Facebook Comments Box

Saturday, October 5, 2013

TWENTY PERCENT NA MAN WALTER WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Twenty Percent akiwa ameshikana mikono na Man Walter mara baada ya kupatana.

Hatimaye bifu kali kati ya msanii aliyewahi kutwaa tuzo 5 nchini za KTMA na kuvunja rekodi TWENTY PERCENT (kushoto) na aliyewahi kuwa Producer wake na pia ni mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki nchini KTMA  2012 MAN WATER (kulia) limemalizika rasimi leo kwa wawili hao kukutana nakumaliza tofauti zao.

Man Water na 20% walikutana leo katika studio za Magic fm na Channel Ten ambapo wawili hao wamekubaliana kufanya kazi tena pamoja na kusahau yaliyopita.

Akizungumzia kiundani kuhusu tofauti zao Man Water alisema tatizo lilikua ni kutoelewana au kupishana kidogo kwa kauli ambazo leo walizimaliza na hatimaye kuweka mikakati mipya ikiwemo ya kufanya kazi pamoja kwa makubaliano maalumu.

Kwa upande wake 20% amesema tofauti zao hazikuwa za msingi bali ni kupishana tu kwa kauli na sasa yuko tayari kufanya kazi pamoja na Man Water.

Inaaminika kwamba kufanya kazi pamoja kwa wawili hao kuna maana kubwa kutokana na kuwezana na kuelewana katika kazi zao mbalimbali walizowahi kufanya ikiwemo kazi ya Yanini malumbano,Tamaa mbaya,Mama Neema na nyinginezo.
Peace And Love
Chanzo: Michuzi


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU