
Mtangazaji wa televisheni ya Chanel 5 EATV Joyce Kiria akiwa 
amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo kulia na Lincorn wakati 
alipozungumza na waandishi wa habari katika mtaa wa Samora na kupaza 
sauti kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili
 kusaidiwa na kujua aliko mume wake Henry Kileo ambaye inadaiwa 
amepelekwa Igunga akituhumiwa na kesi huko Joyce Kiria amesema mpaka 
sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa 
anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa
Bw.Henry
 Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili
 wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara 
ya kwanza 
 
 Wanachama
 wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi 
ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na 
kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni 
za
 uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika 
msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga. 
 
Kamanda
 Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na wtuhumiwa wenzake wanne 
wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena 
Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2012.