MBUNGE wa Mbeya Mjini
Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa
kwa dhamana.
Mwandishi wetu akiwa
Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi
baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.
Sugu alikamatwa na
kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa
kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano
mengine.
Hata hivyo taarifa za
awali za tukio la kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na
Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na kosa la kutoa maneno ya
uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mizengo Pinda.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog