Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya kiislamu nchini, Sheik Ponda amerudishwa tena maabusu baada ya kunyimwa dhamanulinzia ya kesi yake iliyokuya ikisikilizwa leo katika mahakama ya Hakimu mkazi mfawidhi mkoani Morogoro. Kesi iyo imehairishwa hadi tarehe 1/10/2013
Tuesday, September 17, 2013
MAMLAKA YA MAWASILIANO (TCRA) YAENDESHA WARSHA YA SIKU MBILI KWA WANA BLOG
WATUHUMIWA WA MAUWAJI YA MFANYABIASHARA WA ARUSHA ERASTO MSUYA WAKAMATWA SIKONGE TABORA WAKIFANYA ZINDIKO WASIKAMATWE
Jeshi la polisi mkoa wa kilimanjaro linawashikilia watu wanne zaidi wakidaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara bilionea wa madini ya tanzanite Arusha Erasto Msuya 43 wawili kati yao walikutwa kwa mganga wa kienyeji (sangoma) wakifanyiwa zindiko ili wasikamatwe na vyombo vya dola.
Pia jeshi limenikiwa kunasa bunduki aina ya SMG yenye namba za usajili KJ10520,inayoaminika kutumika katika mauaji hayo.Msuya aliuawa kwa kupingwa risasi zaidi ya 10 kifuani Augost 7mwaka huu,katika eneo la mijohoroni wilayani Hai.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Robert Boaz aliwataja watuhumiwa kuwa ni Sadiki Jabiri 32 mkazi wa Dar es Salaam na Lang'angata wilayani Hai
.Karimu Kihundwa 33 mkazi wa Lawate Wilayni Siha ambao wanatajwa kuwa ni muhimu katika mauji hayo.Alisema watuhumiwa hao wawili walikamatwa eneo la Kaliua sikonge mkoani Tabora wakiwa kwa sangoma wakifanyiwa zindiko ili wasitiwe mbaroni.
Baada ya kuhojiwa na polisi walieleza jinsi walivyoshiriki mauaji hayo na mahali walipoficha silaha hiyo na pikipiki zilizotumika katika tukio hilo.
Boaz aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Jalila saidi 28 mkazi wa Mkoani Manyara na Kondoa Mkoani Dodoma na Joseph Damas Mwakipesile maarufu kama "Chusa"(35) ambae pia ni mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite anayeishi Arusha .
Alisema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata pikipiki nyingine inayodaiwa kutumika katika tukio hilo yenye uasjili T751 aina ya Kinglion rangi nyeusi ambayo wakati wa tukio ilikuwa ikutumia namba za bandia.
Kamanda Boaz alisema bunduki iliyokamatwa ilikutwa ikiwa imefichwa kwenye tindiga katika eneo la Baroi kwenye mpaka wa wilaya ya Hai na Siha.
Kukamwatwa kwa watuhumiwa hao wanne sasa kunabadilisha sura ya kesi hiyo ambapo awali walifikishwa mahakani watuhumiwa watatu Sharifu Athumani (31),Shaibu Saidi maarufu kama mredi (38) na Mussa Mangu (30) Kesi huyo namba 6 ya mwaka2013,imepangwa kesho tehehe 18,09,2013 kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
CHANZO:TANZANIA DAIMA
WAMALAWI WAFURIKA OFISI ZA UHAMIAJI DAR KWA AJILI YA KUJIORODHESHA KUPATA UHALALI WA KUISHI TANZANIA
Raia wa Malawi wakiwa katika foleni ya kuingia kujiandikisha katika Idara ya Uhamiaji, Mkoa wa Dar es Salaam jana kuhusu zoezi linaloendelea la kuwatambua wahamiaji haramu Jijini Dar es Salaam. Mamia ya wakazi hao walimiminia katika ofisi hizo kujiorodhesha ikiwa ni agizo la Rais Jakaya Kikwete.
SEVERINA LWIGA ATWAA TAJI LA MISS TANZANIA PERSONALITY
FORM ONE GIRL CHARGED WITH MURDER OF LOVE
By WILFRED AYAGA
A 17-year-old Form One student in Nairobi is facing murder charges after allegedly stabbing her 22-year-old boyfriend.
The student was yesterday arraigned before Justice Roseline Korir and charged with killing her boyfriend at Kiamumbi Estate, Kasarani, over what the prosecution said was a misunderstanding over a phone call.
According to the police charge sheet, the student allegedly committed the offence on August 22 after they quarreled over a phone call that the girl had received a few days before the killing.
Although the girl claimed that the phone call was from her mother, the boyfriend did not believe her leading to the dispute that ended tragically.
“They had a domestic dispute over the call. She then grabbed a knife and stabbed him, killing him,” the court was informed.
pool of blood
A neighbour later found the deceased lying in a pool of blood outside the house. He died as he was being rushed to Kiambu District Hospital for treatment.
SOURCE: STANDARD MEDIA
MWALIMU MBARONI KWA KUBAKA WANAFUNZI WAKE WAWILI
MNAMO TAREHE 13.09.2013 MAJIRA YA SAA 21:30HRS HUKO KATIKA SHULE YA SEKONDARI MONTFORT WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ANDREW S/O SHADRACK, MIAKA 26,MKURYA, ALIYEKUWA MWALIMU WA SHULE YA SEKONDARI MONTFORT AKIFUNDISHA MASOMO YA LUGHA YA KIINGEREZA NA MASOMO YA DINI AMBAYE HIVI SASA NI MWALIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWEMBENI –MUSOMA MKOANI MARA ALIMBAKA, MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE SHULENI HAPO JINA LIMEHIFADHIWA, MIAKA
17, MHEHE . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMTOA DARASANI WAKATI AKIJISOMEA “PREPO” NA KUMPELEKA GIZANI KISHA KUMBAKA KWA NGUVU HUKU AKIMPA AHADI MBALIMBALI.
AIDHA MAJIRA YA SAA 22:00HRSKATIKA SHULE HIYO MWALIMU HUYO ALIMBAKA MWANAFUNZI MWINGINE WA KIDATO CHA NNE JINA LIMEHIFADHIWA, MIAKA 18, MPARE. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMUITA KUTOKA BWENI AKIWA AMEPUMZIKA NA KUMBAKA KWA NGUVU HUKU AKIMPA AHADI MBALIMBALI.
MTUHUMIWA ALIKUWA AKIWARUBUNI WAHANGA KWA AHADI MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA KUWAPA MSAADA KATIKA MASOMO KWA KUWA ATARUDI KATIKA SHULE HIYO MUDA SI MREFU KUSHIKA WADHIFA WA MWALIMU MKUU.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI LEO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA TAMAA ZA KIMWILI NA MADHARA YA KUFANYA MAPENZI [NGONO] ZEMBE KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO. AIDHA ANATOA RAI KWA WATU WAZIMA KUACHA TABIA YA KURUBUNI /SHAWISHI WATOTO WADOGO HUSUSAN WANAFUNZI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, BADALA YAKE WAWE WAAMINIFU KWA KUCHAGUA MWENZI MMOJA WA KUISHI NAE.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
ZANZIBAR POLICE ARREST 15 SUSPECT IN CONNECTION WITH ACID ATTACK
A senior Police Officer has said that suspected Islamist militants and other individuals linked to an acid attack on a clergyman, have been arrested in Tanzania's semi-autonomous Zanzibar islands, reports Reuters.
"Fifteen people have been arrested in police raids on criminal networks," "Among them are suspected members of al Shabaab, suspects behind the recent acid attack on a Roman Catholic priest and unlicensed acid distributors," Zanzibar's police commissioner, Mussa Ali Mussa, told Reuters.
All those arrested on Sunday were Tanzanian nationals, Mussa added.
Mussa did not say what the suspected militants were doing on the archipelago, though he said they were not linked to the acid attacks.
Mussa said prosecutors were close to laying charges against two other men detained in connection with the attack on Britons Katie Gee and Kirstie Trup. The young women suffered facial, chest and back injuries
CHADEMA KUMSHITAKI BALOZI WA CHINA UMOJA WA MATAIFA
CHADEMA iimesema itamshitaki Balozi wa China nchini, Lu Younqing Umoja wa Mataifa (UN) kwa kukiuka Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa mwaka 1964 ambao unaeleza uhusiano wa kibalozi kati ya nchi na nchi.
Aidha, kimesema kitaiandikia barua Serikali ya China ili kutaka ufafanuzi kama imemtuma Balozi wake kufanya kazi ya uenezi siasa kwenye vyama baada ya Balozi huyo kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CCM Septemba tisa mwaka huu kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Wilaya ya Kishapu Shinyanga, ambapo Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana alimtambushisha Balozi huyo huku akiwa amevaa sare za chama hicho.