Facebook Comments Box

Saturday, September 13, 2014

AZAM YAPANIA KUSHINDA MECHI YA KESHO



NI MECHI MUHIMU! Kocha mkuu wa klabu ya
Azam Joseph Marius Omog ameutaja mchezo
wa kesho wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga
kuwa ni mchezo muhimu. Omog amesema ni
muhimu kwa timu yake kushinda mchezo wa
kesho ili kuimarisha Morali ya timu kabla ya
kuanza kwa ligi. Azam inacheza mchezo huu
kwa mwaka wa tatu mtawalia ambapo miaka
miwili ya nyuma ilikua inacheza kama makamu
bingwa na mara zote ilipoteza dhidi ya
mabingwa Simba na Yanga, kesho inacheza
kama bingwa kwahiyo Azam ina nafasi kubwa
kushinda kama historia itatenda haki lakini pia
kutokana na maandalizi na usajili uliofanyika.
Raia huyo wa Cameroun alisema amewapa
wachezaji wake kilakitu kitakachowawezesha
kushinda mchezo huo, Kwahyo kazi imebaki
kwao kushinda na kuleta furaha klabuni.


WENYE NYUMBA ZA KUPANGISHA KUANZA KULIPA KODI

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imesema ipo kwenye harakati za kuhakikisha wananchi wanalipa kodi kulingana na mfumo wa maisha yao.

Hayo yamesemwa na Meneja wa elimu ya Mlipa kodi kutoka kwenye mamlaka hiyo Diana Masala ambapo amesema kwa sasa TRA inafanya utafiti ili kufahamu ni jinsi gani ya kukusanya mapato kwa wananchi ambao wenye shughuli nyingi za kujiingizia kipato kikubwa kwa mwezi kupitia miradi midogo.

Amebainisha hayo katika semina iliyoandaliwa na walipa kodi pamoja na Mamlaka hiyo kuhusu ukusanywaji wa mapato na uendeshwaji wa ushuru wa forodha.

Ameeleza wapo wananchi wengi wenye nyumba zaidi ya moja na zenye wapangaji ikiwemo mifugo mbali mbali lakini ukiangalia kwa undani kwa mwezi zaidi ya kiasi cha shilingi 170,000/- zinakusanywa na wananchi hao, ambao baadae watatakiwa kulipa kodi.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU