Facebook Comments Box

Wednesday, April 24, 2013

ANGALIA MATOKEO YA DORTMUND NA REAL MADRID NA MAGOLI MANNE YA LEWANDOWSKI NA MOJA C. RONALDO YALIVYOKUWA

http://cdn.bleacherreport.net/images_root/article/media_slots/photos/000/827/539/ScreenShot2013-04-24at1.38.58PM_original.png?1366836014http://cdn.bleacherreport.net/images_root/article/media_slots/photos/000/827/543/ScreenShot2013-04-24at1.39.04PM_original.png?1366836024Save_originalOverheadgoal_originalScreenshot2013-04-24at1Goal4_originalhttp://cdn.bleacherreport.net/images_root/article/media_slots/photos/000/827/460/ScreenShot2013-04-24at1.00.50PM_original.png?1366833682Goal3_originalGoal2_originalNopenlaty_originalScreenshot2013-04-24at12Ornaldogoal_originalRonaldokick_originalScreenshot2013-04-24at11
Goal1view2_originalGoal1_original

MAMA HUYU WA KIINGEREZA AMESEMA WATANZANIA NI NGURUWE

Bibi. Sarah Hermitage ambaye ni Mwanasheria raia wa Uingereza, mwanaharakati wa kupambana na rushwa na pia mwekezaji katika shamba la Silverdale. Anapatikana @Chomachomp au http://thesilverdalecase.blogspot.com/
Bibi. Sarah Hermitage ambaye ni Mwanasheria raia wa Uingereza, mwanaharakati wa kupambana na rushwa na pia mwekezaji katika shamba la Silverdale.

Anapatikana @Chomachomp au http://thesilverdalecase.blogspot.com/
KATIKA hali inayoonyesha dharau kwa Watanzania na waumini wa Dini ya Kiislamu, Muingereza Sarah Hermitage, amefananisha Watanzania na nguruwe ambaye ni mnyama haramu kwa mujibu wa imani ya Kiislamu.
Sarah ambaye amekua akiwakashifu viongozi na wananchi wa Tanzania mara kwa mara alivuka mipaka na kufananisha Watanzania na nguruwe, baada ya kulalamikiwa kwa vitendo vyake vya kutoa maneno machafu kwa Watanzania katika mitandao ya kijamii.
Kauli hizo za Sarah amekua akizitoa kupitia mitandao ya twitter kupitia ukurasa wake wa https://twitter.com/Chomachomp kwa muda mrefu sasa bila kuchukuliwahatua zozote na viongozi wala watendaji wa serikali ya Tanzania.
Kauli ya Sarah kuita Watanzania ilianzia pale Mtanzania mmoja ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe Mbaraka Islam, kulalamikia kitendo chake cha kutukana viongozi na Watanzania wote kwa ujumla wao bila kuwa na hoja zinazowahusu.
Huku akijua aliyewasiliana naye ni Muislamu, Sarah aliandika katika ukurasa wake kwamba “anga la Tanzania limejaa nguruwe wanaopaa, Mbaraka Islam, ni kupe wa mwezi”, akimaanisha kwamba Mbaraka Islam ni mmoja wa nguruwe wengi wanaoelea katika anga la Tanzania.
“Kwa maana yoyote anayotaka kuuaminisha umma na katika mazingira ya Tanzania na Dini yetu, haiwezekani kwamba Sarah hakujua kwamba ni kashfa nzito ya Kidini kumfananisha Muislamu na nguruwe kwa namna yoyote ile. Alijua mimi ni Muislamu alifanya hivyo kusudi.
“Huyu mama (Sarah) amefanya hivyo baada ya kuona Watanzania wamelala na hakuna anayethubutu kumgusa hasa viongozi wetu anaowatukana anavyotaka bila kuguswa na yeyote,” alisema Islam na kuongeza kwamba amechukua hatua kadhaa ambazo hajapenda kuziweka hadharani kwa sasa.
Kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislamu, mnyama nguruwe ni haramu na najisi na kwamba haruhusiwi kuliwa na unapomgusa unapaswa kujitakasa kwa kuoga mara saba moja ikiwa ni kwa kutumia mchanga.
Sarah alikerwa na makala aliyoandika Islam katika gazeti la Raia Mwema, ambayo  ilielezea kukerwa na maneno machafu anayoyatoa kwa Watanzania.
Katika makala hiyo, Islam alisema:
KWA takriban miaka mitano sasa, raia mmoja wa Uingereza, Sarah Hermitage amekuwa akiendesha kampeni ya kumchafua Rais Jakaya Kikwete, Serikali ya Tanzania, taasisi muhimu za nchi yetu kama vile mahakama, waandishi wa habari na hata Watanzania ambao wamekua wakimpinga.
Pamoja na kuwa kumekua na mapungufu katika serikali yake na vyombo vyake kama ilivyo kwa serikali nyingine Duniani ikiwamo ya Uingereza, Muingereza huyu amekua akitoa kashfa kwa kila jambo linaloandikwa ama kujadiliwa kuhusiana na viongozi wa Tanzania na taasisi zake na kwa kutumia lugha isiyo na staha.
Watanzania siku zote wakiwamo wanasiasa, waandishi wa habari na wanaharakati, wamekua wakiikosoa na hata kuishambulia serikali na vyombo vyake inapokosea jambo ambalo ni jema na linasaidia kuimarisha utawala bora, lakini kwa staili anayotumia Muingereza huyu ni kupitiliza mipaka na zaidi ya yote ni udhalilishaji usioweza kuvumilika kwa mtu mwenye mapenzi mema na nchi yake.
Dhumuni la Sarah Hermitage na washirika wake wakiwemo baadhi ya Watanzania ni kuzishawishi nchi za Magharibi wakianzia na Uingereza kusitisha misaada na uwekezaji katika Tanzania. Hilo angeweza kulifanya huko kwao kwa kuwasiliana na serikali yake, lakini badala yake amekuwa akitumia mitandao ya kijamii na barua pepe tena kwa kutumia lugha ya kukashifu na kudhalilisha.
Watanzania wote tuna jukumu la kutetea heshima ya nchi yetu, lakini wapo wale ambao tumewapa jukumu la kusimama mstari wa mbele. Jambo la kusikitisha ni kwamba ni watu wachache sana kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambaye ambaye amekua na ujasiri wa kumkabili Muingereza huyu, kwa kumwambia wazi kwamba kama ni misaada ana haki ya kuishawishi nchi yake kuzuia misaada kwa Tanzania lakini si kwa kudhalilisha Watanzania.
Zitto alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba nchi nyingi tajiri duniani ikiwamo Uingereza, zimejengwa kwa kutumia rasilimali walizozipora katika nchi walizozitawala ikiwamo Tanzania na kwamba nchi hizo zinaweza pia kuendesha shughuli zake bila misaada ya dharau. Bahati mbaya sana watendaji wengine wengi ambao wanapaswa kutetea heshima yetu, hili suala limewapita, pengine kutokana na kutokua na taarifa sahihi ama kwa kutowajibika.
Jambo la kujiuliza, wale ambao miongoni mwa majukumu yao ya kila siku ni kutetea na kulinda hadhi na heshima ya nchi yetu wanafanya kazi gani? Sasa tunawalipa mishahara mikubwa na marupurupu ya nini kama hawawezi kututetea tunapodhalilishwa ama kutukanwa?
Hali hii inatufanya tukumbuke ujasiri wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara kadhaa aliwatunishia misuli viongozi wa mataifa makubwa walipotaka kuidhalilisha nchi yetu, sembuse raia mmoja ambaye amekua akitumia matatizo yake binafsi kutaka kuidhalilisha Tanzania na kutaka kuishinikiza serikali yake na nyingine kuichukia Tanzania.
Jinsi anavyotumia mtandao wa twitter kuchafua Tanzania
Sarah Hermitage amekua akitafuta katika taarifa za vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania vinavyoandika taarifa zozote kuhusu Tanzania na kuziongezea maneno ya kukashifu na kejeli.
Kwa mfano amekua amechukua taarifa inayomunukuu Raia Jakaya Kikwete akiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupambana na rushwa hadi ndani ya Baraza la Mawaaziri, na yeye kuongezea maneno akisema, “kundi moja la majambazi linaliambia kundi lingine la majambazi kukamata mwizi”.
Akachukua taarifa iliyochapishwa katika vyombo vya habari ikimnukuu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribisha wawekezaji katika kilimo na yeye kuongeza maneno akisema, “Mheshimiwa Pinda kitakachoendelea kukandamizi uwekezaji katika kilimo cha Tanzania ni uporaji wa ardhi ya wawekezaji katika mtindo wa Mugabe (Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe).”
Amekua akidiriki kukashifu hadi majaji wote wa Tanzania kwamba wana bei akisema, “sina hakika kama unaweza kupata jaji ambaye si mla rushwa. Wote wana bei,” kauli ambayo hata Watanzania wanakua wakiitoa kwa uangalifu maana hata kama kuna majaji ambao si waadilifu, haiwezekani wakawa ni wote, kama ilivyo katika taasisi nyingine.
Raia mmoja wa Kenya anayeishi Tanzania, aliyejitambulisha kwa jina la Marigi Patrick aliandika katika mtandao kwa kusema;
“Sisi Wakenya tuna matatizo yetu na tumekua na tofauti kubwa sana za wazi wazi, lakini anapotokea raia wa kigeni kumshambulia kiongozi wetu tena kama Rais wa nchi, tunaungana na kumshughulikia. Kuna wakati Wazungu walimshambulia Rais Mwai Kibaki, sote tukisaidiwa na wabunge wetu na vyombo vya habari tulimshambulia hadi akakoma kutudharau.”
Marigi ambaye anajihusisha na biashara ya bima, anasema Watanzania bado ni wachanga katika demokrasia, ama wanadharau kila kitu bila kujua madhara yake katika hadhi na heshima ya Taifa, na ndio maana wanashindwa kutofautisha kati ya demokrasia na udhalilishaji unaofanywa na raia wa nchi nyingine kama alivyo Sarah Hermitage.


VIDEO: ANGALIA MAGOLI YOTE YA BAYERN MUNICH DHIDI YA BARCELONA HAPA




MWENYEKITI WA UMOJA WA SACCOS TAIFA AUAWA KINYAMA

  Picture
Hapa ndipo gari ilipogonga na kupinduka wakati akikimbizwa na wauaji
Picture
Hapa ndipo alipouawa
Mwili wake umeharibiwa vibaya hivyo picha zake hazitawekwa hapa.
Mwili umepangwa kuzikwa mkoani Kilimanjaro leo, Jumatano.
Picture
Hapa ndipo alipochomwa moto

TAARIFA YA JESHI LA POLISI

MNAMO TAREHE 20.04.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITAGANO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. AMBROSE S/O LUKAS @ SHAYO, MIAKA 45,MCHAGA, MFANYAKAZI TAZARA – IYUNGA JIJINI MBEYA MKAZI WA IYUNGA. ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KWA KUTUMIA SILAHA ZA AINA MBALIMBALI NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA KISHA KUMCHOMA MOTO. AIDHA KATIKA TUKIO HILO WATU HAO WALIHARIBU GARI LA MAREHEMU T.750 AZD AINA YA TOYOTA HILUX RANGI NYEKUNDU KWA KULIBONDA MAWE KISHA KULITUPA KWENYE MTARO WA MAJI UMBALI WA KILOMITA MOJA  KUTOKA ENEO LA TUKIO.

  • CHANZO NI TUHUMA ZA KUTAKA KUIBA WATOTO KIJIJINI HAPO.MWILI  WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE IKIWA NI PAMOJA NA KUKATWA PANGA  KICHWANI NA MDOMONI NA MAJERAHA YA KUCHOMWA MOTO MIGUUNI NA KICHWANI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
  • KATIKA TUKIO HILO WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI.
  • HATA CHANZO SAHIHI CHA MAUAJI HAYO BADO KINACHUNGUZWA KUTOKANA NA KUPOKELEWA KWA TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA KWA RAIA WEMA KUWA MAREHEMU ATAKUWA ALIUAWA KWA SABABU ZINGINE TOFAUTI NA ILIVYODAIWA AWALI KWAMBA ALITAKA KUIBA WATOTO.
  • KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISIBARAKAEL MASAKI  ANAENDELEA KUTOA KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAFIKISHE MALALAMIKO/KERO ZAO KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WATU WALIOHUSIKA NA TIKIO HILO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


Signed By,
[BARAKAEL MASAKI  – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



HILI NDILO BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LA KENYA NA WASIFU WA MAKATIBU WAKE WATARAJIWA





 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU