Pichani ni mmoja wa Mtambo wa kuzalisha umeme ambao ni miongoni mwa mitambo itakayotumiwa katika kuzalisha kiasi cha megawati 150 za umeme katika Mradi wa Kinyerezi I. |
Washirika wa Maendeleo kutoka taasisi mbalimbali nchini waliotembelea Mradi wa kuzalisha Umeme wa Kinyerezi I na kituo cha kupokea Gesi wameeleza kufurahishwa na kuridhika na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.
Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier, akiongea kwa niaba ya washirika hao ameeleza kuwa, wameridhishwa na hatua ambazo miradi hiyo imefikia na kupongeza jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba inafanyia kazi changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika Tanzania. Pia Dongier ameitaka Serikali kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme ili iweze kufikia lengo lake la kuhakikisha Tanzania inazalisha umeme wa kiasi cha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza wakati ujumbe huo ulipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 na kituo cha kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim ameeleza kuwa, Wizara imeona ni jambo la msingi kwa wadau hao kutembelea miradi hiyo ili kujionea hatua mbalimbali ambayo miradi hiyo imefikia.
Aidha, Maswi ameongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imedhamiria kuleta mabadiliko ya kiuchumi kupitia sekta ya nishati hususani kupitia gesi asilia na kuongeza kuwa, hakuna kinachoshindikana hivyo, miradi hiyo inatarajiwa kukamilishwa kwa wakati kama ilivyopangwa.
Kwa mujibu wa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba, ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo cha kupokea gesi cha Dar es Salaam umekamilika kwa asilimia 60. Naye Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Mhandisi, Saimoni Jilima ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho umekamilika kwa asilimia 70.Washirika wa Maendeleo waliotembelea miradi hiyo ni pamoja na Benki ya Dunia, GIZ, USAID, MCC, Korea Exim Bank, Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB),DFID, Umoja wa Ulaya,Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Ujerumani na Ubalozi wa Ufaransa
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog