| ||||
|
||||
Israel has launched two Palestinians-only bus lines
in the occupied West Bank, a step an Israeli rights group described as
racist and which the Transport Ministry called an improvement in
service. The left-wing Haaretz daily reported that the ministry opened the lines on Monday, to be used by Palestinian labourers travelling between the West Bank and Israel, after Jewish settlers complained that Palestinians on mixed buses were a security risk. "Creating separate bus lines for Israeli Jews and Palestinians is a revolting plan," Jessica Montell, director of the B'Tselem rights group, said on Army Radio. "This is simply racism. Such a plan cannot be justified with claims of security needs or overcrowding." The Transport Ministry said the two new lines would "improve public transport services for Palestinian workers entering Israel" and replace pirate buses charging them "exorbitant prices". "The Ministry of Transport has not issued any instruction or prohibition that prevents Palestinian workers from travelling on public transport in Israel nor in Judea and Samaria," it said, referring to the West Bank. "Furthermore, the Ministry of Transport is not authorised to prevent any passenger from using public transport services." Concerns Rights groups, however, voiced concern that Israeli police at checkpoints in the West Bank would remove Palestinian passengers from regular bus lines and order them to use the new ones. Police spokesman Micky Rosenfeld said all Palestinians returning to the West Bank would be searched for stolen property, describing this as a routine Israeli precaution. He said he did not know whether and how this might affect Palestinian travel on regular buses. Herzl Ben-Zvi, mayor of the Karnei Shomron settlement, said the new lines "answer the needs of all passengers; Palestinians and settlers" because they would relieve overcrowding on buses in the area. Israel occupied the West Bank in the 1967 Middle East war and maintains a network of roadblocks in the territory, severely restricting movement of Palestinians in the area. Palestinians seek the West Bank, along with the Gaza Strip and East Jerusalem, for a future state, a claim supported by most world powers, which also view the settlements as illegal. |
Tuesday, March 5, 2013
ISRAEL LAUNCHES SEGREGATED BUS SERVICE
HALI ILIVYO DAR ES SALAAM LEO JIONI BAADA YA MVUA
Hapa ni maeneo ya kijitonyama wakati mvua ikiendelea kunyesha |
Mvua zikianza tu lazima mitaro izibe na maji yajae barabarani |
WAZANZIBAR HAWATOKUBALI KUKOSEKANA Z’BAR YENYE MAMLAKA KAMILI-MALIM SEIF
Chama cha wananchi CUF kupitia katibu mkuu wa chama hicho ambae pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kimemuhakikishia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania , Jaji Joseph Warioba, kwamba Wazanzibari kwa umoja wao hawatokubali chochote kile ambacho kitasababisha kukosekana kwa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mfumo mpya wa ushirikiano na Tanganyika kupitia Muungano.
Maalim Seif aliyasema hayo huko Makunduchi mkoa wa kusini Unguja
alipokuwa akizungumza na wananchi mbali mbali kwenye mkutano wa hadhara
wa chama hicho,amesema kutokana na matukio ya asilimia 66 ya maoni ya
wazanzibar kutaka mamlaka kamili ya nchi yao basi hakun haja ya
kutokuirjesha Zanzibar hadhi yake.
Kufuatia mkutano huo Maalim Seif amesema kuwa kwa sasa Zanzibar
haiwezi tena kukubali kukosa mamlaka yake ya kuwa na udhibiti wa mambo
ya nje na mahusiano ya kimataifa kwani imechoka na udhalilishaji
inaofanyiwa na Tanganyika kupitia Serikali ya Muungano.
Aidha Maalim ametolea mifano mbali mbali ambayo Serikali ya Muungano
imeilazimisha Zanzibar kujitoa katika Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC)
mwaka 1993 pamoja na hatua ya hujuma iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya
Nje, Benard Membe, ya wiki iliopita ya kufuta maeneo ya ushirikiano
yaliyohusu Zanzibar yaliyokuwa yawe sehemu ya makubaliano katika Mkataba
wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman.
Sambamba na hayo Maalim Seif alitaja athari ya Zanzibar kukosa nafasi
ya kufaidika na misaada ya kimataifa katika maeneo yote yasiyo ya
Muungano kwani Tanganyika hutumia jina la Tanzania kujichukulia nafasi
hiyo kwa manufaa na maslahi yake peke yake jambo ambalo limewatoa imani
wazanzibar waliowengi kuendelea na Muungano huu uliopo sasa.
Maalim amefahamisha wazi kuwa kwa sasa Zanzibar inataka kuwa na
Wizara na Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
haitokubali chochote chini ya hapo. Amesema kuwa “udhibiti wa mambo ya
nje ndiyo kigezo cha nchi kukubalika na kutambulika kimataifa na
Zanzibar inataka kurejesha mamlaka hayo na kurejesha kiti chake kwenye
Umoja wa Mataifa”.
WATAALAM WA MAMBO WANASEMA HUYU NDIO MCHUMBA WA JUSTIN BIEBER
Justin Bieber |
Ella-Paige. |
Kuna uwezekano mkubwa Justin Bieber alikuwa na sherehe mbaya ya kuzaliwa ijumaa iliyopita ila alipata mtu ambaye alifanya sherehe yake ya kuzaliwa iwe nzuri kidogo. Na huyo sio mwingine bali ni Ella Paige mrembo ambae anajihusisha na muziki nchini uingereza.
Mrembo huyo ana miaka 17 tu. Inasemekana walionana mara ya kwanza Los Angeles wakati binti huyo akirekodi kama mwenzi mmoja uliopita baada ya hapo wamekuwa wakionekana jijini London wakila raha na kuwa pamoja kwa muda mwingi
UHURU KENYATTA BADO ANAONGOZA
Kura zikihesabiwa kwenye kituo kilichopo Viwanja vya Kibera Social, jijini Nairobi baada ya wananchi wa Kenya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo jana. |
Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha kuwa
Uhuru Kenyatta, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta
anaongoza, huku akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi
hiyo, Raila Odinga.
Kama alivyo Uhuru, Raila pia ni mtoto wa mmoja wa
waasisi wa taifa la Kenya, ambaye alikuwa Makamu wa Mzee Kenyatta,
Jaramong Oginga Odinga.
Hadi majira haya ya saa 6.45 usiku wa kuamkia
leo, Uhuru ambaye ni mgombea wa TNA alikuwa amepata kura 744,648 sawa
na asilimia 56.1 wakati Raila ambaye ni mgombea wa ODM alikuwa akifuatia
kwa kupata kura 527, 780 sawa na asilimia 39.7.
Matokeo hayo ni kutoka katika vituo zaidi ya 5000
kati ya 31,000 na yalikuwa yakionyeshwa moja kwa moja na Tume Huru ya
Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kadri yalivyokuwa yanaingia.
Hata hivyo Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan
akizungumza na vyombo vya habari jana usiku alisema matokeo hayo ni ya
awali na kwamba matokeo kamili yangetangazwa na tume yake baada ya
kukusanya taarifa kutoka vituo vyote vya kupigia kura.
Wagombea wengine walikuwa wameachwa mbali. Hao ni
Musalia Mudavadi, Peter Kenneth, James Kiyiapi, Martha Karua, Mohamed
Dida na Paul Muite.
Waliokufa wafikia 22
Wapema watu 22 wakiwamo askari polisi tisa waliripotiwa kuuwawa baada ya kuvamiwa na kikundi cha watu zaidi ya 200 huko Mombasa na Kilifi saa chache kabla ya Wakenya kuanza kupiga kura jana.
Wapema watu 22 wakiwamo askari polisi tisa waliripotiwa kuuwawa baada ya kuvamiwa na kikundi cha watu zaidi ya 200 huko Mombasa na Kilifi saa chache kabla ya Wakenya kuanza kupiga kura jana.
Saa chache kabla ya uchaguzi huo, askari polisi
tisa waliuawa katika mashambulizi yaliyotokea kwenye miji ya Mombasa,
Kilifi na Kwale na kuacha wavamizi wapatao 10 na raia wa kawaida watatu
pia wakifariki.
Baada ya vifo hivyo, serikali ilipeleka vikosi vya
askari kutoka Mariakani Barracks kwenda kutuliza ghasia hizo wakati
kundi lingine la askari lilitoka Nyali Barracks kwa ajili ya kuweka
doria katika miji ya Mombasa na North Coast.
Taarifa zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa
kwenye mji wa Mombasa askari polisi wanne waliuawa na watu zaidi ya 100
waliovamia kituo cha kura cha Miritini.
Polisi pia ilithibitisha kuuawa kwa watu saba katika mapigano hayo huku na wengine kadhaa kutiwa nguvuni.
Wavamizi wengine waliuawa katika miji ya Kisauni
na Kilifi huku polisi wanne wakiuawa Chumani na mmoja huko Chonyi huku
watu watatu wakiuawa kwa kupigwa risasi.
Subscribe to:
Posts (Atom)