Facebook Comments Box

Wednesday, August 20, 2014

E-FM YAENDELEA KUIBOMOA ITV/R.ONE BAADA YA KITENGE, YAMCHUKUWA KATANGA

Omar Katanga

Katanga

Aliyekuwa mtangazaji wa Radio One,OMARY KATANGA (mlinda mlango no.1) hatimaye leo amejiunga na kituo kipya cha radio(E.FM) kinachorusha matangazo yake toka mikocheni Jijini Dar es salaam.

Katanga ametangaza kupitia katika ukurasa wake wa facebook kuwa amejiunga na E - fm.

Bila shaka wapenzi wa kipindi hicho watahama na watangazaji hao maana kipindi ndiyo kama kimevunjwa kabisa kwa kuwachukuwa waendeshaji wake maarufu ambao wamejizolea sifa hapa nchini.

"WAUNGWANA: WENGI MMEKUWA MKINIULIZA MBONA HAMNISIKII KWENYE KIPINDI CHA SPOTI LEO-NICHUKUE FURSA HII KUWAJULISHA KWAMBA HAMTANISIKIA TENA RADIO ONE KUANZIA IJUMAA ILIYOPITA AGOSTI 15,2014.

KWA UWEZO WA MUNGU MTANISIKIA TENA.......POLENI KWA USUMBUFU LKN....ASANTENI KWA USHIRIKIANO WENU."

Hayo ni maneno aliyo andika Omar Katanga kwenye ukurasa wake wa face book.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU