Facebook Comments Box

Monday, July 21, 2014

VYOMBO VYA HABARI VINAICHUKIA ARSENAL?

Na: HASSAN KABANGE
Kinacho shangaza ni jinsi vyombo vya habari na wapinzani wetu wanavyo ogopeshwa na kushitushwa na uwezo wa ghafla wa Arsenal wa kipato ulioweza kuwavutia wachezaji mahiri duniani. Wanazidi kuchanganyikiwa wanapoona tunaweza kusajili mchezaji yoyote mahiri ambae Prof. Wenger atamtaka.
Mwanzo wa wiki hii Micheal Owen ametabiri Arsenal hawataingia nne bora hata kama wamesajili wachezaji wazuri. Hii sio mara ya kwanza kwa mkongwe huyo kutoa haya maneno ni kila mwaka anasema hivyo na Arsenal wanamdhirishia kuwa ni mtabiri muongo. Sina hofu na msimu huu itakuwa hivyo hivyo.
Mr. Rodgers yeye ameanza kitu ambacho watoto wa mjini wanaita "beef" kwa kusema kuwa Sanchez hakutaka kuishi jiji la Liverpool ndio maana hakujiunga na timu yao. Hapo yeye anazungumzia mazingira ya kijiografia hayo ndio yaliyomfanya Sanchez asiende kwao. Hili linakubalika ila sio sababu kuu kama ambavyo Mr Rodgers anataka kutuaminisha. Timu ya Arsenal inaonekana kukamilika na kujitosheleza katika kila idara, Sanchez atakuwa aliangalia viungo waliopo Arsenal na Liverpool kwa uhakika kabisa hauwezi kulingana viungo wa Arsenal wanawazidi wa Liverpool sana. Kila mshambuliaji ni ndoto yake kucheza mbele ya viungo hawa hebu fikiria mshambuliaji ucheze mbele ya viungo kama  Ramsey, Ozil na Carzola.
Kingine Barcelona na Arsenal ni timu ambazo zina shabihiana kwenye aina ya uchezaji na vilevile ni timu ambazo zina viwanja vizuri na vikubwa ni timu zenye washabiki wengi na mwisho ni timu zenye vifaa vya kutosha kwa ajili ya mazoezi.
Kingine ambacho Mr Rodgers anashindwa kukielewa ni kuwa Fabregas atakuwa alikuwa akimzungumzia Prof. Wenger pale Barcelona na hilo ndilo lililomfanya Sanchez achague kuja Arsenal. Kitu pekee ambacho kitawafanya Liverpool kutushinda katika pirika za kugombea mchezaji ni Prof Wenger kuendelea kufananisha kipaji, umri na mshahara.
Kuna mtu anajiita “Special One” yeye mwenyewe juzi juzi aliuchekesha umma baada ya kusema Fabregas hakutaka kujiunga tena na Arsenal na kusema ilimchukua dakika 20 kumshawishi ajiunge Chelsea (Sijui huyu "special one" alikuwa amevuta nini). Maana huu ni uongo ulio tukuka! Bado akaendelea kwa kusema Wilshere ni mfano mbaya kwa vijana baada ya kuripotiwa akiwa anavuta sigara hadharani. Hapa ndio utaona huyu ni "special one" wa ujinga na ujinga huu anao peke yake, huwa anatumia lugha zisizo na staha mbele ya waandishi wa habari ikitokea kakosana na mtu. Ni yeye alie mtetea John Terry kwa kulala na mke wa mchezaji mwenzake ni huyo huyo alie mtetea Hazard kwa kumpiga mtoto mateke ana orodha kubwa ya mambo ya ajabu anayo yafanya ila hayaoni na tukifananisha na hili kosa la Wilshere ambalo ni moja. Japo Wilshere aliahidi mbele ya umma kuwa hatavuta na akarudia tena lakini asihukumiwe kama ameua.
Kuna wakati nashangaa watu wanao isema Arsenal na Prof. Wenger, Liverpool haijashinda kombe lolote kwa muda mrefu vyombo vyote vya habari vimefumbia macho hili. Lakini wakati Arsenal tukiwa hatuna kombe kila mechi watangazaji na vyombo vya habari vilikuwa vikirudia hili.Sasa Arsenal tumepata kikombe je, vyombo vya habari vitakuja na mada gani juu ya Arsenal?
Arsenal ni klabu kubwa na nzuri, Hatupo makini "perfect" lakini angalau tunafanya vitu katika umakini unao hitajika bila kuangalia vilabu vingine vinafanyaje na hilo ndilo lililotufanya tuingie kwenye mtafaruku na vyombo vya habari. Walitakiwa watupongeze lakini tumekuwa tukilaumiwa.
Najivunia kuwa mshabiki wa Arsenal na filosofa ya klabu. Kuna wakati klabu inaniumiza lakini angalau hizi "video game" imenifundisha jinsi ya kukaa nao vizuri maadui.
Na sasa napenda kuwaambia maadui kuwa sasa ndio tupo katika mstari na huu ni wakati wetu.
COYG!!!!!


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU