Klabu ya Manchester City imemaliza
rekodi ya Evertonkutofungwa katika Ligi Kuu ya England, baada ya
kuifunga mabao 3-1 jioni hii.
Aston Villa na Bayern Munich Ziliwafanya City waingie kwa hasira leo na kipa wao Joe Hart na
kufanya kweli Uwanja wa Etihad Stadium
Romelu Lukaku aliifungia Everton bao la
kuongoza dakika ya 16, lakini Alvaro Negredo akasawazisha dakika moja
baadaye na Sergio Aguero akafunga la pili kabla ya mapumziko.
Tim Howard akajifunga dakika ya 69, akitoka tu kuokoa penalti ya Aguero.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Hart,
Zabaleta, Kompany/Nastasic dk35, Lescott, Kolarov/Clichy dk58, Toure,
Fernandhino, Milner, Negredo, Silva, Aguero/Nasri dk78.
Everton: Howard, Coleman,
Jagielka, Distin, Baines, Mirallas/Deulofeu dk62, McCarthy, Naismith,
Osman/Gibson dk62, Barkley, Lukaku/Kone dk82.

Sergio Aguero akishangilia bao

Romelu Lukaku

Alvaro Negredo





Joe Hart



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog