ASKARI wa Jeshi la Polisi walilazimika kutumia Mbwa kuwatawanya mamia ya Watanzania waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea lakini wakashindwa baada zoezi hilo kukatishwa.
Mangewa alifariki Dunia nchini Afrika Kusini katika Jiji la Johannesburg Mei 28 mwaka huu na kusafirishwa kuja nchini jana jioni, mamia hao wa watanzania wameshindwa kuuaga mwili wa kipenzi chao baada muda ulioapngwa kukamilka huku wakibaki katika foleni ndefu.
Kitendo cha Kamati ya maandalizi kukatisha zoezi la kuuaga mwili wa marehemu kwa sababu ya muda uliopangwa kukamilika iliwashangaza mamia ya watu waliokuwa kwenye foleni ya kusubiri kupata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho mbele ya Jeneza la Mangwea.
Zoezi hilo liloanza saa 2:30 asubuhi imesitishwa saa 6:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki na Kati, na msafara ukiongozwa na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama waliokuwa katika Viwanja vya Leaders Club.
Barabarani Asakari wa Kikoso Cha Usalama Barabarani pia walijiapanga vizuri kuhakikisha kwamba msafara wa mwili wa marehemu unapita vizuri katika maeneo yaliokuwa yamepangwa kuelekea mjini Morogoro.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr Blue alifika katika viwanja hivyo akiwa amechelewa na kukosa muda wa kuuaga mwili wa Mangwea lakini alipokutana na mashabiki wa muziki wake aliweza kusimama na kuwapa pole.
Mwili wa Mangwea hivi sasa uko safarini kuelekea Mjini Morogoro ambapo utalala nyumbani kwa mama yake na kesho uwakazi wa Mji huo pia watapata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog