Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo
wa mpira wa vikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia
yanayofanyika huko Korea Kusini baada ya kuagizwa kuvua hijab kabla ya
mechi yao dhidi ya timu ya Mongolia .
Wanawake hao walikataa kata
kata kuvua vazi hilo na wakajiondoa mashindanoni wakidai inakiuka
maagizo ya dina ya Kiislamu inayomtaka mwanamke kujistiri nywele zake
haswa akiwa faraghani.
Sheria za shirika la mchezo huo duniani
haziruhusu kuvaliwaj kwa vitambaa vya kichwani wakati wa mechi lakini
sasa wamekuwa wakijadili iwapo sheria hiyo itaondolewe.
Hata
hivyo ilipowadia wakati wa mechi yao dhidi ya Nepal sheria hiyo haikuwa
imebadilishwa na hivyo iliwabidi kuyaaga mashindano.
Fani nyengine za michezo katika mashindano hayo ya Bara Asia zinaruhusu uvaliwaji wa hijab.
Timu ya taifa ya unyanyuaji uzani ya Iran imekuwa ikishiriki mashindano hayo huku wakiwa wamevalia hijab.
Baraza la mashindano ya Olimpiki ya Bara asia OCA imesema kuwa haki za wachezaji ni zinapaswa kupewa kipaombele .
Baada ya kuyaaga mashindano hayo mchezaji wa Qatar Amal Mohamed A
Mohamed alisema kuwa walikuwa wamehakikishiwa kuwa wataruhusiwa
kushiriki mashindano hayo wakiwa wamevalia hijab na hivyo hawaelewi
kwanini sheria hiyo haijabadailishwa.
''nina hakika kuwa hatutashiriki mashindano yeyote ya Bara Asia hadi sheria hiyo ibadilishwe''
Mashindano
hayo hufanyika kila baada ya miaka 4 na huwaleta pamoja washiriki 9000
kutoka mataifa 45 yakishindana katika fani 36 ya michezo.
Mashindano hayo yatamalizika tarehe 4 Oktoba.
Chanzo: BBC