Watu ambao hawajabainishwa wamempiga risasi na kumuua kiongozi
wa Kiislamu aliyeuawa Sheikh Aboud Rogo, Sheikh Ibrahim Rogo pamoja na wenzake
watatu usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe 04-10-2013.
Sheikh Ibrahim Rogo na wenzake wanne walikuwa wakielekea
nyumbani kutoka Masjid Musa kwa ajili ya ibada ndipo gari yao ilipomiminiwa
risasi zilizowaua wanne kati ya watu waliokuwa katika gari hiyo kwenye umbali
wa nusu kilometa kutoka kituo cha polisi cha Bamburi.
Wengine waliokuwa katika hiyo gari ni bwana Gadaffi
Muhammad anayesemekana kuwa fundi seremala, bwana Issa Abdalla shemeji wa Gadaffi
na ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha hiyo gari, Omar Abu Rumeisa na Salim Aboud
ambaye alipona kimaajabu katika shambulizi hilo baada ya kujifanya kuwa amekufa.
Salim Aboud anasema kuwa walikuwa wakielekea nyumbani
katika gari aina ya Toyota Fun Cargo ndipo watu waliokuwa wakitembea walianza
kuishambulia gari yao kwa risasi na kuacha njia.
“Tumewamaliza,” Bwana Salim Aboud aliwasikia wakisema
baada ya yeye kujifanya kuwa amekufa. Wauaji wanasemakana kutumia gari aina ya
Mark X kutoka katika eneo hilo.
Viongozi kadhaa wa Kiislamu, akiwemo Sheikh Abubakar
Sheriff anayejulikana kwa jina la Makaburi ambaye alifika katika eneo hilo
baada ya tukio, alikinyooshea kidole Kikosi Maalumu cha Polisi cha Kupambana na
Ugaidi kuwa ndicho kilichohusika na mauaji hayo.
“Kikosi cha ATPU kilikuwa hapa, kwa nini wamekimbia? Tumefanya
nini na kwa nini wanatuua? Hatujamuua yeyote lakini polisi wanawaua Waislamu
wasiokuwa na hatia,” alisema Sheikh Makaburi.
“Vitendo hivi vinaongozwa na Wamarekani na Waisraeli, Sheikh Ibrahim hakuwa katika Jengo la Westgate wakati wa shambuli kwenye jengo hilo. Serikali za Kimagharibi hawataki Waislamu wazungumzie Jihad. Jihad ni sehemu ya Uislamu, tuuweni sote,” alisema.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog