Facebook Comments Box

Thursday, August 21, 2014

TANZANIA YAZINDUA MGODI WAKE WA KWANZA.

Waziri wa Nishati na Madini Mh Sospeter Muhongo
Serikali ya Tanzania imezindua rasmi mgodi wake wa kwanza wa madini utakaowaajiri wafanyakazi wazawa tu kuanzia ngazi za uongozi hadi chini.

Hatua hiyo imechukuliwa na serikali kama juhudi za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa watanzania.Aidha waziri wa nishati na madini nchini humo Sospeter Muhongo amesema mgodi huo wa dhahabu wa Biharamulo utafuatiwa na mingine kadhaa itakayotowa pia nafasi za ajira kwa wazawa ingawa amesisitiza Tanzania haina nia ya kuwafukuza wageni wanaosimamia migodi mingine ya nchi hiyo.

Kwa kipindi sasa watanzania wengi wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa ajira katika nafasi muhimu katika migodi ya hapa nchini. Watanzania wengine wakilalamikia migodi hiyo kutofaidisha nchi na kutowathamini wananchi wanao zunguka maeneo hayo na wengine wakilalamikia uharibifu wa mazingira wa migodi inayomilikiwa na wawekezaji.

Huwenda hii ikawa njia nzuri ya kuinua uchumi wa nchi pamoja na kukuza ajira kwa vijana wengi wa kitanzania walio maliza vyuo vikuu na kukosa ajira.


HUMAN RIGHT NA HIZB-UT-TAHRIR WAILALAMIKIA KENYA KWA KUUWA WAISLAM

Kwa mara nyengine kikosi cha kupambana na ugaidi kimekashifiwa na kulaumiwa vikali kwa kuhusika na matendo ya kikatili dhidi ya Waislamu. Likizindua taarifa yake siku ya Jumatatu tarehe 18/08/2014, shirika la utetezi la haki za binadamu limeshtumu kitengo hicho kwa kutekeleza mauaji,utekaji nyara pamoja na kuwapoteza washukiwa wa ugaidi. 
“Kikosi cha kupambana na ugaidi kinawauwa watu waso na hatia na kuwapoteza wengine tena mbele ya maafisa wakuu wa serikali, ofisi kubwa za kiubalozi na zile za umoja wa mataifa…” Akasema Bi Leslie Lefkow naibu mkurugenzi wa shirika hilo.

Kufuatia taarifa hii Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inaeleza yafuatayo:-

- Taarifa hizi sio ngeni kwani jamii ya Kiislamu na ya Kenya kwa ujumla. ATPU tokea ibuniwe mwaka 2003, imekuwa ikiyafanya maovu haya paruwanja pasina na kushikwa na hisia ya ubinadamu! Mfano wa uovu walioufanya mchana peupe ni kule kumtia mbaroni kijana Suleiman Swaleh Salim wa Majengo Mombasa akitoka swala ya ijumaa mapema mwezi huu. Hadi wa
leo familia yake haijui yuko wapi? Wanawake wamekuwa wajane,watoto kuwa mayatima na nyumba kubakia pasina barobaro! Na kila ATPU inapo ambiwa iogope Mungu na ikome kufanya mauaji haya hupandwa na mori wa kufanya zaidi
madhambi hayo.

- Mauaji haya ni moja wapo tu ya dhulma kubwa inayotendewa jamii ya Kiislamu ya Kenya. Na imekuwa si tu maafisa wa ATPU bali unyama huu umetapakaa hadi kwa vikosi vyengine vya polisi.
Kwa mfano katika mtaa wa Eastleigh Jijini Nairobi, polisi wa kikosi cha GSU walikuwa wakivamia majumba na kuwapiga Waislamu
wenye asli ya Kisomali na kwenda kuwalaza kwenye baridi kali uwanjani Kasarani. Dhulma hizi zilifanywa kwa kile kilichoitwa oparesheni ‘Usalama Watch’ mwezi Aprili mwaka huu.

- ATPU imetekeleza unyama huu ndani ya dhamana ya Marekani,taifa lenye historia mbovu ya mauaji ya Waislamu ,mfadhili mkubwa wa  vita hivi kote ulimwenguni. Mbali na Marekani kutoa mafunzo kwa vikosi mbali mbali  kwa madai ya kupambana na ugaidi, aidha hufadhili kifedha mataifa na taasisi zake za kiusalama ati kupambana ‘ugaidi’. Kwenye taarifa ilioandaliwa kwa ushirikiano wa mashirika mawili ya kutetea haki za binadamu,; Open Society Justice Initiative na Muslim For Human Rights (Muhuri) yalidokeza kuwa katika mwaka ulioanzishwa kikosi hiki cha ATPU kilipewa kitita cha $ 10 milioni kutoka Marekani. Na bila shaka hadi sasa kikosi hiki kinaendelea kupata ufadhili kutoka Marekani.

Mwisho tunawakumbusha Waislamu kuwa mateso haya dhidi ya Waislamu wa Kenya ni sehemu tu mateso yanaowakubwa Waislamu wote duniani. Kwa hakika lau tutaandika taarifa za mauaji ya Waislamu kwenye vita hivi basi tutachukua muda na kujaza vitabu vingi. Ni muhimu kuelewa kuwa vita hivi ni kampeni
ya kuzuia Uislamu usisimame kuongoza dunia huku Marekani aendelee na kukoloni dunia kimawazo na kivitendo. Cha msingi ni kuelewa kuwa Waislamu ndio walengwa katika vita hivi kwa kuwa wana mfumo safi ulio na uwezo kuongoza Ulimwengu na kung’oa mfumo wa kikoloni wa kibepari unaongozwa na Marekani. Hivyo ni muhimu kupaza sauti yetu kwa pamoja kila tunapokumbwa na madhila haya huku tukifanya kazi ya kuregesha mfumo wetu kuongoza maisha jumla ya wanadamu chini ya kiongozi Khalifa atakayezuia dhulma za wenye kudhulumu na kueneza haki kwa walimwengu wote.

KUMB: 20/1435AH    24 Shawwal, 1435 Hijri  20-08-2014

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir East Africa

Tel:  +254 720  597 841 +254 0789 574 608

E-mail: media@hizb-eastafrica.com
Official website of Hizb ut-Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Media office website of Hizb ut-Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.info


SITTA AZUNGUMZIA MWENENDO WA KAMATI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao leo kuhusu muhtasari wa kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo kilichokaa leo kutathmini kazi za kamati 12 za Bunge hilo lilipofikia pamoja kuridhia baadhi ya maependekezo ya kuongeza ibara na sura ndani Rasimu ya Katiba katika Kamati zao.



HUYU NDIO SEWA HAJI ALIEJENGA HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA HELA YAKE

Sewa Haji Paroo
Sewa Haji Paroo alijenga jengo la kutoa huduma za afya kwa watu mbalimbali. Picha na Charles Kayoka.

Wasomaji kadhaa walitaka kujua zaidi kuhusu Sewa Haji Paroo anayetambulika kama mtu wa kwanza aliyejitolea kuanzisha huduma za afya na elimu kwa faida ya watu wote bila kujali rangi,
daraja la kiuchumi wala dini ya mtu yoyote.

Ikumbukwe kwamba Bagamoyo kabla ya 1900 ulikuwa mji maarufu sana na makao makuu ya kwanza ya Serikali ya kikoloni yalikuwa katika mji huo chini ya Deutch Ost Africa. Watu wengi wakiwamo wazazi wa Sewa Haji walifika Bagamoyo kutoka pande mbalimbali za dunia kutafuta maisha.

Sewa Haji Paroo anatajwa na Henry Morton Stanley mpelelezi na mwandishi wa habari kutoka Marekani mwenye asili ya Uingereza kama Soor Hadji Paloo katika kitabu chake kuhusu safari ya Kumtafuta Dk David Livingstone.

Stanley alifika Bagamoyo akitokea Unguja Machi 1871 akiwa njiani kwenda Ujiji kumtafuta Livingstone na alielekezwa kumwona Soor Hadji (Sewa Haji) kwa ajili ya msaada wa kumtafutia wapagazi wa kumbebea mizigo hadi Ujiji; kumtafutia nguo, majora, vitenge na kaniki na sari na khaki tetroni.

Pia alikusanya shanga za aina mbalimbali ambazo zilikuwa zikitumika kama malipo kwa ajili ya kununulia mbuzi, mtama na vyakula vingine kwa ajili ya kuwalisha wapagazi. 

Soor Hadji, alitambulika pia kama mchuuzi mashuhuri wa biashara ya silaha ambazo alikuwa akiziagiza kutoka India. Wakati alipokutana na Stanley alikuwa na miaka 20 tu, alizaliwa 1851.

Wakati huo wamisionari na wapelelezi kama kina Livingstone, Burton, Speke na Stanley walikuwa wakihitaji bunduki kwa ajili ya ulinzi na kuwindia wanyama.

Stanley anamweleza Soor Haji kama
kijana mwenye unyenyekevu sana wa dini, lakini katika biashara alikuwa mwerevu sana na mwenye akili iliyokuwa ikifikiri kwa kasi sana.
Anamlaumu kuwa, katika kufanya biashara alikuwa mjanja kwa kupata zaidi ya Dola 1,300 za Marekani kutoka kwa Stanley peke yake. Soor Haji alinunua majengo Bagamoyo na Dar es Salaam na huko Mombasa kwa ajili ya kutumika kwa watu maskini.

Chanzo:Mwananchi
===================

Sewa Haji, soma historia ya mtu alietukuka. Ndie alietajwa katika moja ya wodi ama majengo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili...

Hospitali ya Muhimbili ndie alieijenga kabla ya Waingereza kuichukua na kuiendeleza.

SEWA HAJI PAROO, ALITOA MCHANGO MUHIMU KATIKA MAENDELEO YA AFRIKA.

Ingawa alikuwa mfanyabiashara marufu na tajiri sana, Bw. Sewa Haji Paroo anatajwa alikuwa mcha Mungu na alijulikana zaidi kwa kusaidia wasio na uwezo na wagonjwa, ambapo alisaidia Wahindi, Waarabu na Waswahili bili kuchagua wala kubagua kwa Dini au Rangi zao.

Ndie alietajwa katika moja ya wodi za Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam, ambapo kuna wodi ama jingo linaloitwa Sewa Haji. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuthamini na kutambua mchango wake kwa Jamii ikaamua kuipa moja ya wodi za Hospitali hiyo ya Taifa jina la Sewa Haji kwa heshima yake.

Sewa Haji Paroo alifariki dunia mnamo mwezi wa February mwaka 1897 akiwa na umri wa miaka 46 na kuacha Simanzi kubwa na huzuni isiyomithilika kwa Wakazi wenzie wa Bagamoyo hasa Wanyonge, Wagonjwa na Wahitaji ambao aliwasaidia sana.

DUKAWALLA.

Historia ya Afrika ina mengi sana, moja kati ya Maandiko ya Historia ya Afrika juu ya Usuli wa ujio wa Jamii ya Waasia wengi katika Afrika Mashariki yameitaja sana Zanzibar na Bagamoyo. Maandiko hayo yameainisha kuwa watu wengi wa Jamii hiyo walikuja Afrika Mashariki kwa Sababu ya Kufanyabiashara na walitambulika zaidi kama "DUKAWALLAS" (MADUKAWALLA), Ukoo wa kina Sewa Haji Paroo ni sehemu ya Maandiko hayo.

Haji Paroo Pradhan alihama kutoka Bhuj, Kutchh mpaka Zanzibar akiwa pamoja na kaka yake Jaffer Paroo Pradhan, hawa wanatajwa kuwa miongoni mwa Madukawalla wa awali kabisa.

Mwaka 1852 walianzisha Duka dogo la Bidhaa mbalimbali ambapo mpaka Mwaka 1860 biashara yao ilikuwa imekuwa zaidi na hivyo kuamua kuanzisha Tawi Mjini Bagamoyo.
Mmoja kati ya Watoto wanne wa Bwana Haji Paroo Pradhan alikuwa ni bwana Sewa Haji Paroo, ambaye alizaliwa mwaka 1851 ikiwa ni mwaka mmoja tu tokea wazazi wake wahamie Zanzibar. Sewa alilelewa katika makuzi ya Kidini na kufunzwa biashara na baba yake katika umri mdogo tu.

Mwaka 1869 Mzee Haji Paroo alipata msiba mzito sana wa kuwapoteza vijana wake wawili kati ya wanne aliobarikiwa kupata, hivyo basi kumtaka Sewa Haji Paroo kuchukua nafasi ya kaka zake
katika usimamizi wa biashara za Familia ambazo zilikuwa chini ya Kampuni iitwayo Haji Kanji & Co.

MISAFARA YA WAPAGAZI NA KILELE CHA MAFANIKIO.

Mwaka 1870 mara baada ya kijana mdogo Sewa haji Paroo kukabidhiwa Mamlaka ya uendeshaji wa biashara za Familia yao alifanya mabadiliko mengi ya kimsingi ambayo yaliiongezea mapato
mno kampuni yao. Akiwa na umri wa miaka 18 tu Sewa Haji Paroo alivivuka vizingiti vyote na kufuta dhana ya umri katika utafutaji kwa kuifikisha biashara yao katika kilele ambacho hata baba yake hakuota kukifikia.

Msingi Mkuu wa mafanikio ya Biashara yao ni ubunifu wake wa kutumia misafara ya Wapagazi katika kueneza bidhaa zake na kusaka bidhaa mpya, misafara hiyo aliieneza nchini kote ikipita Unyanyembe, Mwanza mpaka Ujiji. Kwa kuwa Makao yake yalikuwa Bagamoyo alieneza misafara ya Wapagazi mpaka Zanzibar ambako ndiko yalipokuwa Makao yao ya mwanzoni.

Mwanzoni Wafanyabiashara wengi wa Kizungu waliipinga dhana yake ya kueneza biashara kwa kutumia Misafara ya Wapagazi lakini mara baada ya kuliteka soko lote la Biashara kwa Misafara yake watu wengi walianza kumuiga na kuikubali mbinu yake hiyo.

Sewa alijishughulisha zaidi na Uuuzaji wa Nguo, Vitambaa, Vitanda, Sufuria za Bati na Chuma huku naye akinunua bidhaa kama Pembe za Ndovu na meno ya Tembo kwa ajili ya kuuza kwa Wazungu. Pia Sewa Haji alipata kibali cha kufanya Biashara ya Silaha ambapo kwa eneo hili alikuwa ndiye mfanyabiashara mkubwa sana wa Silaha.

Mafanikio yake kwenye Biashara yalimzalishia Faida kubwa sana
ambayo iliongeza Maradufu utajiri wa Familia yao.

MSAADA KWA WAHITAJI.

Waneni hunena kuwa Mali na utajiri mwingu humbadili mtu na kumfanya awe na kiburi, ajinate na kujiona tabu. Ajabu kwa Bwana Sewa Haji Paroo ni kuwa Mali na Utajiri mwingi ambao alibarikiwa na Mungu ulimfanya awe karibu zaidi na watu na wala haukumpa Kiburi na Majinaki.
Mafungamano na Ubaramaki wake na Wapagazi viliwashangaza wengi katika wakati ule, haikuwa Mazoea kuonekana Matajiri wakila au hata kujichanganya na Masikini namna ile. Sewa Haji alipituka mipaka kwa kufikia hatua ya kununua Eneo na kujenga Makazi Maalum kwa ajili ya Wapagazi ili kuwapunguzia adha ya Makazi waliyokuwa nayo.

Kwa Bwana Sewa Haji Rangi au Dini ya Mtu haikuwa na Thamani zaidi kuliko Utu wake, alijenga Makazi Maalum kwa ajili ya Makazi ya Wakoma na pia Akanunua Baadhi ya Majengo kwa ajili ya kuanzisha Hospitali ambayo aliikabidhi kwa Kanisa La Bagamoyo na akaainisha katika Wosia wake Theluthi moja ya Mali zake itumike kusaidia Gharama za Uendeshaji wa Hospitali hiyo.

Katika Mji wa Mzizima (sasa Dar es salaam) bwana Sewa Haji Paroo alijenga Hospitali ambayo ilijulikana kama Sewa Haji Hospital, Hospitali ambayo Wakoloni wa Kiingereza waliibadili Jina na kuiita Princess Margaret Hospital kabla ya kubadilishwa jina na kuwa Muhumbili mwaka 1961 baada ya Uhuru wa Tanganyika.

SKULI YA SEWAHAJI/ SKULI YA MWAMBAO - SHULE YA KWANZA ISIYO YA KIBAGUZI.

Sewa Haji alitambua na kuthamini sana Elimu, lakini pia alikera mno na namna hiyo elimu ilivyotolewa kibaguzi na kutumika kujenga Matabaka katika Jamii. Hivyo basi Mwaka 1892 alinunua Jengo la Ghorofa kadhaa na kuligeuza kuwa Shule ya Kwanza ya Mchanganyiko ambayo haikujali Dini, Rangi, Kabila au jinsia ya Mwanafunzi, Yeyote aliyekuwa Tayari kujifunza alikuwa huru tu kwenda kusoma.

Shule hiyo ambayo ilijulikana kama Skuli ya Sewa Haji au Skuli ya Mwambao ilifanya kazi kwa muda wa miaka mitatu chini ya ufadhili wake ambapo mwaka 1895 Serikali ilichukua rasmi na kuigeuza Shule ya Serikali ambapo yeye aliajiri Mkurugenzi mpaya wa Shule na pia kufadhili utafiti wa uanzishaji wa Mtaala Bora zaidi wa kusomea.

MCHAMUNGU SEWA HAJI, DINI NI KIUNGANISHI.

Sewa Haji alikuwa mchamungu na mtu aliyependa sana dini, alitumia sehemu kubwa ya mali yake katika kuendeleza Nyumba za Ibada bila kuleta Ubaguzi wowote wa Kidini, Sera yake kuu ilikuwa ni Upendo kwa kila mmoja.

Kiongozi wa Jumuia ya Waislam wa Madhehebu ya Ismailia ambayo ndipo Bwana Sewa Haji Paroo ndo alitokea, Mawlana Sultan Muhammad Shah alimpachika bwana Sewa Haji Cheo Kikuu cha Alijah kwa kuchamini mchango wake kwenye Jumuiya Hiyo.

Majengo ya Jumuiya Hiyo yalioko Mombasa yalijengwa naye kama sadaka kwa Jamii yake.
Sewa Haji hakujali Dini ya Mtu katika kutoa misaada yake, kwa Bagamoyo alijulikana sana kama Mfadhili Mkuu wa Kanisa Katoliki na mara baada ya kifo chake Gazeti la Kanisa lilimuita "Mja Mwema wa Kipekee". Wamishenari wa Bagamoyo walizoea kumuita Sewa Haji "Rafiki yetu Mtukuka" na Kuonyesha namna Kanisa lilivyoguswa na Kifo chake siku nane tu baada ya kifo hicho kilibandikwa kibao chenye Picha yake katika lango la kuingilia Kanisani ambacho kilisomeka “This devoted friend of the mission will not forget (us) in his last wishes.” Utu, Kujali na Upendo wake huu kwa watu na Jamii iliyomzunguka vinaonyesha na kutoa taswira namna Bwana Sewa Haji Paroo alivyokuwa kiumbe wa namna yake, Jamii ya sasa inapaswa kuiga mema yake haya.


MAGAZETI YA LEO: ALHAMISI 21/08/2014








HII NDIO RATIBA YOTE YA LIGI KUU YA VODACOM 2014/2015

Hatimaye TFF wametoa ratiba ya mechi zote za ligi kuu ya vodacom.



JUSA NA MAALIM SEIF WAMTANGAZA MANSOUR SHUJAA

Mansour
Na mwandishi wetu Unguja :

Wiki  moja  kabla  ya  kupewa  dhamana  Mh. Mansour  Yusuph  Himid  katika  mkutano  wa  Chama cha wananchi  Cuf  uliofanyika  kwenye  viwanja  vya  Demkokrasia  Kibanda maiti  mjini  Unguja  alitangazwa  kuwa  ni  shujaa  tena  kidume haswaa, hayo  yalisemwa na Mh.Ismail  Jussa  Ladhu  pale aliposimama  na kuzungumzia  kwa  ufupi  juu  ya  kukamatwa kwa  waziri  huyo  wa  zamani wa serikali  ya  Smz, mh.Jussa  alisema kuwa  walipokuwa  wamempelekea  chai  ya  asubuhi  bw. Mansour  aliwaambia  wasimletee  tena  chai  kwa  kuwa atakunywa  tu  uji  wa kule  gerezani na kuwa  uji  ule wa  gerezani  ni mtamu sana  huku  akimalizia  kwa  kumwita  ni shujaa  tena  kidume hasa.

Maalim  Seif  yeye  kwa  upande  wake  akimzungumzia  mh.  Alisema  kuwa  Mansour  Yusuph  Himid  wote  tunajua  kuwa  ni  raia  wa  Zanzibar  kazaliwa  Zanzibar  na  baba  yake  ni miongoni  mwa  wanamapinduzi, waliokuwa hawamjui  wajue  hivyo, ametoka  katika   mifupa ya wanamapinduzi, kapatwa na mtihani kakamatwa na sasa  hivi  yuko  jela, Na mh. Jussa  amewaambia  kuwa  kwenda  jela  ni  ishara  nzuri, niwaulizeni  nabii  Yusuph  hakwenda  jela?  Sasa  ikiwa  mitume  walikwenda  jela  itakuwaje  sisi? Yanayo  mkuta  Mansour  leo  hii  wanampitisha  kwenye  njia  zile  zile  walizompitisha  Maalim  seif, Maalim  Seif  kwanza  alifukuzwa  Chama, kama  vile  haitoshi  wakamtafutia  shitaka  halina  dhamana  wakamuweka  jela kwa muda  waliotaka  wenyewe  ulipofika  muda  wakaniambia  toka, lakini  wakaniambia unatoka  lakini  huna  ruhusa  ya  kuzungumza  kwenye  mikutano  ya  hadhara  nikaitikia  Inshaallah, tumeanzisha  Cuf  mkutano  wa kwanza  tumeufanya  malindi  pale  mimi  nipo  kama  makamu  mwenyekiti  lakini  ndiyo  nilifungwa   mdomo  nilikuja  kwenye  jukwaa  pale  nyote  mnakumbuka  nikatoa  mkono  tu  wakaenda  wenyewe  mpaka  wakaamua  basi  sasa  kesi  tunaifuta  na  maalim  Seif  Yule  Yule  sasa  ni  makamu  wa  rais  wa  Zanzibar.

Nakumbuka  wakati  ule  napelekwa  jela  askari   walikuwa  wananitukana  na  kuninyanyasa  mie  kimyaa   kabisa  lakini  mungu  si  Athumani  wala  si  Msaki  mmoja  wao yupo  Dar  es  salam  pale  akiniona  sasa  hivi  anapiga  saluti, kwa hivyo  nasema  na  Mansour  ni  ishara  njema  na  hatujui  mwenyezimungu  huko  mbele  kamuandikia  nini ,lakini  najua  kamuandikia  mambo  mema  Inshaallah, lakini  papo  hapo  niseme  nataka  niamini  kwamba  Mansour  hakukamatwa  kwa sababu  yeye  si  mwanachama  tena  wa  chama  cha  mapinduzi, nataka  niamini  kwamba  Mansour  kakamatwa  kwa  sababu  ametoka  hadharani  na kuunga  mkono  mamlaka  kamili  kwa Zanzibar, nataka  niamini  kwamba  Mansour  hakukamatwa  kwa sababu  kasema  wazi  wazi  kwamba  atamuunga  mkono  maalim  Seif  mwakani  kwenye  uchaguzi, nataka  niamini  kwamba  Mansour  hakukamatwa  kwa  sababu  kasema  atagombea  jimbo  la Kiembe  samaki  kwa  tiketi  Cuf, Nataka  niamini kuwa  hizo  siyo  sababu  hizo  siyo  sababu  zilizofanywa  Mansour  akamatwe, Nataka  niamini  kwamba  Mansour  atatendewa  haki  kama  raia  yoyote  mwingine  katika  nchi  hii  na kwamba  yale  mashitaka  yote  yanayomkabili  basi  sheria  itachukua  mkondo   wake  pasiwepo  na  shinikizo  za  kisiasa,akitoa  mfano  kwenye  kesi  Maalim  seif  alisema  yeye  siku  moja  ya  kesi  hakimu  anayehusika  alikuwa  anakutana  watu  kwenye  ofisi  ya  waziri  kiongozi  halafu  wanaamua  kesho  tukafanye  kwa maalim  Seif, sasa  nataka  niamini  hayo  hayatatendeka   kwa  Mansour kwamba  mahakama  iliyo  huru  itaweza  kabisa  kusikiliza  shitaka  lilipo  mbele  yake  kwa  mujibu  wa  sheria  za  Zanzibar, kwa  sababu  sasa  hivi  siyo  tena  mwaka  64, wala  sasa  hivi  siyo  tena  mwaka  74  wala  siyo  tena  84  sasa  hivi  viongozi  wote  tunapiga  kelele  tunataka  utawala  wa  sheria.
Tumeambiwa  kabla  ya  kufa  huajaumbika  huyu  mh. Mansour  si alikuwa  Waziri  huyu  na walikuwa  wakimpigia  saluti  huyu si mwenzao? Sasa  kama  watu  wapo  walikula  njama  basi  wajue  mwenyezimungu  anahukumu  hapa  hapa  duniani  Akhera  inakwenda  hesabu tu, kwa  hivyo  yaliyomfika  Mansour  yanaweza  kumfika  mtu  yeyote sasa  kama  kuna  watu  kweli  wamekula  njama   Mnsour   akae  ndani  basi  wajue  kuwa  wakati  mwingine  ukilitandika  godoro  uliloweka  miba ili mwenzako  aje  alale  basi  ipo  siku  utakuja kulilalia wewe alimalizia  maalim  Seif.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU