Facebook Comments Box

Sunday, September 21, 2014

PICHA: ARSENAL YAMPIGA ASTON VILLA 3 BILA NA R.MADRID YASHINDA 8 KWA 2



'DANNY BOY' Welbeck leo amefunga bao lake la kwanza akiwa na klabu yake ya Arsenal wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 Ugenini dhidi ya Aston Villa.

Arsenal walipata mabao yao matatu ya haraka ndani ya sekunde 200, kwa mabao ya Mesut Ozil, Danny Welbeck na la tatu Aston Villa wakijifunga.
OZIL AKITUPIA LA PILI

BAO LA KUJIFUNGA LA ASTON VILA

JINSI BAO LA WELBECK LILIVYOTENGENEZWA

ARSENE WENGER AKIPIGA PICHA NA KATUNI WA ASTON VILLA

CHRISTIANO Ronaldo ni hatari bwana! amelidhihirisha hilo leo wakati akifunga Hatrick yake ya 23 tangu alipojiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 8-2 dhidi ya klabu ya Deportivo.

Mabao ya Madrid katika mchezo huo yalifungwa na Ronaldo  29', 41', 78', Rodriguez 36', Bale 66', 74', Hernandez 88', 90' huku yale ya Deportivo yakifungwa na Medunjanin 51', Verdú Nicolás 84' 









YANGA YAPIGWA 2 KWA 0 JAJA AKIKOSA PENATI


Unaukumbuka ule msemo wa Okwi mwisho Chalinze, mjini kila mtu JAJA! Basi leo hali imekua tofauti kwenye uwanja wa Manungu jijini Morogoro baada ya Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil Geilson Santos Santana 'JAJA'  kuonyesha kuwa makali yake mwisho ni kwenye nyasi za uwanja wa taifa jijini Dar es salaam tu, lakini akitoka hapo hamna kitu!

Wakiwa ni wenye matumaini makubwa Yanga waliosindikizwa na mashabiki lukuki walijikuta wakikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar inayonolewa na kocha Mecky Mexime.

Mabao ya Mtibwa katika mchezo huo uliokuwa wa kasi kwa dakika zote 90 yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mussa Hassan 'Mgosi' kwenye dakika ya 15 wakati msumari wa pili ukishindiliwa kimiani na Ali Ame kwenye dakika ya 83.

Katika mtanange huo pia ulishudia mshambuliaji pendwa katika kikosi cha Yanga Geilson Santos Jaja akikosa penati kwenye dakika ya 46 ya kipindi cha pili cha mchezo iliyopanguliwa na kipa wa Mtibwa Said Mohammed.

Yanga walionekana kuutawala mchezo huo kwa kipindi kirefu lakini Mtibwa walionekana kunufaika zaidi na mipira ya 'counter Attack' mashambulizi ya kushtukiza yaliowapa mabao yao mawili kwa njia nyepesi.

 KIKOSI CHA YANGA KILIWAKILISHWA NA

1. Deo Munish "Dida" - 30
2. Juma Abdul - 12
3. Oscar Joshua - 3
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Kelvin Yondani - 5
6. Mbuyu Twite - 6
7. Hassan Dilunga - 26
8. Haruna Niyonzima - 8
9. Geillson Santana "Jaja" - 9
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamis Kizza - 20

Subs:
1. Juma Kaseja - 13
2. Rajab Zahir - 4
3. Omega Seme - 14
4. Nizar Khalfani - 16
5. Saimon Msuva - 27
6. Hussein Javu - 21
7. Said Bahanuzi - 11

YANGA WAKIPASHA KABLA YA MCHEZO KUANZA


MASHABIKI WA YANGA WAKIFATILIA KWA MAKINI MCHEZO
YANGA WAKIPASHA


BASI LA MASHABIKI WA YANGA KUTOKA DAR-ES-SALAAM

YANGA WAKITOKA UWANJANI CHINI YA ULINZI MKALI


HABARI MCHANGANYIKO

Rais Nicholas Sarkozy atanganza nia tena ya kugombea Urais kwa kupitia upinzani lakini alama za nyakati inaonyesha nafasi yake ni finyu.

Raia wa Uskochi watangwana Makonde baada ya kugombea matokeo yaliyotolewa ya kula ya Ndiyo au Hapana.Bwana Salmand aendelea kusisitiza "for me a dream never die" moto wa kudai uhuru sasa umewaka rasmi.

Iran yakataa kushirikiana na Amerika katika kuwasambaratisha wapiganaji wa Isis kwani Amerika ni wasaliti.

Katibu mkuu Ombeni Sefue atangaza kuhusu kustafu kwake.asema anahitaji muda wa kupumzika ampongeza Mh.Rais asema elimu ya juu imepanuka sana asema chuo kikuu kipya cha Dodoma kimejengwa na serikali na kuleta tija.pamoja na Taasisi ya Nelson Mandela kule Arusha,chuo kikuu cha sayansi na Teknolojia cha Mbeya na chuo kikuu cha kilimo kinachopangwa kujengwa Butiama pamoja na kampasi mpya ya chuo kikuu cha Muhimbili kule Mlonganzila.

Mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za serikali(CAG).Ludovick Utoh amemaliza muda wake kisheria na kustafu kwa kutimiza miaka 65.

Libya yatangaza hali ya hatari dhidi ya wanamgambo wenye msimamo mkali,,hayo yamejitokeza huku bunge likikataa kuidhinisha baraza jipya la Mawaziri lililoteuliwa na Waziri mkuu Abdullah Al-Thinni.polisi walaaniwa kila kona ni juu ya ukikwaji wa haki za binadamu wanazofanya.

Askari wa zamani ashtakiwa kwa makosa 300,000 nchini Ujerumani bwana Oscar Groening aliyëkuwa katika kambi ya kifo ya Auschwitz mwaka 1994.Kesi hii inatukumbusha wajibu wa vijana kusomea fani ya FOLENSIC SCIENCE(Tizama channel ya discovery Investigation).

Kongamano la sayansi kufanyika Iringa.Chuo kikuu cha Iringa (IU) nóvemba 4 hadi 6 mwaka huu.

Utafiti unaonyesha watu takribani 500 hufariki kwa siku kutokana na matumizi ya tumbaku.

Hizo ni baadhi ya habari zilizopewa uzito. Tukutane wakati mwingine.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU