Facebook Comments Box

Monday, August 18, 2014

WAYAHUDI WAANDAMANA WAKIPINGA MYAHUDI KUOLEWA NA MUARABU

Maandamano ya kupinga ndoa ya myahudi na muarabu nchini Israel

Wayahudi wanne wenye msimamo mkali wamekamatwa nchini Israeli baada ya kuzua rabsha katika sherehe ya kuadhimisha harusi ya mwanamke myahudi aliyebadili dini na kuwa Muislamu na kisha kuolewa na mwanamume Mwarabu raiya wa Israeli. Mamia ya watu waliandamana nje ya ukumbi uliotumika kwa
sherehe hiyo katika mji wa Rishon LeZion Jumapili wakipinga ndoa hiyo licha ya kuwepo kwa maafisa wa Usalama. Bwana harusi, Mahmoud Mansour, alikuwa amechukua hati ya
mahakama ya kupinga kufanyika kwa maandamano ya kupinga nikah yake lakini maafisa wa usalama wakashindwa kuzima maandamano hayo.

Maandamano ya kupinga ndoa hiyo

Rais wa Israeli Reuven Rivlin amekashifu upinzani dhidi ya ndoa hiyo. Muungano wa wayahudi wenye msimamo mkali Jewish Lehava walipewa ruhusa ya kuandamana kupinga ndoa hiyo ilimradi tu wasikaribie chini ya mita 200 karibu na ukumbi wa sherehe hiyo. Kundi hilo linapinga ndoa kati ya Wayahudi na Waarabu.

Waandamanaji wanne walikamatwa na polisi kwa kukiuka masharti yao kulingana na mtandao wa habari wa kiyahudi.Sadfa ni kuwa kundi lingine linalounga mkono ndoa kati ya Waarabu na Wayahudi lilifanya maandamano kuunga mkono ndoa hiyo na hivyo kuwalazimu maafisa wa usalama kufanya kazi ya ziada kuzuia makabiliano baina ya makundi hayo hasimu.

Polisi wakiwadhibiti waandamanaji

Bi Harusi Morel Malka, alikuwa amewaalika wageni 500 katika hafla hiyo. Bi Malka, 23, alikuwa amesilimu kabla ya sherehe hiyo kuambatana na desturi za kiislamu. "Kwa kweli tunaishi pamoja kwa amani na sielewi kwanini ndoa hii inawahusu watu." alisema bwana Mansour, 26. Rais Rivlin alifananisha maandamano hayo dhidi ya ndo hiyo na ''panya anayengata msingi wa unaoliunganisha taifa hilo la Israeli''.

 CHANZO: BBC SWAHILI


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU