Facebook Comments Box

Monday, June 16, 2014

UCHUNGUZI: SIMU YA MKONONI ZINAATHIRI MBEGU ZA KIUME

Baadhi ya watu wanahisi kuwa uchunguzi zaidi unahitajika
Uchunguzi wa utafiti kutoka chuo kikuu cha Exeter nchini
Uingereza, unaonyesha kuwa kiwango cha mbegu za uzazi za
wanaume huathiriwa kwa kuweka simu za mkononi kwenye mifuko
ya suruali.
Hata hivyo ,mwana sayansi wa maswala ya uzazi na
shahawa,alisema kuwa ushahidi huo bado haukuwa na uhakika
wowote hivyo basi simu yake bado inaendelea kukaa mfukoni
mwake.
Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la 'Environment
International' ulilaumu mnunurisho wa kielectromagnetiki kuwa
chanzo kikuu.
Lilichanganua tafiti kumi tofauti kuonyesha ubora wa shahawa
ikihusisha wanaume 1,492.Hii ilijumuisha kupimwa kwa shahawa
zilizowekwa wazi kwa mnunurisho wa simu za rununu, kwa
maabara na udadisi wa wanaume katika cliniki za uzazi
Kiongozi wa uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews aliambia BBC kuwa
kutokana na uchunguzi huo,moja tu ndio ulionyesha uhusiano kati
ya utumizi wa simu na kudidimia kwa ubora wa shahawa.
"Nafikiri kwa mwanamume wa makamu hakuna haja ya kuingiwa na
hofu,iwapo unajua una uwezekano wa kuwa na shida ya kizazi basi
itakuwa jambo la busara kutoweka simu mfukoni ,pia kugeuza
mtindo wako wa kula."
Mbegu za uzazi za wanaume zinasemekana kuathirika kutokana na simu za mkononi
'Uchunguzi zaidi'
Alikubali kukosolewa na wana sayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi zaidi.
Dkt,Mathews alimaliza kwa kusema"hili ni jambo la kusisimua lakini hatusemi kwa uhakika kuwa kila anayebeba simu mfukoni atakuwa na shida ya kizazi."
Dkt.Allan Pacey kutoka chuo kikuu cha Sheffield anasema kuwa wazo hilo la kudidimia kwa shahawa na kuharibu "DNA"linatokana na "radio frequency" na mnunurisho wa kielectromagnetiki zinazopatikana kwenye simu na pengine joto aidha moja kwa moja kutoka kwenye simu au mnunurisho.
Dkt huyo anayefanya uchunguzi wa shahawa bado hajashawishika akisema ushahidi huo hauna msingi na ataendelea kuweka simu mfukoni.
Aliambia BBC,"kumekuwa na shauku kwa mda kama kuweka rununu mfukoni kunaweza changia kudidimia kwa ubora wa shahawa na nguvu za kiume kivyovyote.
"Kumekuwa na habari zisizokuwa na msingi lakini kwa maoni yangu uchunguzi uliofanywa hadi kufika sasa haujakuwa wa kutosha kwa sababu wachunguzi aidha hawakuhifadhi shahawa vile inavyofaa ama wamedadisi matumizi ya simu kati ya wanaume bila kuzingatia mambo mengine kama mitindo yao ya maisha.
"Tunayohitaji ni uchunguzi kufanywa ambapo utumizi wa simu unazingatiwa vile vile tabia zinazoathiri maisha yao.
Hadi pale tutakapo tafakari hayo,nitaendelea kuweka simu yangu katika mfuko wa mkono wa kulia wa suruale yangu!"

CHANZO: BBC


MUHADHARA MKUBWA LEO MAGHARIBI: UTAKUWA LIVE TV IMAAN NA RADIO IMAAN

Assalaam Alaykum warahmatullah wabarakatuh. .

Tangazo la Muhadhara.

Eneo: Masjid Haqq Morogoro.
Baada ya maghreb na kisha saa 9pm patakuwa na Kipindi maalum Cha Fatawa (maswali na majibu) Live Radio na Tv Imaan.

Mtoa Mada: Shekh Issa Almubali3 شيخ عيسى المبلع (kutoka Saudi Arabia).Ni mmoja katika wanafunzi wa mashekh wakubwa kama Ibn othaymeen, Ibn Baaz, Albaniy, Na Jibreen. (ALLAH AWAREHEM)

Tunaomba kila mmoja amwambie mwenzie.


SOMA MAGAZETI YA LEO TAREHE 16,JULY 2014



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU