Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. |
BUNGE nchini Uganda limetumia zaidi ya dola 377,000 kununa kompyuta aina ya iPad kwa ajili ya wabunge wote .
Maofisa wa bunge hilo walisema kuwa mbali na
kuwaweka wabunge hao karibu na ulimwengu wa teknolojia, wanatarajia
kuwasaidia kupunguza gharama za fedha zinazotokana na matumizi ya
uchapishaji wa nyaraka mbalimbali.
Kamishna wa bunge hilo Elijah Okupa alisema kuwa kompyuta hizo ni bora na zinafaa kwa matumizi hivyo ni vyema zikatumiwa vizuri.
Alisema iPad hizo zitakuwa ni mali ya wabunge
lakini kama mtu atatumia kwa muda wa miaka mitano asitegemee itakuwa na
ubora uleule wa kumwezesha mwingine atumie kwa miaka hiyo alisema Okupa
Kwa mujibu wa takwimu kutoka katika bunge hilo
zilionyesha Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya dola 12 katika miaka
miwili sasa kwa ajili ya mahitaji ya kama kompyuta, uchapishaji wa
nyaraka, mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kuwa bora katika
bunge.
Kwa mujibu wa mbunge kutoka mashariki, Medard
Segona alisema kuwa kutokana na uwepo wa ipad hizo wanategemea kupunguza
matumizi ya fedha zilizokuwa zikipotea hapo awali.
‘’Vifaa hivyo vitapunguza sana matumizi ya fedha
kwa kuwa hapo awali wizara ya fedha ilikuwa ikichapisha zaidi ya nyaraka
400 kwa kila mbunge na maofisa wengine waliopo ndani ya bunge
hilo’’alisema
Aliongeza kuwa komputa hizo ni muhimu kwa utendaji kazi hasa katika kipindi hicho cha kuendeleza matumizi ya teknolojia.
Hata hivyo taarifa zilisema kuwa wabunge hao bado
hawana uelewa mzuri juu ya matumizi hayo licha ya kuwa kampuni imeahidi
kutoa mkataba wa mafunzo ambayo pia yatasaidia kupunguza gharama za
matumizi.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog