Facebook Comments Box

Monday, April 21, 2014

MZEE WA MIAKA 61 AKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI MBEYA


Majirani wakimuhudumia majeruhi
NA Ezekiel Kamanga,Ileje Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la London Haonga(61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya
Mbebe Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya amejeruhiwa vibaya kwa
kukatwa nyeti zake na watu watatu wasiofahamika kisha
kutokomea nazo kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku April 19 mwaka huu
baada ya mmoja kati ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee
huyo kisha kubisha mlango akiomba msaada wa kuonyeshwa njia
akidai amepotea njia.
Mzee London alipotoka nje ya nyumba akiwa anamwelekeza njia
mtu huyo anayedaiwa kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka
nyumbani kwake alifunikwa na kitambaa usoni na watu wawili
kisha kuangushwa na kukatwa nyeti zake ambazo waliondoka
nazo.
Mtendaji wa Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga amesema baada
ya unyama huo Mzee London alipoteza fahamu na alipozinduka
alipiga yowe kuomba msaada ambapo majirani walifika na kutoa
msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Ileje huku
wakiwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa watuhumiwa wa
tukio hilo wanatokea Mpemba wilaya ya Momba ambao
walitambuliwa na mhanga wa tukio hilo ambapo baada ya kupewa
PF 3 mzee London amekimbizwa Hospitali ya Rufaa Mbeya
ambapo alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa 11:00 jioni
April 20 huku akilalamika kwa maumivu makali.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed
Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa
chanzo cha awali imedaiwa sababu za kutendewa ukatili huo
umetokana na mmoja wa ndugu aliyedai kuwa mzee huyo
anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mdogo
wake hivyo watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.
Aidha imedaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine
kudai kuwa tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina kwani
imedaiwa watuhumiwa kuimbilia nchi jirani mara baada ya kutenda
kitendo hicho cha kikatili.
Kamanda Msangi ameoa wito kwa jamii kuacha tabia za
kujichukulia sheria mkononi amesema pindi wanapokuwa na
migogoro ni vema kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo ili
kuleta amani na kuahidi wale wote waliohusika na tukio hili
wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwani
hakuna mtu aliye juu ya sheria.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU