HALI ya taharuki imetanda katika mitaa mbalimali nchini Afrika Kusini kufuatia hali ya Rais wa kwanza mweusi nchini humo, Nelson Madiba Mandela (94) kuwa mbaya na kukata kauli.Taharuki hiyo imetokea baada ya Ikulu ya Afrika Kusini kutangaza kwamba afya ya kiongozi huyo ni mbaya kuliko siku mbili zilizopita,huku taarifa za ndani ya Serikali ya Afrika Kusini zikidai kwamba Madiba hajafungua macho wala kuzungumza chochote kwa wiki moja sasa.Hata hivyo taarifa hiyo ilithibitishwa jana na Rais Jacob Zuma ambaye kwa mara ya kwanza alikiri hadharani kwamba hali ya afya ya Mandela ni mbaya na madaktari wanaendelea na juhudi za kuokoa maisha yake.Zuma ambaye pia ni Rais wa Chama cha African National Congress (ANC), alikiri kufadhaishwa na hali ya kiongozi huyo wa zamani, alipomtembelea katika Hospitali ya Magonjwa ya Moyo ya Medi-Clinic mjini Pretoria na kuzungumza na mkewe, Graca Machel kuhusu hali yake.Hata hivyo Afisa mmoja kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania ameidokeza Habarimpya.com kwamba Serikali ya nchi hiyo ina wakati mgumu huku kila idara ikitakiwa kuwa tayari kwa lolote na kwamba mara watakaposikia taarifa za kifo cha mwasisi wa taifa hilo waanze kufanya maandalizi ya haraka ya kupokea msiba huo mzito.Mbali na hilo Henry Masanja ni mtanzania anayeishi nchini Afrika Kusini akizungumza na Habarimpya.com kwa njia ya simu akiwa Pretoria alisema kwamba, Hali si shwari katika miji mbalimbali ya nchi hii"."Wananchi wote wameshakata tamaa ya kupona kwa kiongozi wao, huku wengine wakiamini kwamba pengine ameshafariki dunia kwa sababu yuko kwenye mashine na hawezi kuzungumza chochote kwa siku kadhaa wala kufungua macho,hivyo Serikali imeamua kutangaza kuwa afya ya Madiba ni mbaya ili wapate muda wa kufanya maadalizi ya kuitaarifu dunia juu ya kifo cha Madiba alisema Masanja.
SOURSE: HABARI MPYA
SOURSE: HABARI MPYA
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog