Facebook Comments Box

Friday, June 7, 2013

KIEMBA: MIMI NI MCHEZAJI HURU NA BADO SIJASAINI YANGA

KWA mara ya kwanza, kiungo Amri Ramadhani Kiemba ameibuka na kukanusha kusaini Yanga SC, ingawa amesema yeye bado mchezaji huru, kwa kuwa hadi sasa hajasaini timu yoyote baada ya kumaliza Mkataba wake Simba SC. Akizungumza  Kiemba alisema kwamba hajasaini timu yoyote hadi sasa na anajitambua kama mchezaji huru. Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, Kiemba alisema kwa sasa akili yake ipo kwenye kuisaidia timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iweze kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia. “Sasa hivi ukiniuliza mambo ya klabu, utakuwa unanionea tu. Nipo katika kambi ya timu ya taifa, fikra zangu ni majukumu yangu ya kitaifa. Nadhani baada ya hapa, nitazungumzia hayo mambo,”alisema Kiemba. Kiemba aliibua wasiwasi mkubwa kwa wapenzi wa Simba SC, baada ya kuvuma kwa habari amesaini Yanga SC, huku Mkataba wake ukiwa umemalizika Msimbazi. Na anaonekana mtu asiye na wasiwasi kabisa kuhusu mustakabali wake- pengine inatokana na kiwango chake cha juu hivi sasa. Stars inashika nafasi ya pili katika Kundi C, kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwakani Brazil, ikiwa na pointi sita nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, ambayo kesho itakuwa ugenini ikimenyana na Gambia katika mchezo mwingine wa kundi hilo. Stars ilitua hapa Jumatatu ikitokea Ethiopia ambako iliweka kambi ya wiki moja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan, ulioisha kwa sare ya bila mabao. Kabla ya kuja hapa, Stars iliweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ikijifua Uwanja wa Karume na siku chache kabla ya kuondoka ilialikwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, aliyewapa hamasa kwa hotuba nzuri.

SOURSE: BIN ZUBEIRY


MWANAMKE AFARIKI AKIJARIBU KOTOA MIMBA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani akizungumza na mwandishi wa Mtandao Huu bwana Prosper Mfugale Juu ya Tukio Hilo.
Mkazi Mmoja wa Mtaa wa Idundilanga Mjini Njombe Yasinta Mdetele Mwenye Umri wa Miaka 25 Amefariki Dunia Wakati Akijaribu Kutoa Mimba.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kusema Kuwa Tukio Hilo Limetokea June Tano Mwaka Huu Majira ya Saa Tatu Asubuhi Baada ya Kunywa Kinywaji Kinachodaiwa Kuwa na Sumu.
Amesema Marehemu Alikutwa Chumbani Kwake Akiwa Amefariki Huku Pembeni Yake Kukiwa na Mtoto wa Kike Ambae Pia Alikutwa Amefariki na Kuongeza Kuwa Marehemu Hakuacha Ujumbe Wowote na Hakuna Mtu Yoyote Anaeshikiliwa Kutokana na Tukio Hilo.
Ameongeza Kuwa Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi wa Tukio Hilo na Kutoa Wito Kwa Wananchi Kuacha Vitendo Vya Utoaji Kwani ni Kosa la Kisheria na Pia Linaweza Kuhatarisha.


Thursday, June 6, 2013

PICHA M TO THE P AKIMUAGA MANGWEA MOROGORO LEO




MAREKANI WAANDAA SHERIA ITAKAYO KATAZA WATU KUVAA MLEGEZO


Sina shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume zenye majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa majina lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio.
Kama ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha miili yao hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa wakilalamikiwa kwa style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana wadogo ambao bado wako shuleni.
Katika hali ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya makalio uongozi wa Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria mpya itakayoweza kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa mlegezo na kukatiza mitaani.
Sheria hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali, kaptura, mavazi ya kuogelea na sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni mwa mvaaji.

Mayor wa Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia waandishi wa habari kuwa amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana wanaotembea makalio nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.


HII NDIO KAULI YA M 2 THE P BAADA YA KUFIKA TANZANIA KUMZIKA MANGWEA


 Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya leo (June 6).Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2 The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake Mangwea. “Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi, asanteni,” alisema. Msikilize hapa 


PICHA ZA UTOAJI WA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU MANGWEA MOROGORO

Meza kuu hii ikiwa ni maandalia ya kuuwaga mwili wa msanii marehemu Albert Mangwea aliyefariki dunia na anatarajiwa kuzikwa leo mkoani morogoro.Utaratibu huu umeandaliwa katika uwanja wa jamuhuri mkoani morogoro kwa lengo la kuwapa fursa wakazi wa mji huo kupata nafasi za kuuwaga mwili huo kabla ya maziko

Umati mkubwa wa wakazi wa morogoro waliojitokeza katika zozi za kuwaga mwili wa msanii huyo mchana huu kabla ya maziko yake leo.Marehemu albert mangwea alifariki wiki iliyopita nchini afrika kusini na maziko yake yatafanyika leo mkoani hapa.


 Mama Mzazi wa Mangweha, Denisia Mangweha akiwa nyumbani kwake kabla ya safari kuelekea Uwanja wa Jamhuri.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiwasili nyumbani kwa Mama mzazi wa Mangweha.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera asubuhi hii amefika nyumbani kwa Mama Mangwea eneo la Kihonda Mazimbu Road na kumpa pole kwa niaba ya wakazi wote wa mkoa wa Morogoro. Baada ya kutoa pole, Mhe. Bendera aliongoza umati wa watu kutoka Kihonda kuelekea Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli za kuaga mwili wa Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei 28 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Mangwea anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kihonda nje ya Kanisa la Mtakatifu Monica jirani kabisa na alipozikwa baba yake mzazi Mzee Keneth Mangwea.
943280_10152915710755525_916679441_n
 Wakazi wa mjo wa morogoro waanza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu albert Mangwea kabla ya kumpeleka katika Nyumba yake ya Milele. Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala Pema.




MAJANGA YAZIDI MUANDAMA MR. NICE SASA MKATABA WAKE NA GRAND PA RECORDS YA KENYA WAVUNJWA


Mwanamuziki aliyevumbua staili ya muziki ya TAKEU (Tanzania Kenya Uganda), Mtanzania Lukas Mkenda aka Mr Nice amepoteza mkataba wake na kampuni ya kurekodi muziki ya nchini Kenya, kwa kile kilichoelezwa na kampuni hiyo kuwa ni tabia ya Mr Nice ya uvivu, ulevi, asiyeaminika na asiye na ushirikiano. 
Zaidi ya maandishi yaliyoandikwa na GrandPa Records kwenye ukurasa wao wa Facebook, pia wamezungumzia suala hilo walipohojiwa na kituo cha EA Radio ambapo wamesema Mr Nice amesema ataendelea kubaki mjini Nairobi nchini Kenya akitafuta kujiweka sawa. 



Wednesday, June 5, 2013

KOCHA WA YANGA AWASILI KWA AJILI YA KUINOA TIMU KWA AJILI YA MSIMU MPYA

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Ernie Brandts (kulia) baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam usiku wa leo akitokea kwao Uholanzi kwa mapumziko mafupi baada ya kumaliza msimu, tayari kuanza maandalizi ya kikosi chake kwa msimu mpya. Aliyemlaki kushoto ni Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh.

Anaondoka Airport 

Baada ya kutua, kitu cha kwanza aliwasha simu yake

Anafungua mlango wa gari lake apakie mizigo

Anafungua mlango wa nyuma apakie mizigo

Hahitaji msaada wa mtu, anapakia mwenyewe

Anafunga mlango baada ya kupakia

BIN ZUBEIRY anaondoka baada ya kumaliza kazi yake

Brandts naye anapanda gari lake

Anapiga stata...


Anaondoka Airport 


POLISI WATUMIA MBWA KUTAWANYA WATU LEADERS BAADA MUDA WA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KUISHA

Asakari Polisi wakitumia mbwa kutawanya maelefu ya watanzania waliotaka kuuaga mwili wa Mangwea baada ya muda uliopangwa kukamilika
ASKARI wa Jeshi la Polisi walilazimika kutumia Mbwa kuwatawanya mamia ya Watanzania waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea lakini wakashindwa baada zoezi hilo kukatishwa.
Mangewa alifariki Dunia nchini Afrika Kusini katika Jiji la Johannesburg Mei 28 mwaka huu na kusafirishwa kuja nchini jana jioni, mamia hao wa watanzania wameshindwa kuuaga mwili wa kipenzi chao baada muda ulioapngwa kukamilka huku wakibaki katika foleni ndefu.
Kitendo cha Kamati ya maandalizi kukatisha zoezi la kuuaga mwili wa marehemu kwa sababu ya muda uliopangwa kukamilika iliwashangaza mamia ya watu waliokuwa kwenye foleni ya kusubiri kupata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho mbele ya Jeneza la Mangwea.
Zoezi hilo liloanza saa 2:30 asubuhi imesitishwa saa 6:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki na Kati, na msafara ukiongozwa na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama waliokuwa katika Viwanja vya Leaders Club.
Barabarani Asakari wa Kikoso Cha Usalama Barabarani pia walijiapanga vizuri kuhakikisha kwamba msafara wa mwili wa marehemu unapita vizuri katika maeneo yaliokuwa yamepangwa kuelekea mjini Morogoro.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr Blue alifika katika viwanja hivyo akiwa amechelewa na kukosa muda wa kuuaga mwili wa Mangwea lakini alipokutana na mashabiki wa muziki wake aliweza kusimama na kuwapa pole.
Mwili wa Mangwea hivi sasa uko safarini kuelekea Mjini Morogoro ambapo utalala nyumbani kwa mama yake na kesho uwakazi wa Mji huo pia watapata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU