya ukaribu na mvuto fulani ikirejea kati yetu. Sikumsimulia Jane kuhusu hali hii. Kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo nilivyozidi wepesi wa kumbeba. Yumkini ilisababishwa na
ile hali ya kumbeba kila siku kiasi cha kumuona kuwa ni mwepesi. Asubuhi moja alikuwa akichagua nguo ya kuvaa. Alijaribu nguo kadhaa lakini hakupata
inayomfaa. Alishusha pumzi na kusema: “Nguo zangu zote hazinienei,
zimekuwa kubwa”. Nilibaini kuwa alikuwa
amekonda na ndiyo maana niliweza kumbeba kwa urahisi. Nilisikitika kwa
sababu nilihisi kuwa alikuwa amebeba mambo mengi moyoni mwake. Hivyo nilimsogelea na kukipapasa kichwa chake. Ni wakati huo ambapo mtoto wetu aliingia na kusema: “Baba sasa ni muda wa kumbeba mama”. Tukio la kumuona
baba yake akiwa amembeba mama yake
lilimuathiri na kuwa sehemu muhimu sana ya maisha yake. Mke wangu alimuita na kumkumbatia kwa upendo.
Niligeuza uso wangu pembeni, sikutaka
kuangalia tukio hilo nisije nikabadilisha uamuzi wangu wa talaka. Nilimnyanyua na kumbeba mke wangu,nikatembea kutoka chumbani, sebuleni mpaka nje. Aliizungusha mikono yake mizuri shingoni kwangu, nami nikamshikilia vizuri; ilikuwa kana kwamba ni siku ile ya harusi yetu. Lakini wepesi wa mwili wake ulinifanya niwe mwenye huzuni. Siku ya
mwisho nilipombeba niliingiwa na uzito
wa kupiga hatua. Wakati huo mtoto wetu tayari alikuwa shule. Nilimshikilia vizuri na kusema: “Sikuwa nimejua kuwa maisha yetu yamekosa mvuto”. Niliwasha gari kuelekea ofisini, niliamua kupita kwa Jane.
Nilipofika nilitoka haraka bila hata kuubana mlango wa gari. Nilikuwa na wasiwasi nisije nikaghairi nia yangu…
Nikapandisha ngazi. Jane alipofungua
mlango nilimwambia: “Samahani Jane, sitaki kuachana na mke wangu”. Alinitazama kwa mshtuko na kunigusa kwenye paji la uso. “Una homa?” alisema. Niliutoa mkono wake na kumwambia: “Samahani Jane, sitaki kumuacha mke wangu. Yawezekana maisha yangu na mke wangu yalikosa uchangamfu kwa sababu hatukuwa karibu, sio kwa sababu hatukupendana. Sasa nimebaini kwamba kwa kuwa nilimbeba siku ya ndoa yetu, ninapaswa kuendelea kufanya hivyo mpaka kifo kitutengenishe.” Jane alionekana kushtuka sana. Alinizaba kibao, akaubamiza mlango na kuanza kulia. Nilimuacha nikapanda gari na kuondoka. Njiani nilipita kwenye duka la maua nikaagiza shada la maua kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza ujumbe unaotakiwa kuandikwa juu ya kadi nikatabasamu na kumwambia aandike: “Kila siku asubuhi nitakubeba mpaka kifo kitakapotutenga nisha”.
Jioni nilifika nyumbani nikiwa na maua mkononi, tabasamu usoni, nikapandisha ngazi mpaka ndani. Nilipofika chumbani mke wangu alikuwa amelala akiwa amefariki dunia. Kumbe alikuwa akipambana na KANSA kwa miezi kadhaa lakini sikujua kwa sababu nilikuwa nimetekwa na Jane. Bila mimi kufahamu, kumbe marehemu mke wangu alijua kwamba muda si mrefu atafariki dunia na alitaka kuniokoa dhidi ya fikra yoyote mbaya kutoka kwa mtoto wetu kama tungeachana muda mfupi kabla ya kifo chake. Angalau machoni mwa mwanangu naonekana kuwa mume
mwenye upendo…
WAPENDANAO NATAKA MJIFUNZE
(1) Wengi wanatengana si kwa sababu hawapendani, bali hawapeani muda wa kusikilizana.
(2)Wengi wanaamini ukiachana na mpendwa wako ni lazima muwe maadui.
(3)Busara ndani ya pendo ni zaidi ya mali na pesa.....
(4) Kaa karibu na mkeo na familia yako muda wote ili ujue nini kinawasibu na uwasaidie katika utatuzi.
(5)Mkeo/mmeo hupenda wewe uwe na furaha hata kama yeye anaumia.


MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 14/08/2014

 



ANGALIA JINSI KIBONDE NA GARNER WALIVYO FIKISHWA MAHAKAMANI

Watangazaji Ephraim Kibonde (wa kwanza kushoto) na
mwenzake Gardner Habash (wa pili kulia) wakielekea
kizimbani.

Watangazaji hao wakiongozwa na maofisa wa polisi
kuelekea mahakamani.

...Wakiingia mahakamani.

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na
mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya
Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na
kudharau amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.
Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili
wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta
Wambura.
Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo
Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika
eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha
gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja
wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu
itakaposikilizwa tena.(Picha na Shakoor Jongo / GPL)


MKE WA AFANDE SELE (MAMA TUNDA) AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia hivi pune ni kuwa msanii mkongwe Selemani Msindi maarufu kama Afande sele amefiwa na mke wake. Habari kamili zitakujia hapa baada ya muda mfupi ujao
Afande sele akiwa na marehemu mke wake na mtoto wake Tunda



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU