Facebook Comments Box

Monday, June 23, 2014

HAWA NDIO WACHEZAJI 11 WALIOTEMWA YANGA: CHUJI NA LUHENDE WAMO.


Ikiwa dirisha la usajili limeshafunguliwa tangu wiki iliyopita kwa timu
mbali mbali kuanza kufanya usajili wa wachezaji na zingine zikianza
mazoezi, timu ya Young Africans imeweza kuweka wazi majina ya
awali ya baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia katika msimu
ujao wa 2014/2015.
Young Africans ambayo msimu uliopita ilikua na kikosi bora kabisa
ambacho kiliweza kuwatoa jasho Mabingwa wa Kihistoria Barani
Afrika timu ya Natioal Al Ahly katika mashindano ya Klabu Bingwa
Afrika, ambapo Mabingwa hao wa kutoka nchini Misri waliweza
kusonga mbele kwa mikwaju ya penati.
Msimu uliopita Young Africans ilikuwa na kikosi cha wachezaji 30
kutoka timu ya Wakubwa na wachezaji watano (5) kutoka timu ya
vijana  (U20) waliokuwa wamepandishwa kwa ajili kupata uzoefu na
kuingozea nguvu timu ya wakubwa katika michezo mbalimbali.
Kutokana na ripoti ya Benchi la Ufundi iliyowasilishwa mara baada
ya kumalizika kwa Msimu wa Ligi Kuu 2013/2014 baadhi ya
wachezaji hawataitumikia tena Yanga SC kwenye msimu ujao,
wachezaji 11 wamemaliza muda wao na kumalizana na uongozi
hivyo wapo huru kujiunga vilabu mbalimbali:
Wachezaji hao ni:
1. David Luhende
2. Athuman Idd "Chuji"
3. Geroge Banda -U20
4. Yusuph Abdul -U20
5. Rehani Kibingu -U20
6. Hamisi Thabiti
7. Reliants Lusajo
8. Bakari Masoud - U20
9. Shaban Kondo
10. Abdalllah Mguhi "Messi" U-20
11. Ibrahim Job
Hii ni orodha ya awali ya wachezaji ambao hawataitumikia Yanga SC
msimu ujao, huku zoezi la usajili likiendelea kujaza baadhi ya nafasi
zilizopo kulingana na maelekezo ya Benchi la Ufundi.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU