Facebook Comments Box

Thursday, September 20, 2012

MADEREVA WA BODABODA ARUSHA WAFANYA VURUGU

Picture
Dereva pikipiki ambaye hakujulikana mara moja jina lake akitaka kupasua kioo cha gari dogo baada ya dereva wa gari hilo kutaka kupita eneo walilozuia.
MADEREVA pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zaidi ya 300, jijini Arusha wameandamana na kufunga barabara kuu ya Moshi-Arusha kwa zaidi ya saa 3, katika eneo Ngulelo, wakilituhumu jeshi la polisi kumwachia mtuhumiwa wa mauaji anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwenzao bila hatia.

Madereva hao wakiwa na pikipiki zao, walifunga barabara hiyo kuanzia majira ya  saa 4  asubuhi hadi saa 6 mchana kwa mawe na magogo hali iliyolazimu jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto .

Kwa mujibu wa mmoja wa waendesha pikipiki, Jonathan Emanuel, Mkazi wa Ngulelo wilaya ya Arumeru, maandamano hayo yalilenga kulaani mauaji ya mwenzao aliyemtaja kwa jina la Hilari Elias (36) mkazi wa Oldadai, aliyeuawa kwa kupigwa risasi  Septemba 15 mwaka huu akiwa barabarani  eneo la Baraa akimsafirisha abiria aliyekuwa amemkodi.


Madereva hao wakiwa na mabango  yenye ujumbe mbalimbali  wa kulaani jeshi la polisi kumwachilia mtuhumiwa wa mauaji (jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa na uwezo wa kifedha na mmiliki wa garage ya kutengeneza magari  na mkazi wa Baraa, walilituhumu jeshi la polisi mkaoni hapa kwa kucheza mchezo mchafu wa kumwachulia mtuhumiwa aliyempiga risasi dereva mwenzao na kumsababishia kifo chake.

Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha basi eneo la Ngulelo majira ya saa 2 asubuhi kuelekea mjini katika chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru kuuchukua mwili wa merehemu na baadaye yalielekea nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo madereva hao kwa pamoja  walivunja lango la kuingilia na kuharibu mali za mtuhumiwa ikiwemo gari lake  lililovunjwa vioo vyote pamoja na vyoo vya nyumba hiyo.

Aidha baada ya tukio hilo madereva hao walifunga barabara katika eneo la Ngulelo kwa mawe na magogo wakishinikiza  mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kufika eneo hilo na kuwasikiliza kwani walikuwa hawana imani na jeshi la polisi huku wakidai ya kuwa mtuhumkiwa wao naonekana akirandaranda mitaani.

Katika eneo hilo pamoja na kufunga barabara hiyo,madereva hao  walivunja vioo vya magari kwa kupiga  mawe vioo vya magari na kuharibu baadhi ya magari yaliyokuwa yakijaribu kupita kwa nguvu wakati wamefunga barabara hiyo,huku wakipaza sauti kwa kupiga yowe wakiwa wamelala barabarani huku wakitaka mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo afike kuwasikiliza kilio chao kwani hawana imani na jeshi la polisi.

Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabasi na kueleza kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi hapo baadae,na mwili wa merehumu huyo umezikwa na umati mkubwa wa watu nyumbani kwap eneo la Oldadae.



Jaji Mkuu, Othman Chande aahirisha kesi ya rufaa ya Godbless Lema



 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande ameahirisha kesi ya rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, hadi Oktoba 2, 2012 kwa mujibu wa maombi ya mawakili wa pande zote mbili, CCM na CHADEMA walioandika barua ya kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo baada ya kifo cha mzazi  wao ambaye maziko yake yanatarajiwa kufanyika Septemba 22, 2012.

Jaji Mkuu ametoa amri fupi ya Mahakama kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa anajibu maombi wa pili aunganishwe kama mtu muhimu katika kesi hiyo.

Kesi hiyo ambayo imesikilizwa kwa takribani saa mbili chini ya Jaji Mkuu na Majaji wengine wawili wa Rufani, ni ya kukata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).

Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa, umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za CHADEMA ambapo Lema aliongea na wananchi waliokuwa wakimsindikiza na kuwasihi kuwaombea Majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki, “mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi,” alisema Lema.

Katika kesi hiyo, Lema anatetewa na Tundu Lissu, wakati kaka yake, Alute Mughwai, anawatetea walalamikaji.

Wakili Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dkt. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.

Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.

Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.

Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

*picha zimepatikana kwenye blogu ya "Libeneke la Kaskazini"

Picture
Umati wa wakazi wa Arusha waliofika eneo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa hiyo.
Picture
Wananchi wakiwa nje ya ofisi ya chama wanamsikiliza Lem


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU