Wednesday, September 12, 2012
RAIS KIKWETE AKIWA KATIKA ZIARA RASMI YA KISERIKALI NCHINI KENYA
SIMBA WACHUKUA NGAO YA HISANI
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Mkongoro Mahanga akimkabidhi Ngao ya Hisani
nahodha wa Simba, Juma Kaseja baada ya kuifunga Azam FC 3-2 katika
mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam
Add caption |
Mshambuliaji
wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Azam FC, Aggrey Morris katika
mchezo wa Ngao ya Hisani uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam. Simba imeshinda 3-2. Mapato ya mchezo huo yataelekezwa katika
shughuli za kijamii Hospitali ya Temeke.
Mashabiki wa Simba
Akuffo akijaribu kuleta simanzi kwenye lango la Azam |
Heka heka katika lango la Azama FC
SIMBA KUJIONDOA LIGI KUU
Mwandishi wa habari za michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba Siku moja baada ya kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF kutoa maamuzi juu ya mapingamzi ya Simba dhidi ya wachezaji Kelvin Yondani na Mbuyu Twitte kuichezea klabu Yanga – kwa kuwaidhinisha wachezaji hao kuichezea Yanga. Leo hii klabu ya Simba imesema inafikiria hatua za kuchukua juu ya uamuzi huo wa kamati ya Alex Mgongolwa.
Kwa taarifa za kuaminika alizozipata Shaffih kutoka ndani ya uongozi wa Simba ni kwamba kamati ya utendaji ya klabu hiyo itakutana usiku wa leo (sept 11) kujadili hatua za kuchukua huku baadhi ya wajumbe wakisema kutokana na uonevu wanaotendewa na TFF itabidi wajitoe kushiriki kwenye ligi kuu kwa sababu hawana imani na shirikisho hilo.
Simba inalalamika kwamba wachezaji wote wawili Mbuyu Twitte na Kelvin Yondan wamesajiliwa na Yanga isivyo halali. Kwa upande wa Twitte walitaka walipwe fedha zao $32,000 walizompa mchezaji huyo na akasaini nao mkataba kabla ya Yanga kuwazidi kete na kumsainisha mkataba mpya beki huyo aliyekuwa akiichezea APR ya Rwanda, na pia walitaka Twitte afungiwe kwa sababu alisaini mkataba na kalbu zote mbili kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Kwa upande wa Yondani Simba wanadai mchezaji huyo ni halali yao kwa sababu bado ana mkataba na klabu hiyo, pia wakataka Yanga iadhibiwe kwa kitendo cha kufanya mazungumzo na mchezaji ambaye bado ana mkataba na klabu yake ya zamani lakini jana kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF ikatoa maamuzi ya kuwaidhinisha Twite na Kelvin Yondan kwenda Yanga, maamuzi ambayo Simba wamesema sio sahihi.
Subscribe to:
Posts (Atom)