Facebook Comments Box

Saturday, June 14, 2014

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 14 JUNE 2014



RAIS WA KENYA IPELEKA HARAMBEE STARS BRAZIL

Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta akitoa hotuba yake katika Ikulu ya Nairobi wakati wa hafla ya kuiaga timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars aliyoipa ofa ya kwenda ziara ya mafunzo kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil

Rais Kenyatta akiongea na wachezaji wa Harambee Stars



Rais Kenyatta akigawa tiketi kwa wachezaji huku akishuhudiwa na mkewe Margaret Kenyatta na Seneta wa Nairobi Mike Sonko (kushoto)


Rais Kenyatta, mkewe Mama Margaret Kenyatta na Seneta wa Nairobi Mike Sonko wakipozi Ikulu ya Nairobi na Harambee Stars wakati wa hafla hiyo fupi ya kukabidhi tiketi za ndege za kuendea Brazil kuona kombe la dunia

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa kuifadhili timu ya taifa ya soka Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la dunia 
Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil. 
Kitendo cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji wa timu ya taifa ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika baadaye mwakani.
Mmoja wa wachezaji hao alifurahi sana na kusema kuwa hatua ya Rais Kenyatta kwao imetimiza ndoto yao. Rais atagharamia tiketi za timu hiyo kutazama michuano, malazi na usafiri ingawa haijulikani ni mechi zipi watakazotazama. 
Hatua ya Rais Kenyatta imewashangaza watu wengi sana nchini Kenya kwa kuwa timu ya taifa ya Kenya haikuwahi kufuzu kushiriki michuano hiyo, sasa wengi wanahoji hatua yake itasaidia nini?
Soka ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba, usimamizi duni na wachezaji kukosa motisha ya kufanya vyema kwa ajili ya usimamizi huo mbaya. 
Kenyatta na mkewe mama wa kwanza wa taifa Margaret Kenyatta wamewafadhili vijana hao kwa kima cha dola elfu arobaini. 
Akitoa ufadhili huo Kenyatta amesema lengo lake hasa ni kuwapa matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.
Pia ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe la Cecafa. 
Kenyatta mwenyewe hatakwenda na kikosi hicho bali amewaasa vijana hao kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil. Ufadhili huu unakuja miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja miotano ijayo. 
Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 Julai.
CHANZO:BBC


NYUMBA YA BALOZI WA MSUMBIJI TANZANIA YAUNGUA

Habari zilizotufikia ni kwamba nyumba ya balozi wa Msumbiji iliyoko maeneno ya Masaki imewaka moto. Habari zinaendelea kutupasha kwamba fire walifika lakini maji yalikuwa kidogo.


UHOLANZI WAIPA UISPANIA KIPIGO CHA MBWA MWIZI.

Van persie akishangilia kwa kugonganisha mikono na kocha wake
Magoli mawili  yaliyofungwa na Van persie na mawili yaliyofungwa na roben na moja la vrij yaliyosha kabisa kuisambaratisha uhispania japo wao ndio walikuwa wakwanza kupata goli kwa njia ya penati.
Timu ya uhispania ndio ilitabiriwa na wengi kuonesha mpira mzuri na kuchukua kombe ila kwa jana wengi wanasema huu ndio mwisho wa utawala wake kisoka na wanaipa nafasi kubwa uholanzi.
 
Van persie akifunga goli kwa kichwa cha kuchumpa watu wanakifananisha na ndege kubwa za mizigo na watu ikiwa inaruka



BOMU LAUA MTU MMOJA KWENYE DAURA ZANZIBAR

Hii ni picha ya mtu anaesadikiwa kufa baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu kurushwa zanzibar.eneo la darajani kulikokuwa kunafanyika daura ya masheikh wa Afrika mashariki. Inasemekana huyu aliekufa ni mwanafunzi wa sheikh Quasim Mafuta Qaasim wa tanga na sheikh mwenyewe kaumia mkono na mguu kulikuwa na sheikh mwingine kutoka kenya ambae hakupata madhara yoyote. Tunamtakia apone mapema. Na marehemu Allah amuhifadhi.
Inna lilayh wa inna ilayhi rajiuun 


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU