Facebook Comments Box

Monday, August 18, 2014

MAHAKAMA YAMWACHIA MANSOUR HIMID KWA DHAMANA

Mahakama ya Mkoa,Vuga imempatia dhamana aliekuwa waziri wa zamani wa serikali ya Mapinduzi (SMZ),Mansour Yussuf Himid anaetuhumiwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume na sheria ya Zanzibar, baada ya kupata maelekezo kutoka Mahakama kuu.
Hakimu Khamis Ramdhani ametoa dhamana hiyo leo baada ya kutakiwa kusimamia maamuzi yakupatiwa dhamana yaliotolewa na Mahakama kuu chini ya Jaji Abraham Mwampashe kufuatia kusikilizwa kwa ombi la dhamana lililowasilishwa Mahakama hapo na mawakili
wanaomtetea Mh.Mansour.
Mapema Jaji Abraham Mwampashe, akitoa dhamani hiyo, amesema Mahakama yake imeangalia hoja za kisheria zilizotolewa na pande zote mbili za muombaji na mpigaji dhamana zilizowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa pande zote mbili. Jaji mwampashe amesema kutokana na kifungu cha sheria cha (150) kifungu kidogo cha nne(4) sheria No (7 )ya mwaka (2004) sheria ya Zanzibar,kinaipa uwezo Mahakama kuu kutoa dhamana kwa mtuhumiwa ikiwa itaridhika na hoja zilizowasilishwa.
“hakuna kosa lolote lisolokua na dhamana,kifungu kidogo cha nne (4) kiko wazi kimeeleza Mahakama kuu ina uwezo wa kutengua makosa yote yaliokuwa hayana dhamana ikiwa itajiridhisha kama yalivyoorodhesha katika kifungu kidogo cha kwanza” Alisema Mwampashe.
Amesema baada ya kuangalia hoja za kisheria pia amechanganya na akili zake mwenyewe kwa kuangalia faida na hasra za mtuhumiwa kuwepo nje na kuwepo kizuizini. Amesema gharama za kumhudumia na kumleta Mahakamani mtuhumiwa kunaitia hasara jamii ,hivyo Mahakama hiyo haioni sababu ya mtuhumiwa kuendelea kubaki kizuizini. Mwampashe amesema hasa akiangalia mtuhumiwa hana historia ya uhalifu,pia mtuhumiwa anamajukumu ya kuendesha biashara zake ambazo kunafaida ya ajira kwa vijana walioajiriwa hapo katika vitega uchumi vyake.

Amesema Mahakama hii haiwezi kumyima mtu dhamana bila ya kuambiwa sababu ya msingi kuwepo kwake nje kuweza kuathiri mwenendo mzima wa kesi yake. Pia amefahamisha kwamba endapo Mahakama kuu itamnyima mtuhumiwa dhamana,huku kesi inaendelea na kufikia kufutwa au mtuhumiwa kushinda kesi, jamii inayomzunguka wataingia hasara ikiwemo kukosa huduma muhimu kutoka kwa ndugu
wanaemtegemea.
Aidha Jaji Mwampashe ametowa masharti ya dhamana kwa mtuhumiwa huyo kutoa dhamana ya shilingi milioni tatu tasilim za Tanzania, wadhamini wawili wanaoaminika kwa kusaini dhamana ya milioni tano za maandishi, kwa kila mmoja. Pia mtuhumiwa huyo alitakiwa kukabidhi Mahakamani hapo hati zake za kusafiria, pia hatoruhisiwa kutoka nje ya Nchi bila ya kuiarifu
Mhakama.
Wakati huo, huo Hakimu Khamis Ramadhani alihairisha kesi mama inayomkabili mtuhumiwa huyo hadi Agosti 28,mwaka huu na mtuhumiwa yuko nje baada ya kutimiza masharti yote ya dhamana.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU